Tetesi: TBS wamesema mzigo huo ni mafuta ghafi (crude oil), wakati TRA wanadai ni 'semi-refined'.

Tetesi: TBS wamesema mzigo huo ni mafuta ghafi (crude oil), wakati TRA wanadai ni 'semi-refined'.

Meli mbili zenye mafuta ya kula tani 62 zimekwama kwa zaidi ya wiki mbili katika Bandari ya Dar kufuatia mvutano juu ya aina ya mzigo uliomo kwenye meli hizo na kodi wanayotakiwa kulipa. TBS wamesema mzigo huo ni mafuta ghafi (crude oil), wakati TRA wanadai ni 'semi-refined.'

MYTAKE:
kati ya TRA na TBS nani yupo sahihi? au hivi vyombo haviaminiani?
Inanikumbusha ya makinikia hii kitu.


Hatuwezi kusema nani mkweli na nani mwongo kama hatujauona huo mzigo bayana
 
ikumbukwe Mh.Rais alisema akiwa Singida..(wengine wanaleta mafuta wanasema n crude oil na wengine mnao hapa hapa) kwa kauli hii n wazi MO aendelee na biashara zingine. tuko kwene vita ya kiuchumi ila bado hatujajua tunapgana nan...
Kama ni hivi basi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS ajiandae kisaikolojia! Lakini kama ana uhakika na taarifa za maabara yake awe na amani. Maabara ni msema kweli kama itatumika vizuri
 
Watu wanabishana na majibu ya maabara. TRA wanashupaa sana kutaka kumfurahisha bwana yule, mwisho wa siku wanaonekana ni wapuuzi wasio jua kazi. Anaejua aina za mafuta ni TBS na ndio mwenye maabara za upimaji.
Hivi kama wewe ni mwanamme na ukienda hospital kupima mkojo ukiambiwa una ujauzito utakubali tu kwa sababu ni majibu ya maabara? Nauliza hivi kwa sababu kwa nchi uliyojaa rushwa kama yetu pengine TRA wameona kuna kitu ambacho hakipo sawa ndiyo maana wakawa na wasiwasi. Nadhani tushauri uchunguzi wa kina ufanyike na siyo kulazimisha wakubali eti kwa sababu ni majibu ya maabara!
 
Back
Top Bottom