Mkuu kwa uelewa wangu TBS pamoja na taasisi ya chakula na lishe (TFNC) kwa kushirikiana na taasisi binafsi pamoja na za serekali (Tamisemi, afya, kilimo, Mkemia mkuu, waziri mkuu) huwa na zoezi la ufuatiliaji wa usalama wa vyakula lakini pia na urutubishwaji wa hivi vyakula (food safety and fortification assessment) ambapo sampuli huchukuliwa viwandani (mathalani unga wa ngano kwa Bakhressa au sembe hapo tandale kwa wasagaji wadogo au mafuta ya alizeti pale dodoma na kwingineko nchi nzima) sampuli pia huchukuliwa sokoni zinapouzwa (madukani, supermarket,kiosk kwa mangi nk). Sampuli hizi hupelekwa kupimwa kwenye maabara zetu za ndani (tbs,tfnc na mkemia mkuu) lakini pia baadhi hupelekwa maabara za nje ambazo huitwa reference labs.sasa majibu ya huu uchunguzi hurudishwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya utekelezaji (kwa kiwango gani utekelezaji unafanyika sijui).