Tetesi: TBS wamesema mzigo huo ni mafuta ghafi (crude oil), wakati TRA wanadai ni 'semi-refined'.

Meli mbili zenye mafuta ya kula tani 62 zimekwama kwa zaidi ya wiki mbili katika Bandari ya Dar kufuatia mvutano juu ya aina ya mzigo uliomo kwenye meli hizo na kodi wanayotakiwa kulipa. TBS wamesema mzigo huo ni mafuta ghafi (crude oil), wakati TRA wanadai ni 'semi-refined.'

MYTAKE:
kati ya TRA na TBS nani yupo sahihi? au hivi vyombo haviaminiani?
Inanikumbusha ya makinikia hii kitu.
TBS wako sahihi zaidi.. Japo kwa lugha ya TRA nayo pia ni sahihi
 
sio kweli mzee sio kila wanaloambiwa wakubaliane nalo: hao TRA ndio wanaowajua wakwepa kodi na wanajua wanakwepaje, hapo kuna kitu TRA wasipuuzwe hii awamu inataka kupunguza ujanja ujanja
Ni kweli mkuu,
Yawezekana kukawepo ujanja ujanja

Ila, TRA Ni vema wakafany kazi yao kwa weledi bila kushupaza mishipa ya shingo.

Maana,
Nna imani hao maafisa wa TRA wakiombwa wathibitishe kua

Hayo mafuta "Ni refined na sio Crude"

Nna imani hawatakua na hoja/ushahidi wa maana wa kutetea wanachokisema.

My take,
Wote TRA na TBS Ni ndugu wa baba mmoja

Wakae washauriane na wakubaliane.

WAKIENDELEA KULUMBANA WANAZIDI KUTUCHANGANYA SISI WANANCHI.

HII INAWEZA KUTUJENGEA HALI YA KUTOKUA NA IMANI NA VYOMBO VYETU HIVI

TULIVYOVIPA MAMLAKA YA KUSIMAMIA RASILIMALI ZETU NA MAPATO YETU.
 
Meli mbili zenye mafuta ya kula tani 62 zimekwama kwa zaidi ya wiki mbili katika Bandari ya Dar kufuatia mvutano juu ya aina ya mzigo uliomo kwenye meli hizo na kodi wanayotakiwa kulipa. TBS wamesema mzigo huo ni mafuta ghafi (crude oil), wakati TRA wanadai ni 'semi-refined.'

MYTAKE:
kati ya TRA na TBS nani yupo sahihi? au hivi vyombo haviaminiani?
Inanikumbusha ya makinikia hii kitu.
Mkuu usitulishe matango pori, tani 62 ni mzigo wa kubeba jahazi moja la kawaida tu toka TANGA KUJA PEMBA.
 
Nilikuwa nikiuliza TBS wanatoka wapi kwenye food regulations hapa nchini? Mbona mwenye jukumu la kutoa jibu la kimamlaka ni TFDA ambaye ndiye regulator wa drugs and Food hapa Tanzania?

Ukiona hivo kuna harufu ya rushwa nambapo impoter hataki kwenda TFDA (regulator) anataka kutumia TBS kama standard body kinamna.
TBS anasimamia Viwango na Ubora wa bidhaa zote zinazozalishwa nchini na zinazoingizwa nchini na jukumu la TFDA ni kusimamia Usalama kwa mtumiaji kwa bidhaa za chakula na madawa
 
Hao wote TBS na TRA walizoea kukatiwa "mchuzi" halafu mzigo unapita safari hii tumeweka mtego tutaona atakaeruhusu. Maagizo ya Rais yapo wazi kabisa kodi ilipwe Mara 2 au 3 kabisa ili huyo muagizaji akome. Ngoja tusubiri
Hilo la crude au semi refined ni dogo sana.
Hahaha ili kulinda viwanda vya ndani
 
Kazi kujua kama Ni refined au semi-refined Ni kazi ya TBS
(wazee wa ubora)

TFDA- Wao kazi yao Ni kukagua viambata sumu isije ikawa na athar za kiafya kwa mlaji

My take;
TRA kazi yao Ni kuichukua tu kauli ya TBS na kuifanyia kazi

TRA Hawana maabara ya kupima mafuta,

TBS ,ndo wenye maabara na mamlaka ya kupima ubora wa mafuta.

