PureView zeiss
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 10,786
- 35,916
Kama siti zimeliwa na panya wa huko Japan!Wanakagua nini kwa kuanzia?
Mengi yameshakuwa nje ya specs tayari ndo maana yanauzwa kwetu maskini.
Au wanapanua goli ili kupiga pesa.
Tatizo ni uaminifu wa mtanzania huyo atakayekagua hiyo gari.Nakwambia kuna watu watafungua maduka ya spea.Mi sioni cha ajabu hapa.
Kwa kuwa, hata sasa hivi ukiagiza gari kutoka Japan, lazima likaguliwe, na utalipia gharama ya kukaguliwa na kampuni ambayo imepata kibali kutoka Tanzania. Tena unalipa kwa $ kati $100 hadi $300 kama mdau alivyosema hapo juu.
Kilichobadilika ni kuwa badala ya kulipia na kukaguliwa Japan, sasa utalipia na kukaguliwa hapa.
Mi naona ni jambo nzuri. Kwanini tuiingizie hela ya ukaguzi Japan badala ya hiyo hela ibaki Tanzania?
Kwanini uangaike ku badilisha hela ya TSh kwenda $ kwa ajili ya kulipia ukaguzi Japan ambapo $ ni gharama badala ya kulipia kwa TSh?
Mitano tena itapendeza!!Uchumi wa kati ndugu zangu
😀Mpumbavu
Je hii itaongeza maumvu kwa walala hoi au kupunguza?Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linawataarifu waagizaji na wauzaji wa magari kutoka nje ya nchi kuwa kuanzia tarehe 01 mwezi Machi, 2021, utaratibu wa kukagua magarikutoka nje ya nchi utafanyika baada ya kuwasili hapa nchini (Destination Inspection). Hivyo,magari yote yatakayosafirishwa kuanzia tarehe tajwa hapo juu yatakaguliwa katika bandari yaDar-es-Salaam.
Kwa sasa TBS inakagua magari kutoka nje ya nchi kupitia mawakala watatu(3) kutoka Japan na mmoja(1) kutoka Dubai ambao mikataba yao itakoma hivi karibuni.
Hivyo vyeti vya ukaguzi vitakavyotolewa na mawakala tajwa kwa magari yatakayosafirishwa kuanzia tarehe 01 mwezi Machi, 2021 havitatambulika na TBS.
Aidha,magari yatakayopimwa bandarini na kutokidhi matakwa ya kiwango yatahitaji kufanyiwa matengenezo nje ya bandari na kisha kuletwa na kupimwa tena kwenye yadi ya UDA mkabala na Bandari ya Dar es salaam.
Shirika litaendelea kuhakikisha kuwa magari yote yaliyotumika nakuingizwa nchini yanakidhi matakwa ya kiwango cha magari yaliyotumika.
Kwa taarifa zaidi kuhusu utaratibu huu mpyausisite kuwasiliana na:-
Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania (TBS),
SLP 9524,
Dar es Salaam.
View attachment 1682017
Hapo sasa ni kuomba dua gari uliloagiza liwe vizuri,maana likija na taili kipara kazi unayoHapa navyoona itakuwa inspection fee ziko mbili ya japan na ya hapa kwetu na sion haja ya kuja kukagua tena wakati aa Japana wanakagua na kama linashida hiwa wanaonyesha kwenye karatasi yao labda kama wangekuwa na akili wangekuwa wanacollect zile karatas za inspection then wanaingiza kwenye database yao na mtu unapokabidhiwa gari yako unatakiwa ulishughulikie ile shida ya gari baada ya mwezi so utapikamatwa baada ya hapo unapigwa fine lakin kutokana na kutaka mapato zaid kuliko huduma wameona ndio njia sahihi
Huyo walipiga 15% penalty, ila nae huyo ana matatizo sana maana ingekua gari ta Singapore inajulikana kua zinakaguliwa hapa hapa TanzaniaNina mwanangu aliagiza gari hakukagua huko JP. Hatari na nusu.
Gari ikafika wakaenda kukagua NIT gharama knm. Hafu ukirudishwa ni gharama zako kutengeneza. Unaweza kuta ukatumia Million kimasihara hivi hivi.