Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,926
- 95,626
Panga Pangua, Anzisha, Bomoa...., kila siku ni kubadilisha badilisha
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Panga Pangua, Anzisha, Bomoa...., kila siku ni kubadilisha badilisha
Mara paap TBS wanapeleka magari kukaguliwa temesa ambao hata kukagua landrover 109 hawaweziUKAGUZI WA MAGARI YANAYOTOKA NJE KUFANYIKA NCHINI CHINI YA TBS KUANZIA MARCH 01,2021 HIVYO VYETI VYA UKAGUZI KUTOKA NJE YA NCHI KUANZIA MARCH 01,2021 HAVITATAMBULIKA NCHINI. View attachment 1681995
Safi sana
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linawataarifu waagizaji na wauzaji wa magari kutoka nje ya nchi kuwa kuanzia tarehe 01 mwezi Machi, 2021, utaratibu wa kukagua magarikutoka nje ya nchi utafanyika baada ya kuwasili hapa nchini (Destination Inspection).Hivyo,magari yote yatakayosafirishwa kuanzia tarehe tajwa hapo juu yatakaguliwa katika bandari yaDar-es-Salaam.
Kwa sasa TBS inakagua magari kutoka nje ya nchi kupitia mawakala watatu(3) kutoka Japan na mmoja(1) kutoka Dubai ambao mikataba yao itakoma hivi karibuni.
Hivyo vyeti vya ukaguzi vitakavyotolewa na mawakala tajwa kwa magari yatakayosafirishwa kuanzia tarehe 01 mwezi Machi, 2021 havitatambulika na TBS.
Aidha,magari yatakayopimwa bandarini na kutokidhi matakwa ya kiwango yatahitaji kufanyiwa matengenezo nje ya bandari na kisha kuletwa na kupimwa tena kwenye yadi ya UDA mkabala na Bandari ya Dar es salaam.
Shirika litaendelea kuhakikisha kuwa magari yote yaliyotumika nakuingizwa nchini yanakidhi matakwa ya kiwango cha magari yaliyotumika.
Kwa taarifa zaidi kuhusu utaratibu huu mpyausisite kuwasiliana na:-
Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania (TBS),
SLP 9524,
Dar es Salaam.
View attachment 1682017
hiyo hela ya inspection kwa Tanzania tulikuwa tunaipoteza bure, kwa sababu inspection unalipia inafanyika nje kuna ubaya gani ikifanyika ndani?Wanakagua nini kwa kuanzia?
Mengi yameshakuwa nje ya specs tayari ndo maana yanauzwa kwetu maskini.
Au wanapanua goli ili kupiga pesa.
Sema itasababisha msongamano mkubwa na hivyo kuchelewesha clearance ya magariMi sioni cha ajabu hapa.
Kwa kuwa, hata sasa hivi ukiagiza gari kutoka Japan, lazima likaguliwe, na utalipia gharama ya kukaguliwa na kampuni ambayo imepata kibali kutoka Tanzania. Tena unalipa kwa $ kati $100 hadi $300 kama mdau alivyosema hapo juu.
Kilichobadilika ni kuwa badala ya kulipia na kukaguliwa Japan, sasa utalipia na kukaguliwa hapa.
Mi naona ni jambo nzuri. Kwanini tuiingizie hela ya ukaguzi Japan badala ya hiyo hela ibaki Tanzania?
Kwanini uangaike ku badilisha hela ya TSh kwenda $ kwa ajili ya kulipia ukaguzi Japan ambapo $ ni gharama badala ya kulipia kwa TSh?
Sijajua nini faida ya hili jambo...
MpumbavuMi sioni cha ajabu hapa.
Kwa kuwa, hata sasa hivi ukiagiza gari kutoka Japan, lazima likaguliwe, na utalipia gharama ya kukaguliwa na kampuni ambayo imepata kibali kutoka Tanzania. Tena unalipa kwa $ kati $100 hadi $300 kama mdau alivyosema hapo juu.
Kilichobadilika ni kuwa badala ya kulipia na kukaguliwa Japan, sasa utalipia na kukaguliwa hapa.
Mi naona ni jambo nzuri. Kwanini tuiingizie hela ya ukaguzi Japan badala ya hiyo hela ibaki Tanzania?
Kwanini uangaike ku badilisha hela ya TSh kwenda $ kwa ajili ya kulipia ukaguzi Japan ambapo $ ni gharama badala ya kulipia kwa TSh?
Mkuu kwani ukiagiza Japan kwa sasa costs za inspection nani analipia?Inspection charge itakuwa juu ya nani?
Huu sasa ni uhuni
Hapa naona vitu vifuatavyo;
1. Hata kama gari itakuja nzima, utaambiwa ni mbovu. Linatakiwa likatengenezwe. Kuna vifaa vitachomolewa halafu utavikuta kwenye garage zao uuziwe mara ya pili.
2. Watalazimisha wapeleke garage zao. Bei zitakuja za ajabu. Usishangae ukaambiwa ulipe 500K kwa kitu ambacho ungetengeneza kwa 200K.
Anaelewa hata hiyo maana ya inspection fee?Mkuu kwani ukiagiza Japan kwa sasa costs za inspection nani analipia?