TBS: Kuanzia 01 Machi 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi, utafanyikia hapa nchini

TBS: Kuanzia 01 Machi 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi, utafanyikia hapa nchini

Shida sio ukaguzi maana hata kabla magari yalikuwa yanakaguliwa kabla ya kuwa shipped. Tatizo litakuwa ukiritimba, lazima kubambikiwa, kulipishwa X2 na kucheleweshewa huduma vitakuwa vipaumbele vyao.

Tutaona!
... hao TBS wana utaalamu wa kukagua magari ya aina zote yanayotengenezwa duniani? Kwanini wenye utaalamu wa specific magari wasiachiwe kazi hiyo? Nachokiona hapa magari yatazidi kuharibiwa tofauti na hali yaliyokuja nayo.

By the way, sijawahi kukutana na hii scenario; kwa ukaguzi unaofanyika huko Japan, ikitokea gari haija-meet vigezo baada ya ukaguzi kinafuata nini? Mteja anatuma tena hela ya matengenezo au inakuwaje? Maana kwa huu ukaguzi wa shithole, naona kabisa wateja wakilipa gharama kubwa za matengenezo kwa kinachoitwa "gari halijakidhi vigezo" ili tu watu wapige pesa!
 
Tunapiga adi magoti shetani m'baya sana moyoni unasema tatizo linakaribia kwisha! Unapiga maneno mazuri shetani anapita maisha yana songa! Ukitoka una nyanyua simu una mpigia jamaa yako unamwambia home kimenuka wife kapandisha mzuka una mpa story anakuambia aahhhh iyo mbona kawaida sana iyo mpango wa kando me mbona ndogo sana me nime mtongoza Mama mkwe na tuka kemea shetani ya kwisha 😂

Wanaume nyie fundi25 🙌🙌🙌

Wakati naolewa bibi yangu kipenzi rip aliniambia umeutaka ukubwa wa kumpenda mtoto wa watu sasa sikiliza....

"kama mwanaume anafanya majukumu yake, Usimpekuepekue na kumtafutia makosa sababu lazima utayapata na hujui ukishayapata utafanya nini
Usishindane na mwanaume hata siku moja maana utachekwa na watu kwa kuwa mama asiye na heshima.
Mwanaume akienda mwache aende wewe baki fanya kazi na utunze familia... huko anakoenda kukimshinda atarudi!
Na akirudi muulize alichovuna huko maana alienda kutafuta na wewe mwonueshe ulichofanya

Mkimaliza hapo mkapime huo ugonjwa wenu wa kisasa maana hicho tuu ndio kitu hatari kwa hiki Kizazi chenu"

Haya maneno ni magumu sana kuyatekeleza na magumu zaidi kuyapuuza😥😥😥
 
Hamna msongamano wa clearance wala nini, ipo hivi unaclear na kulipa kodi zote za serikali, inabaki registration tuu, hapo kama gari ni bovu unakabidhiwa bila usajili ukalitengeneze vitu walivyoainisha, unapewa na muda wa kama mwezi mmoja hivi ukikamilisha matengenezo unapewa vibali vyako
Ndo wamesema hivyo au umewaza tu?
 
Hela nyingin sana zinapotea, pamoja na ajira...kumbuka watakaofanya inspection huku Tanzania ni hawa vijana ambao tunalia kila siku hawana ajira, na watakaofanya ufundi wa kurekebisha magari mabovu ni watanzania na hela inabaki tanzania

Sidhani kama umefikiri vizuri kabla ya kuandika comment ya ki wack namna hii...no brainer
Serikali ijenge viwanda na sio kulazimisha ajira za kulazimisha.

Hapa wadau wanakwepa ukiritimba wa serikali.

Serikali haijawahi kuanzisha kitu na kukifanya kwa usahihi.
 
Wanaweza kuambia iyo gari ina tatizo
Ukaikubali au ukaikataa ikabadilishwa au ika fanyiwa marekebisho ila sio mara zote!
Gari nyingi hazinaga matatizo! Sasa bahati mbaya gari ikifika hapa kuna matatizo mengi yatakuwa changamoto haswa kwa magari ya kisasa kidogo maana spear nyingine itabidi waagize sensor!
Kuajiri huko wataalam wa ajuzi wa ukaguzi ni wengi na vifaa ni vingi na bei nafuu kuliko huku! Kazi ya ukaguzi inahitaji Dr.mjuzi aliye bobea akisikia tu sauti ya engine bila ku kusogelea anajua tiari shidaha ni nini mara nyingi bila kutumia vipimo ndio sifa kubwa ya ufundi vinginevyo uta tafuta tatizo siku 20 au masaa mengi!
Aina za magari huku kwetu zina badilika kila siku zinaonekana aina mpya hko Ulaya zinajulikana mda na utatuzi wa changamoto zake! Tujiandae kuumia kidogo! Kwanza kitu cha kwanza TBS wata fungua duka la matairi magari yote watataka yabadilishwe tairi...
Ukalete magari ambayo yatawafanya washindwe hata kufanya inspection, watafanyaje hapo?
 
Hamna msongamano wa clearance wala nini, ipo hivi unaclear na kulipa kodi zote za serikali, inabaki registration tuu, hapo kama gari ni bovu unakabidhiwa bila usajili ukalitengeneze vitu walivyoainisha, unapewa na muda wa kama mwezi mmoja hivi ukikamilisha matengenezo unapewa vibali vyako
Sawa
 
Binafsi niliagiza gari ..halikupita kwenye inspection ..nikaachana nalonnikatafuta lingine likapita ..na wakanktumia
.

