TBS: Kuanzia 01 Machi 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi, utafanyikia hapa nchini

Kama ni mzoefu wa kuagiza magari, pamoja na gharama nyingine lakini pia kunakuwa na gharama ya ukaguzi, kwa Japan inakuwa around dola 100 mpk 300 kutegemea na gari. Na ilikuwa usipokuwa na cheti cha inspection unapigwa faini hapa bongo. Naona TRA wanazitaka hizo dola badala ya kuwaachia wajapan nk.

Lkn pia wale wajapan ili wafanye biashara walikuwa wana customize vyeti vya ukaguzi vyote vinakuwa qualified hata kama gari halistahili kwa matumizi ya binadamu na mazingira.
 
Mi sioni cha ajabu hapa.
Kwa kuwa, hata sasa hivi ukiagiza gari kutoka Japan, lazima likaguliwe, na utalipia gharama ya kukaguliwa na kampuni ambayo imepata kibali kutoka Tanzania. Tena unalipa kwa $ kati $100 hadi $300 kama mdau alivyosema hapo juu.

Kilichobadilika ni kuwa badala ya kulipia na kukaguliwa Japan, sasa utalipia na kukaguliwa hapa.

Mi naona ni jambo nzuri. Kwanini tuiingizie hela ya ukaguzi Japan badala ya hiyo hela ibaki Tanzania?

Kwanini uangaike ku badilisha hela ya TSh kwenda $ kwa ajili ya kulipia ukaguzi Japan ambapo $ ni gharama badala ya kulipia kwa TSh?
 

Wanatanua wigo wa kukusanya kodi.
 
Sema itasababisha msongamano mkubwa na hivyo kuchelewesha clearance ya magari
 
Mpumbavu
 
Shida sio ukaguzi maana hata kabla magari yalikuwa yanakaguliwa kabla ya kuwa shipped. Tatizo litakuwa ukiritimba, lazima kubambikiwa, kulipishwa X2 na kucheleweshewa huduma vitakuwa vipaumbele vyao.

Tutaona!
 
Nachokiona hapa ni urasimu kuongezeka pamoja na ucheleweshwaji wa magari na wizi wa vifaa kama yatakaguliwa uchochoroni.

Gharama nayo ni heri iwekwe public watu wajiandae mapema.

Nimeona kuna wakala wao ana-charge $295 kwa ajili ya pre-ship inspection huko Japan, hope nao hawatakuwa mbali na hapo.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…