TBS na TFDA okoeni maisha yetu kwa kupima ubora wa unga wa mahindi na muhogo unaosagwa mitaani

TBS na TFDA okoeni maisha yetu kwa kupima ubora wa unga wa mahindi na muhogo unaosagwa mitaani

Wasisahau na hawa Wauza unga lishe. Sasa hivi unga unamchanganyiko hadi midizi ya Kitarasa, kweme, Beet root, Karoti, nyanya, rozella, mlonge etc. Tbs, tfda Njooni twafa huku
Bahati mbaya TBS sisi wanatuona minyangarakasha, wao hufanyia kazi neno likitoka kwa viongozi wa CCM ila kwa hili wanasahau kuwa walaji ni watanzania wote.
 
Wasisahau na hawa Wauza unga lishe. Sasa hivi unga unamchanganyiko hadi midizi ya Kitarasa, kweme, Beet root, Karoti, nyanya, rozella, mlonge etc. Tbs, tfda Njooni twafa huku

Halafu Unapigwa Bla Bla Bla Zinaongeza Nguvu Za Kiume

Oops Chap Unapigwa Haraka

Unakuta umepiga mahindi dawa ili uhifadhi kwa matumizi ya baadaye, mara anakuja mteja na bei nzuri unamuuzia anasafirisha kwenda mjini.

Yakifika huko yanasagwa dona hata bila kusafishwa mwishowe mnakula sumu mbichi kabisa ambayo hata wadudu wasingeigusa.

Tunaishi kwa neema ya Mungu tu ila tunakula sumu kabisa.
Mifuko ya tabaka tatu ni aghali, lakini ndio njia salama ya kuhifadhia nafaka. Lakini ukiweka na gharama ya madawa, kuchanganya na ukweli kuwa dawa hudumu kwa miezi 6, uaghali wa tabaka tatu haupo.
 
Mkuu kwa uelewa wangu TBS pamoja na taasisi ya chakula na lishe (TFNC) kwa kushirikiana na taasisi binafsi pamoja na za serekali (Tamisemi, afya, kilimo, Mkemia mkuu, waziri mkuu) huwa na zoezi la ufuatiliaji wa usalama wa vyakula lakini pia na urutubishwaji wa hivi vyakula (food safety and fortification assessment) ambapo sampuli huchukuliwa viwandani (mathalani unga wa ngano kwa Bakhressa au sembe hapo tandale kwa wasagaji wadogo au mafuta ya alizeti pale dodoma na kwingineko nchi nzima) sampuli pia huchukuliwa sokoni zinapouzwa (madukani, supermarket,kiosk kwa mangi nk). Sampuli hizi hupelekwa kupimwa kwenye maabara zetu za ndani (tbs,tfnc na mkemia mkuu) lakini pia baadhi hupelekwa maabara za nje ambazo huitwa reference labs.sasa majibu ya huu uchunguzi hurudishwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya utekelezaji (kwa kiwango gani utekelezaji unafanyika sijui).
Yote hayo, lakini kumbuka tupo dunia ya tatu. Mara ngapi vyakula vibovu vmeingizwa nchini kinyemela na kuuzwa?
 
Miaka ya hivi karibuni kumezuka viwanda vingi sana mitaani vinavyosaga unga wa mahindi na muhogo, ubora wa unga huo u atia mashaka kwani viwanda husika haviko kwenye usafi unaoridhisha.

Kiwanda ambacho hakiko kwenye usafi hata ubora wa unga wake utatia shaka, ni wazi viwanda hivyo vina mashine ya kukoboa na kusaga, havina mashine ya kusafisha nafaka husika hivyo kunauwezekano mkubwa kusagwa na takataka nyingine.

Nafaka zinazopatikana miaka hii huwa na uwezekano wa kuathirika na sumu kuvu na sumu zitokanazo na madawa ya kuhifadhia nafaka pamoja na ya kuua wadudu mashambani, haya yote ni hatari kwa afya zetu.

Ni jambo lililo wazi nchini kwetu hakuna utamaduni wa kichukua sampuli madukani na kwenda kuzipima maabara, TBS na TFDA nendeni madukani mchukue sampuli mkazipime naamini matokeo yatalishitua taifa kutokana na utitiri wa viwanda vya vichochoroni.
Mitaaani maana yake ni nini? Viwanda unavyovitambua wewe viko mbinguni siyo mitaani?
 
