TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Upya wa utendaji kazi au upya wa vitendea kazi?
 
Ivi hii ni television ya taifa au ya ccm?
 
TBC mpaka iwe mpya sio rahisi.
1. Mwandaaji na aina ya vipindi ni vya kizee mno. Ubunifu ni zero.
2. Mnavaa kama madereva na sio watangazaji. Mnekukula mmenenepeana haswa wanawake ni vipipa. Hao rudisha nyuma kuandaa na kuongoza vipindi. Eleweni kutangaza kwenye tv ni zaidi ya kazi ya PR. Muonekano ndio branding. Get people with best voice and appearence plus brains. WAPO TELE.
3. Hamjaweza tumia teknologia ipasavyo. Quality ya video zenu inasikitisha. TV ya Taifa? No way. Mnashindwaje na madogo kama ayo, itv nk ?
4. Wekeni channels tofauti. Say TBC 1 huko wekeni watu wa serikali na programme za kuisifu serikali. Fine. TBC 2 ya biashara na programme zilizochangamka za vijana, kisasa, nk
TBC 3 say International hii ni ya utalii na kwa kiingereza. Huko unaiuza Tanzania duniani na sera ya viwanda na ipatikane free duniani kote na balozi zetu na airport zote na portal zote kubwa. Weka vivutio, mahoteli, mbuga, na quality ya picha iwe ya kimataifa.
5. Hiyo serikali mtandao ionekane kimataifa. Mambo ya passport, viza, uwekezaji na fursa. Wawepo watu wanaojua lugha na sio kiingereza cha kihaya.[emoji2][emoji1]
 

Huu ni ushauri bora kabisa... Plus muonyeshe shughuli za kitaifa ikiwemo BUNGE
 
Jf wengi ni wadau wa kile chama hivyo comment za kuvunja moyo puuza.
1. Mimi kuanzia kimuonekano, rangi zenu sio nzuri. Yaani hata nikiiangalia tbc ktk king'amuzi cha dstv bado muonekano haivutii.
2. Jaribuni kuvuta watu kwa kuonyesha vipindi vya michezo hasa mpira wa miguu na mieleka. Ikiwezekana wwe tena sio mechi za zamani na pia ligi tofauti kama za Tz, uk, spain, italy etc.
3. Habari kwa upande wa watangazaji wanaume mmajitahidi, wanaume wamechangamka wanapotangaza habari. Wanawake wengi wamezubaa maana unakuta mtangazaji mwanaume anajaribu kumu-engage mtangazaji mwanamke kwenye mazungumzo ya kuchangamsha habari ila unakuta mwitikio ni mbovu. Wamezubaa wengi.
3. Kingine nafikiri kinawaangusha ila hamna namna ya kukizuia ni KUAJIRI vyeti badala ya vipaji. Ni bahati mbaya ila hamna namna. Kuna vijana wana vipaji na ubunifu wa hali ya juu ktk mambo ya journalism ila vyeti ndio 'taizo'.
4. Watengenezaji wenu wa documentaries za hapa kwetu wawe na ubunifu. Documentaries zimezubaa ma kupooza.

Kwa hiyo, Anzeni na muonekano wa tv yenu. Kweli Rangi imepooza sana. Hamna ule uHD.

Nawapa pongezi pia kwa kuwa na nia ya kutaka kubadilika na kuomba mawazo ya watu. Kwa ujumla, mjikite ktk quality amd contents ya vipindi na muonekano wenu.
Mnajitahidi.
 
Siipendi TBC na naikwepa kuiangalia, baasdi ya vipindi vyake vinakera.
 
Mliwahi ona BBC au CNN, RT, DW wanaonesha vituko kama :
Tatu MZUKA /BIKO mda wa habari (serious news hour)
Chereko Chereko
Kualika makada wa Chama tu kama akina MKINGA bila kubalance na Pro opposition
Kutoonesha proceedings muhimu kwa Taifa kama BUNGE huku mda huo huo mnaonesha maigizo ya gawiwo au ufunguzi wa kitawi cha Chama /Benki

PIA
Sisi tunataka Live match hata mara moja moja kwa Timu ya Taifa kama uzalendo kwa raia wenu.
Picha zenu zina JIVU.
Badilikeni.
 
Ili kuunga mkono juhudi za TCRA, niliamua kuiblock hii channel kama walivyoblock local channels nyingine.

Hii imeongeza ufanisi wangu katika kuwakwepesha wanangu kujifunza ujinga. Wenye akili zao hawawezi kupoteza muda kuangalia ujinga.
 
Safi sana. Bonge la ushauri. Kwa kweli watangazaji wao wa kike wamezubaa na vipindi ni vya kizee plus muonekano wa vipindi vyao ni mbaya.
 
Hizo ni international versions za hizo tv. Bbc wana bbc kadhaa nafikiri ipo inayoonyeshaga lotteries za kule kwao. Kuna mdau kawashauri wawe na tbc1, 2, 3 kwa audience tofauti.
 
HatuweZ kuwalaumu tBC,
Hapa tuwe wavumilivu hadi mhula wa huyu jamaa uishe.
 
Maoni yangu ni haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…