Kumbe TBC sio watu.
Walirusha picha chafu na mbaya kwa watanzania, asira za Chedema zilipanda juu kwa kasi ya ajabu.
Hii ilikuwa uzinduzi wa kampeni za urais Mh. Tundu Lisu Aug 28, 2020.
Maswali ya msingi.
2015 watu walijaa sana katika mikutano ya Chadema je. Walikuja wenyewe au waliwaleta kwa kuwabeba.
Kama walikuja wenyewe kwanini jana kule Zakhemu Mbagala watu hawakuja kama 2015 kwa Lisu? kwanini?
Kama waliwanunua kwanini jana hawakufanya hivyo kama kawaida yao? Maana uzinduzi wa kampeni wa Lisu ulikuwa kama wa diwani pale Mbagala.
Hii ni aibu katika medani za kisiasa kwani kuporomoka hivi inaonyesha kuwa hawana haja ya kuharibu pesa zao kwa kutafuta urais labda wajikite kutetea majimbo ya ubunge na kurudisha madiwani wao. Wataalam wa picha wanasema walikuwa watu 880 kadirio la juu.
Hii ilikuwa uzinduzi wa kampeni Oct, 2015 pale Jangwani.
Chadema ilizindua kampeni na mamilioni ya watu.
Huyu alikuwa kibwetele wa maisha yao hawakujua 2015
Kulikua hakuna sehemu ya kukanyaga vipi kwa Lisu, Watanzania kumbe nao siyo watu hata huruma tu mtu anatembea na risasi mwilini hawataki.
Hii ni jangwani 2015, kila mtu alijua CCM inaondoka, sasa hii ya Zakhiem mi sichangii.
Hii ni leo 29 Aug, 2020 kule Dodoma katika viwanja vya Jamuhuri
Mamilion ya watu wamemiminika. Na hilo likichwa unaloliona hapo ndiyo ambalo baadae wazungu watakuja kulichukua kama walivyo chukuwa fuvu la Mtemi Mkwawa wa Iringa kwenda kulipima kama hiyo miakili ilikaaje kaaje. Huyo ni noma jamani nadhani ni bora kumwacha apite ndiyo mje njifaye mnadindisha, maana ukisogeza ugoko yeye anasukuma jiwe.