Mitaaani maana yake ni nini? Viwanda unavyovitambua wewe viko mbinguni siyo mitaani?
Kuna maeneo ya viwanda na maeneo ya makazi kama vile mtaani kwako, maeneo ya makazi yanatambuliwa kwa mitaa na maeneo ya viwanda yanatambuliwa kwa barabara.
Nimekujibu tu pamoja na dharau yako ya ujuaji.
Naona wewe haujui kama kuna madhara kwenye nafaka tunazotumia, wewe shida yako ni mitaa tu.
 
Dogo acha woga na wasiwasi. Tanzania na watanzania tuna Mungu na ndio mlinzi wetu Ndo sababu bado tunasurvive licha ya shida zetu. Jiulize kipindupindu tu kimeshindwa kutufyeka nini tena Zaid kitatuondoa? Mungu wa mbinguni Ndo mlinzi wetu na tegemeo letu. Usiwe na hofu kabisa bwanamdogo hakuna madhara yoyote yatakayotutokea kwa sababu Mungu wa Israel atatulinda.
 
Kula dona aliyoandaa mkeo nyumbani kwa kuosha na kusafisha kabisa ile sumu ya kuhifadhia nafaka.
Hakuna mfanyabiashara anaejali afya yako bali pesa yako. Hapo ujala chapati zilizogeuzwa kwa sponchi, ugali uliofunikiwa nylons juu eti usipoe, samaki waliofungiwa gazette.
Maisha haya ukipona kansa ni kumtukuza Sana Mungu.
 
Tatizo siyo ujuaji. Wewe unashindwa kueleza tatizo unaloliona badala yake unaelekeza mashambulizi kwa uwekezaji ulio karibu na unakoishi bila kujua wanavyo manage regulatory compliance requirements kwa uwekezaji wao. Ukiingia huko ndiyo utapata nafasi ya kujua na kuacha kuwapiga vita. Acha kuogopa kisichokuwepo.
Kuna maeneo ya viwanda na maeneo ya makazi kama vile mtaani kwako, maeneo ya makazi yanatambuliwa kwa mitaa na maeneo ya viwanda yanatambuliwa kwa barabara.
Nimekujibu tu pamoja na dharau yako ya ujuaji.
Naona wewe haujui kama kuna madhara kwenye nafaka tunazotumia, wewe shida yako ni mitaa
 
Serikali ya Samia ni wakati muafaka sasa kuirudisha TFDA maana TBS imeshindwa kusimamia masuala mazima ya ukaguzi na udhibiti wa ubora wa chakula na vipodozi nchini.

Hivyo kuhatarisha afya za watanzania.

#MaendeleoHayanaChama
 
Now ni TMDA sio TFDA
 
TBS inaonekana wazi imeacha kusimamia ubora wa viwango vya bidhaa baada ya kupewa ulaji wa bandarini.
Hivi sasa mchele tunaokula unawekwa mafuta tusiyoyajua ni ya nini ingawa baadhi ya watu wanadai ni ya upako.
Unga wa dona nao ni balaa kwani huchukuliwa unga wa sembe kisha huchanganywa na pumba na kusagwa ili kupata dona, sasa mara nyingi pumba huwa zimeanza kuvunda kutokana na joto zilizo nazo hivyo ni rahisi kuhatarisha maisha ya walaji wa dona.
 
(food safety and fortification assessment)

Katika mambo yote kuhusu vyakula vya nafaka, mimi naogopa sana hicho kitu kinachoitwa "fortification" kinachofanyika katika unga wa sembe.

Kwa fikra zangu hizo fortifications ni "slow killing poisons" za kuua watu weusi kwa siri, ni mpango wa wazungu, tunanunua sumu kujiua sisi wenyewe. Unless TBS etc, watuambie hizo fortifications zinaongeza kitu gani katika miili yetu na kwa utafiti upi walioufanya.
 
Kula dona aliyoandaa mkeo nyumbani kwa kuosha na kusafisha kabisa ile sumu ya kuhifadhia nafaka.
Hakuna mfanyabiashara anaejali afya yako bali pesa yako. Hapo ujala chapati zilizogeuzwa kwa sponchi, ugali uliofunikiwa nylons juu eti usipoe, samaki waliofungiwa gazette.
Maisha haya ukipona kansa ni kumtukuza Sana Mungu.

Kwa asiyekuwa na mke?!🤣
 
Back
Top Bottom