Michuano ya kombe la dunia itarushwa live kupitia chanell ya taifa kwa kushirikiana na TV1...
Nani kafurahishwa na hili[emoji41] [emoji41]
TBC1 itaonesha bure michuano ya kandanda ya Kombe la Dunia. Michuano hiyo itakayofanyika nchini Rusia itafanyika kwa muda wa mwezi mzima kuanzia tarehe 14 mwezi Juni mpaka tarehe 14 Julai 2018. Serikali kupitia luninga yake ya TBC1 kwa kushirikiana na luninga ya TV1 itaonesha matangazo hayo na kuwa serikali ya kwanza kusini mwa jangwa la Sahara kurusha bure matangazo ya michezo hiyo inayopendwa mno na zaidi ya watu bilioni nne duniani.
Hayo yamejulikana leo hii wakati wa uzinduzi rasmi wa matangazo hayo ambapo mgeni rasmi alikuwa msanii Ali Kiba. Pia katika hafla hiyo alikuwepo waziri michezo Daktari Harrison Mwakembe na mkurugenzi mkuu wa TBC Daktari Ayoub Rioba na wakurungezi wa TVI.
Kwa kweli serikali hii itakuwa inaendelea kutimiza lengo lake la kuwatumikia watanzania walio wanyonge.
Hongera Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari John Magufuli.