TBS: Kuanzia 01 Machi 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi, utafanyikia hapa nchini

TBS: Kuanzia 01 Machi 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi, utafanyikia hapa nchini

Shida sio ukaguzi maana hata kabla magari yalikuwa yanakaguliwa kabla ya kuwa shipped. Tatizo litakuwa ukiritimba, lazima kubambikiwa, kulipishwa X2 na kucheleweshewa huduma vitakuwa vipaumbele vyao.

Tutaona!
Watafanya na uharibifu pia na wizi pengine
 
Mi sioni cha ajabu hapa.
Kwa kuwa, hata sasa hivi ukiagiza gari kutoka Japan, lazima likaguliwe, na utalipia gharama ya kukaguliwa na kampuni ambayo imepata kibali kutoka Tanzania. Tena unalipa kwa $ kati $100 hadi $300 kama mdau alivyosema hapo juu.

Kilichobadilika ni kuwa badala ya kulipia na kukaguliwa Japan, sasa utalipia na kukaguliwa hapa.

Mi naona ni jambo nzuri. Kwanini tuiingizie hela ya ukaguzi Japan badala ya hiyo hela ibaki Tanzania?

Kwanini uangaike ku badilisha hela ya TSh kwenda $ kwa ajili ya kulipia ukaguzi Japan ambapo $ ni gharama badala ya kulipia kwa TSh?
Ni hapo tutakapojikuta tunalipa mara 3 ya gharama za Jp!
 
Mapato ndio hasa yanalengwa hapo, hao mawakala walikuwa wanakula pesa za bure tu, sasa pesa zote zinaenda serikalini
 
Mi sioni cha ajabu hapa.
Kwa kuwa, hata sasa hivi ukiagiza gari kutoka Japan, lazima likaguliwe, na utalipia gharama ya kukaguliwa na kampuni ambayo imepata kibali kutoka Tanzania. Tena unalipa kwa $ kati $100 hadi $300 kama mdau alivyosema hapo juu.

Kilichobadilika ni kuwa badala ya kulipia na kukaguliwa Japan, sasa utalipia na kukaguliwa hapa.

Mi naona ni jambo nzuri. Kwanini tuiingizie hela ya ukaguzi Japan badala ya hiyo hela ibaki Tanzania?

Kwanini uangaike ku badilisha hela ya TSh kwenda $ kwa ajili ya kulipia ukaguzi Japan ambapo $ ni gharama badala ya kulipia kwa TSh?
Good point!!
 
Mimi nitabaki wa uber tuu na miguu yangu. Mkinikuta msininyime lift☺☺
Madereva wa TBS sio?  kwenye chakula wamoo, kwenye madawa wamoo, kwenye vifungashio wamoo, kwenye maji wamoo, kwenye chemical wamoo, kwenye magari wamoo, hawa sio watu ni mashetani pengine🙆
 
Nina mwanangu aliagiza gari hakukagua huko JP. Hatari na nusu.

Gari ikafika wakaenda kukagua NIT gharama knm. Hafu ukirudishwa ni gharama zako kutengeneza. Unaweza kuta ukatumia Million kimasihara hivi hivi.
Hiyo gari itakua imetoka Singapore,Kwa Japan ilikua huhitaji ukaguzi
 
Sema bongo tunaiga tuu gari insyotakiwa kukaguliwa ni ile iliyopata ajali ili irudi bara barani Kama imekidhi viwango kwa kuangalia mikanda ipo sawa cheses haijapinda na vitu vingine ila kwa gari ambayo haijapata ajali inaangaliwa ni ya mwaka gani gari inawaka unapewa certificate ili ukapate kibali cha kulipia TRA ila hapo Bongo hao TBS ni TRA iliyo na maandishi ya TBS...
 
Naumia sana kuona password zikiongezwa kwenye magari wakati hayo magari yaliyopo yameingia kwa gharama kubwa sana na bado wanataka kuongeza gharama zisizostahili tena badala ya kupunguza vipengele vya kufanya Kodi inakua kubwa kwenye magari ninyi ndio kila kukicha mnaongeza magari mazuri yatabaki kuwa Transit tuu kwenda Congo DRC na Zambia sisi tukiabaki kujadili matatizo ya passo kila kukicha...
 
Madereva wa TBS sio?  kwenye chakula wamoo, kwenye madawa wamoo, kwenye vifungashio wamoo, kwenye maji wamoo, kwenye chemical wamoo, kwenye magari wamoo, hawa sio watu ni mashetani pengine🙆
😥😥😥😥😥😥
 
Back
Top Bottom