Sasa kwa huu ukaguzi wa tbs wa hapa ndani itakuwa ni majanga tuu
.
.maana nakumbukai Ile canter ilikuwa inasumbua kwenye Gea. ...simpati picha Kama ndo ingeingia hapa alafu tbs ndo wakague.....gearbox ya canter bei yake inajulikana
 
Itakuaje Kwa IT ?
HAPA kuna harufu ya upigaji pesa kwasabb ili gari ipitishwe kama imekidhi vigezo itahitajika pesa ya kupoza ili mambo yasiwe mengi...
na itakavyozidi kukaa yard kuna charge ya storage yaani ni mateso mpaka huyu mshamba anaondoka madarakani
hili swali hata mimi nimejiuliza.
 
Hapa navyoona itakuwa inspection fee ziko mbili ya japan na ya hapa kwetu na sion haja ya kuja kukagua tena wakati aa Japana wanakagua na kama linashida hiwa wanaonyesha kwenye karatasi yao labda kama wangekuwa na akili wangekuwa wanacollect zile karatas za inspection then wanaingiza kwenye database yao na mtu unapokabidhiwa gari yako unatakiwa ulishughulikie ile shida ya gari baada ya mwezi so utapikamatwa baada ya hapo unapigwa fine lakin kutokana na kutaka mapato zaid kuliko huduma wameona ndio njia sahihi
Kwa uelewa wangu ni kwamba magari hayatakuwa yanafanyiwa inspection point of origin bali Destination. Maana kwenye waraka wanasema mikataba na wale wanaofanya inspection Japan na Dubai itafikia ukomo.
 
Hapa navyoona itakuwa inspection fee ziko mbili ya japan na ya hapa kwetu na sion haja ya kuja kukagua tena wakati aa Japana wanakagua na kama linashida hiwa wanaonyesha kwenye karatasi yao labda kama wangekuwa na akili wangekuwa wanacollect zile karatas za inspection then wanaingiza kwenye database yao na mtu unapokabidhiwa gari yako unatakiwa ulishughulikie ile shida ya gari baada ya mwezi so utapikamatwa baada ya hapo unapigwa fine lakin kutokana na kutaka mapato zaid kuliko huduma wameona ndio njia sahihi
[emoji106] Wazo zuri sana Mkuu! Kwa ulimwengu huu wa kidigitali TBS wangejadiliana na taasisi husika kwa mfano JAAI ili wawe kwenye mtandao mmoja ambapo kila gari linalokaguliwa kabla ya kuingia nchini, taarifa zake zinaonekana TBS.
Pili kwenye biashara za kimataifa kunahusisha wadau mbalimbali hivyo huwezi kupata " maximum profit". TBS wangeridhika na kile wanachopata au wakae na wadau husika kama wanaona kuna haja ya kufanya hivyo.
 
Mi naona ni jambo nzuri. Kwanini tuiingizie hela ya ukaguzi Japan badala ya hiyo hela ibaki Tanzania?
Ishu kwangu ni uwezo wao wa kufanya hiyo inspection, maana kuna shehena huwa zinalalamikiwa sana kuchelewa kukaguliwa na haohao TBS.
Kwa japani sina shida nao; kuna kipindi nilikuwa nacheki gari, baada ya makubaliano kila kitu, yule seller akasema hataweza kuipeleka Test, kama nataka kununua ninunue tu; hapo nikajua kabisa kwamba JP wakao makini.
 
hiyo hela ya inspection kwa Tanzania tulikuwa tunaipoteza bure, kwa sababu inspection unalipia inafanyika nje kuna ubaya gani ikifanyika ndani?
Hakuna ubaya hata kidogo na hasa kama unajua urasimu wa TBS, wengi watayaacha magari yao pale
 
Mi sioni cha ajabu hapa.
Kwa kuwa, hata sasa hivi ukiagiza gari kutoka Japan, lazima likaguliwe, na utalipia gharama ya kukaguliwa na kampuni ambayo imepata kibali kutoka Tanzania. Tena unalipa kwa $ kati $100 hadi $300 kama mdau alivyosema hapo juu.

Kilichobadilika ni kuwa badala ya kulipia na kukaguliwa Japan, sasa utalipia na kukaguliwa hapa.

Mi naona ni jambo nzuri. Kwanini tuiingizie hela ya ukaguzi Japan badala ya hiyo hela ibaki Tanzania?

Kwanini uangaike ku badilisha hela ya TSh kwenda $ kwa ajili ya kulipia ukaguzi Japan ambapo $ ni gharama badala ya kulipia kwa TSh?
Mkuu shangaa na wewe, kuna vitu vingine watu wanavipinga mpaka unajiuliza hivi wanafikiria sawa sawa kweli kweli? Watu wanaona ni vyema kuwalipa wajapan kuliko kurudisha huu utaratibu tupate hicho tunachowapa wajapan..
 
Itakuwa vizuri TBS wakasema ni vitu gani watakuwa wana check. Hii itasaidia ingawa itakuwa ni extra cost kuli check huko huko Japan kwa kutumia vigezo vya TBS. Kwa mfano wana check tyres na condition ya tyres ni poor , utaingia cost extra kununua tyres Mpya hapa Tanzania tena kwenye outlet designated na TBS.
 
Hii serikali imekuwa ikiingilia private sector ili kupata hela za kuendeshea nchi.
ZIMBABWE ILEEEE
 
Back
Top Bottom