TBS: Kuanzia 01 Machi 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi, utafanyikia hapa nchini

Shida sio ukaguzi maana hata kabla magari yalikuwa yanakaguliwa kabla ya kuwa shipped. Tatizo litakuwa ukiritimba, lazima kubambikiwa, kulipishwa X2 na kucheleweshewa huduma vitakuwa vipaumbele vyao.

Tutaona!
... hao TBS wana utaalamu wa kukagua magari ya aina zote yanayotengenezwa duniani? Kwanini wenye utaalamu wa specific magari wasiachiwe kazi hiyo? Nachokiona hapa magari yatazidi kuharibiwa tofauti na hali yaliyokuja nayo.

By the way, sijawahi kukutana na hii scenario; kwa ukaguzi unaofanyika huko Japan, ikitokea gari haija-meet vigezo baada ya ukaguzi kinafuata nini? Mteja anatuma tena hela ya matengenezo au inakuwaje? Maana kwa huu ukaguzi wa shithole, naona kabisa wateja wakilipa gharama kubwa za matengenezo kwa kinachoitwa "gari halijakidhi vigezo" ili tu watu wapige pesa!
 

Wanaume nyie fundi25 🙌🙌🙌

Wakati naolewa bibi yangu kipenzi rip aliniambia umeutaka ukubwa wa kumpenda mtoto wa watu sasa sikiliza....

"kama mwanaume anafanya majukumu yake, Usimpekuepekue na kumtafutia makosa sababu lazima utayapata na hujui ukishayapata utafanya nini
Usishindane na mwanaume hata siku moja maana utachekwa na watu kwa kuwa mama asiye na heshima.
Mwanaume akienda mwache aende wewe baki fanya kazi na utunze familia... huko anakoenda kukimshinda atarudi!
Na akirudi muulize alichovuna huko maana alienda kutafuta na wewe mwonueshe ulichofanya

Mkimaliza hapo mkapime huo ugonjwa wenu wa kisasa maana hicho tuu ndio kitu hatari kwa hiki Kizazi chenu"

Haya maneno ni magumu sana kuyatekeleza na magumu zaidi kuyapuuza😥😥😥
 
Ndo wamesema hivyo au umewaza tu?
 
Serikali ijenge viwanda na sio kulazimisha ajira za kulazimisha.

Hapa wadau wanakwepa ukiritimba wa serikali.

Serikali haijawahi kuanzisha kitu na kukifanya kwa usahihi.
 
Ukalete magari ambayo yatawafanya washindwe hata kufanya inspection, watafanyaje hapo?
 
Sawa
 
Binafsi niliagiza gari ..halikupita kwenye inspection ..nikaachana nalonnikatafuta lingine likapita ..na wakanktumia
.

Sasa kwa huu ukaguzi wa tbs wa hapa ndani itakuwa ni majanga tuu
.
.maana nakumbukai Ile canter ilikuwa inasumbua kwenye Gea. ...simpati picha Kama ndo ingeingia hapa alafu tbs ndo wakague.....gearbox ya canter bei yake inajulikana
 
hili swali hata mimi nimejiuliza.
 
Kwa uelewa wangu ni kwamba magari hayatakuwa yanafanyiwa inspection point of origin bali Destination. Maana kwenye waraka wanasema mikataba na wale wanaofanya inspection Japan na Dubai itafikia ukomo.
 
[emoji106] Wazo zuri sana Mkuu! Kwa ulimwengu huu wa kidigitali TBS wangejadiliana na taasisi husika kwa mfano JAAI ili wawe kwenye mtandao mmoja ambapo kila gari linalokaguliwa kabla ya kuingia nchini, taarifa zake zinaonekana TBS.
Pili kwenye biashara za kimataifa kunahusisha wadau mbalimbali hivyo huwezi kupata " maximum profit". TBS wangeridhika na kile wanachopata au wakae na wadau husika kama wanaona kuna haja ya kufanya hivyo.
 
Mi naona ni jambo nzuri. Kwanini tuiingizie hela ya ukaguzi Japan badala ya hiyo hela ibaki Tanzania?
Ishu kwangu ni uwezo wao wa kufanya hiyo inspection, maana kuna shehena huwa zinalalamikiwa sana kuchelewa kukaguliwa na haohao TBS.
Kwa japani sina shida nao; kuna kipindi nilikuwa nacheki gari, baada ya makubaliano kila kitu, yule seller akasema hataweza kuipeleka Test, kama nataka kununua ninunue tu; hapo nikajua kabisa kwamba JP wakao makini.
 
hiyo hela ya inspection kwa Tanzania tulikuwa tunaipoteza bure, kwa sababu inspection unalipia inafanyika nje kuna ubaya gani ikifanyika ndani?
Hakuna ubaya hata kidogo na hasa kama unajua urasimu wa TBS, wengi watayaacha magari yao pale
 
Mkuu shangaa na wewe, kuna vitu vingine watu wanavipinga mpaka unajiuliza hivi wanafikiria sawa sawa kweli kweli? Watu wanaona ni vyema kuwalipa wajapan kuliko kurudisha huu utaratibu tupate hicho tunachowapa wajapan..
 
Itakuwa vizuri TBS wakasema ni vitu gani watakuwa wana check. Hii itasaidia ingawa itakuwa ni extra cost kuli check huko huko Japan kwa kutumia vigezo vya TBS. Kwa mfano wana check tyres na condition ya tyres ni poor , utaingia cost extra kununua tyres Mpya hapa Tanzania tena kwenye outlet designated na TBS.
 
Hii serikali imekuwa ikiingilia private sector ili kupata hela za kuendeshea nchi.
ZIMBABWE ILEEEE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…