TRA KAZI YAO NI KUTEMBEZA TU KIBUBU
ie: kukusanya kodi kutokana na maelekezo kutoka TBS.
TRA watakuwa wameangalia kwa macho na kusema mbona yanaonekana kama semi-refined hivi? Wenzao wamepima kwenye maabara sasa sijui ubishi wa nini? Ukiona hivyo ujue TRA wametamani kupiga rushwa kubwa hapo sasa kinawauma sana kupita bila kulamba chochote hapo!! Hii inanikumbusha kuna taahira moja kwenye makinikia lilisema ule mchanga ulikuwa 90% dhahabu na ile 10% inayobaki ni mchanga halisi!!
 
Watu wanabishana na majibu ya maabara. TRA wanashupaa sana kutaka kumfurahisha bwana yule, mwisho wa siku wanaonekana ni wapuuzi wasio jua kazi. Anaejua aina za mafuta ni TBS na ndio mwenye maabara za upimaji.
 
Watakua wanapga mkwala ili wapate cha juu hapo.

Mh. rais inabd uwatizame hao jamaa wa mapato kwa jicho pevu zaidi
 
Meli mbili zenye mafuta ya kula tani 62 zimekwama kwa zaidi ya wiki mbili katika Bandari ya Dar kufuatia mvutano juu ya aina ya mzigo uliomo kwenye meli hizo na kodi wanayotakiwa kulipa. TBS wamesema mzigo huo ni mafuta ghafi (crude oil), wakati TRA wanadai ni 'semi-refined.'

MYTAKE:
kati ya TRA na TBS nani yupo sahihi? au hivi vyombo haviaminiani?
Inanikumbusha ya makinikia hii kitu.
Ni vema yawe Ghafi ikiwakinyume wamekwisha na kazi zao za mazoea.
 
Kazi kujua kama Ni refined au semi-refined Ni kazi ya TBS
(wazee wa ubora)

TFDA- Wao kazi yao Ni kukagua viambata sumu isije ikawa na athar za kiafya kwa mlaji

My take;
TRA kazi yao Ni kuichukua tu kauli ya TBS na kuifanyia kazi

TRA Hawana maabara ya kupima mafuta,

TBS ,ndo wenye maabara na mamlaka ya kupima ubora wa mafuta.

TRA KAZI YAO NI KUTEMBEZA TU KIBUBU
ie: kukusanya kodi kutokana na maelekezo kutoka TBS.
Lakini ujue TRA wanakitengo cha uchunguzi kuna uwezekano wametonywa na wasiri wao kuwa mzigo ni semi refined!!
 
Watu wanabishana na majibu ya maabara. TRA wanashupaa sana kutaka kumfurahisha bwana yule, mwisho wa siku wanaonekana ni wapuuzi wasio jua kazi. Anaejua aina za mafuta ni TBS na ndio mwenye maabara za upimaji.
Mkuu huo ni mtego umenasa, nikama Makinikia vile.
We subiri uone movie, watu wataumbuka.
 
TBS anasimamia Viwango na Ubora wa bidhaa zote zinazozalishwa nchini na zinazoingizwa nchini na jukumu la TFDA ni kusimamia Usalama kwa mtumiaji kwa bidhaa za chakula na madawa
Ni kama vile kuna conflict of duties kati ya TBS na TFDA. TBS akishasema bidhaa hii kimekidhi ubora unaotakiwa TFDA anasimamia usalama gani tena wakati tayari chakula hicho ni bora na ni salama?
 
Tani 62000/620000
Nasema hivo sababu East Coast Oil and Fats kina uwezo wa zaidi ya tani 1000 kwa siku/ 23hrs

Hapo TRA hawatumii akili zao, wanafata tamko la bosi pale Ikulu siku ya wafanyabiashara
 
Meli mbili zenye mafuta ya kula tani 62 zimekwama kwa zaidi ya wiki mbili katika Bandari ya Dar kufuatia mvutano juu ya aina ya mzigo uliomo kwenye meli hizo na kodi wanayotakiwa kulipa. TBS wamesema mzigo huo ni mafuta ghafi (crude oil), wakati TRA wanadai ni 'semi-refined.'

MYTAKE:
kati ya TRA na TBS nani yupo sahihi? au hivi vyombo haviaminiani?
Inanikumbusha ya makinikia hii kitu.
Hapo penye uzito ni sawa? Nadhani tani 62 ni uzito mdogo kwa meli. Labda tani 62'000 kwa meli mbili!
 
Hicho ni chakula muhusika hasa ni TFDA, aje atuambie hicho ni nini hasa?
 
Back
Top Bottom