TBS: Kuanzia 01 Machi 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi, utafanyikia hapa nchini

TBS: Kuanzia 01 Machi 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi, utafanyikia hapa nchini

Itakuaje Kwa IT ?
HAPA kuna harufu ya upigaji pesa kwasabb ili gari ipitishwe kama imekidhi vigezo itahitajika pesa ya kupoza ili mambo yasiwe mengi...
na itakavyozidi kukaa yard kuna charge ya storage yaani ni mateso mpaka huyu mshamba anaondoka madarakani
 
Mi sioni cha ajabu hapa.
Kwa kuwa, hata sasa hivi ukiagiza gari kutoka Japan, lazima likaguliwe, na utalipia gharama ya kukaguliwa na kampuni ambayo imepata kibali kutoka Tanzania. Tena unalipa kwa $ kati $100 hadi $300 kama mdau alivyosema hapo juu.

Kilichobadilika ni kuwa badala ya kulipia na kukaguliwa Japan, sasa utalipia na kukaguliwa hapa.

Mi naona ni jambo nzuri. Kwanini tuiingizie hela ya ukaguzi Japan badala ya hiyo hela ibaki Tanzania?

Kwanini uangaike ku badilisha hela ya TSh kwenda $ kwa ajili ya kulipia ukaguzi Japan ambapo $ ni gharama badala ya kulipia kwa TSh?
Tatizo ni uaminifu wa mtanzania huyo atakayekagua hiyo gari.Nakwambia kuna watu watafungua maduka ya spea.
 
Kuongezea wanunuzi magari gharama za huo ukaguzi wakati japan JAAI tayari wanakuwa wameshakagua tu
 
Sheria za kukurupuka hizi halafu mwisho wa siku wanaona madhara yake
Mtu anaamka asubuhi na kuifanya sheria, hii utazikuta Africa tu
Unaota usiku asubuhi unaifanya sheria
 
Haya majanga sasa, vingi wanavyokagua hua wanavipitisha ili hali havina ubora kabisa...

Labda kama nia yao ni kukusanya kodi tu...





Cc: mahondaw
 
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linawataarifu waagizaji na wauzaji wa magari kutoka nje ya nchi kuwa kuanzia tarehe 01 mwezi Machi, 2021, utaratibu wa kukagua magarikutoka nje ya nchi utafanyika baada ya kuwasili hapa nchini (Destination Inspection). Hivyo,magari yote yatakayosafirishwa kuanzia tarehe tajwa hapo juu yatakaguliwa katika bandari yaDar-es-Salaam.

Kwa sasa TBS inakagua magari kutoka nje ya nchi kupitia mawakala watatu(3) kutoka Japan na mmoja(1) kutoka Dubai ambao mikataba yao itakoma hivi karibuni.

Hivyo vyeti vya ukaguzi vitakavyotolewa na mawakala tajwa kwa magari yatakayosafirishwa kuanzia tarehe 01 mwezi Machi, 2021 havitatambulika na TBS.

Aidha,magari yatakayopimwa bandarini na kutokidhi matakwa ya kiwango yatahitaji kufanyiwa matengenezo nje ya bandari na kisha kuletwa na kupimwa tena kwenye yadi ya UDA mkabala na Bandari ya Dar es salaam.

Shirika litaendelea kuhakikisha kuwa magari yote yaliyotumika nakuingizwa nchini yanakidhi matakwa ya kiwango cha magari yaliyotumika.

Kwa taarifa zaidi kuhusu utaratibu huu mpyausisite kuwasiliana na:-

Mkurugenzi Mkuu,

Shirika la Viwango Tanzania (TBS),

SLP 9524,

Dar es Salaam.

View attachment 1682017
Je hii itaongeza maumvu kwa walala hoi au kupunguza?
 
Hapa navyoona itakuwa inspection fee ziko mbili ya japan na ya hapa kwetu na sion haja ya kuja kukagua tena wakati aa Japana wanakagua na kama linashida hiwa wanaonyesha kwenye karatasi yao labda kama wangekuwa na akili wangekuwa wanacollect zile karatas za inspection then wanaingiza kwenye database yao na mtu unapokabidhiwa gari yako unatakiwa ulishughulikie ile shida ya gari baada ya mwezi so utapikamatwa baada ya hapo unapigwa fine lakin kutokana na kutaka mapato zaid kuliko huduma wameona ndio njia sahihi
 
Hapa navyoona itakuwa inspection fee ziko mbili ya japan na ya hapa kwetu na sion haja ya kuja kukagua tena wakati aa Japana wanakagua na kama linashida hiwa wanaonyesha kwenye karatasi yao labda kama wangekuwa na akili wangekuwa wanacollect zile karatas za inspection then wanaingiza kwenye database yao na mtu unapokabidhiwa gari yako unatakiwa ulishughulikie ile shida ya gari baada ya mwezi so utapikamatwa baada ya hapo unapigwa fine lakin kutokana na kutaka mapato zaid kuliko huduma wameona ndio njia sahihi
Hapo sasa ni kuomba dua gari uliloagiza liwe vizuri,maana likija na taili kipara kazi unayo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Nina mwanangu aliagiza gari hakukagua huko JP. Hatari na nusu.

Gari ikafika wakaenda kukagua NIT gharama knm. Hafu ukirudishwa ni gharama zako kutengeneza. Unaweza kuta ukatumia Million kimasihara hivi hivi.
Huyo walipiga 15% penalty, ila nae huyo ana matatizo sana maana ingekua gari ta Singapore inajulikana kua zinakaguliwa hapa hapa Tanzania
 
Back
Top Bottom