Habari,
Binafsi nimefurahiswa sana na maamuzi ambayo TBC inataka kuyachukua.
Kwanza kabisa;
Kumbukeni hiyo ni Station ya Taifa hivyo ina watazamaji wa kila namna, so kuzingatia maadili ni jambo la muhimu sana.
Pili;
Miaka hii wananchi wamegawanyika, Jambo litakalowateka na kuongeza watazamaji ktk station yenu ni kufanya mabadiliko ya kushangaa, Namaanisha.. Kwa kuwa imeshazoeleka kwa kurusha Events za CCM pia ianze kurusha na za vyama pinzani.
Je, mtalifanyaje hili..?
JIBU NI:
• Hakikisheni mnaongea na Uongozi wa vyama hivi kwanza, yaani mjadili na kujua ni tukio gani au mada gani mtakayokuwa mnairusha hewani na kama ina tatizo basi mliweke sawa kabla ya siku husika, hivyo mfanye malema uratibu wa vipindi vyenu mapema na iwe hivi hata kwa chama tawala pia.
Kwa kufanya hivi, hakika Mtarudisha matumaini kwa wananchi na kuanza kuwa watazamaji wakubwa wa vipindi vyenu.
• Pia, ongeeni na bunge mrudishe tena Bunge Live au baadhi ya mijadala na mingine itangazwe rasmi na bunge kuwa ni Siri Za Nchi hivyo haipaswi kurushwa live, naamini watanzania wote watalipokea vizuri na kufurahishwa na bunge,
Again, fanyeni uratibu wa vipindi mapema na setting za Camera pamoja na mitambo ya kurusha live mapema kabla ya bunge kuanza rasmi.
TATU;
Bei za kurusha matangazo kwenu ziwe kama bure kabisa, hii itawasaidia kuongezeka kwa wadhamini wa vipindi na kuwa station pekee hapa nchi yenye matangazo mengi especially kwa wajasiliamali wadogo wadogo na wawekezaji wa hapa nchini kwetu.
NNE:
Kumbukeni hicho ni chombo cha Burudani basi watangazaji wake wawe ni Vijana wenye Talent, Graphic za TBC ni mbaya sijawahi kuona, hivyo mnahitaji kuwaajiri vijana watakaokuwa wanaenda sambamba na Graphic za Wasafi Tv hali kadhalika na Clouds Tv ambazo zimekaa kisasa zaidi.
TANO;
Ombeni serikali iwekeze kwenu pesa ya kutosha, naamini hata serikali ikisema imetoa Billion kadhaa ili kuboresha Kituo Cha Habari Cha Taifa kiwe cha kisasa naamini hata wananchi wataunga mkono na kumpongeza JPM maana wamechoshwa mno na kituo hicho.
• Hivyo, Ajirini kwanza vijana kwa zaidi ya 90% then muweke kikao na kujadili mnahitaji vifaa gani vya kisasa, Camera zipi za kisasa, Magari ya matangazo na kufungua angalau branch 1 moja kwenye kila mkoa.
Waiteni hata wazungu wawafungie Mitambo hiyo the nitawapa Idea za Vipindi vitakavyokuwa bora zaidi.
Sent using
Jamii Forums mobile app