Tetesi: TBS wamesema mzigo huo ni mafuta ghafi (crude oil), wakati TRA wanadai ni 'semi-refined'.

TBS wako sahihi zaidi.. Japo kwa lugha ya TRA nayo pia ni sahihi
 
sio kweli mzee sio kila wanaloambiwa wakubaliane nalo: hao TRA ndio wanaowajua wakwepa kodi na wanajua wanakwepaje, hapo kuna kitu TRA wasipuuzwe hii awamu inataka kupunguza ujanja ujanja
Ni kweli mkuu,
Yawezekana kukawepo ujanja ujanja

Ila, TRA Ni vema wakafany kazi yao kwa weledi bila kushupaza mishipa ya shingo.

Maana,
Nna imani hao maafisa wa TRA wakiombwa wathibitishe kua

Hayo mafuta "Ni refined na sio Crude"

Nna imani hawatakua na hoja/ushahidi wa maana wa kutetea wanachokisema.

My take,
Wote TRA na TBS Ni ndugu wa baba mmoja

Wakae washauriane na wakubaliane.

WAKIENDELEA KULUMBANA WANAZIDI KUTUCHANGANYA SISI WANANCHI.

HII INAWEZA KUTUJENGEA HALI YA KUTOKUA NA IMANI NA VYOMBO VYETU HIVI

TULIVYOVIPA MAMLAKA YA KUSIMAMIA RASILIMALI ZETU NA MAPATO YETU.
 
Mkuu usitulishe matango pori, tani 62 ni mzigo wa kubeba jahazi moja la kawaida tu toka TANGA KUJA PEMBA.
 
TBS anasimamia Viwango na Ubora wa bidhaa zote zinazozalishwa nchini na zinazoingizwa nchini na jukumu la TFDA ni kusimamia Usalama kwa mtumiaji kwa bidhaa za chakula na madawa
 
Hahaha ili kulinda viwanda vya ndani
 
TRA watakuwa wameangalia kwa macho na kusema mbona yanaonekana kama semi-refined hivi? Wenzao wamepima kwenye maabara sasa sijui ubishi wa nini? Ukiona hivyo ujue TRA wametamani kupiga rushwa kubwa hapo sasa kinawauma sana kupita bila kulamba chochote hapo!! Hii inanikumbusha kuna taahira moja kwenye makinikia lilisema ule mchanga ulikuwa 90% dhahabu na ile 10% inayobaki ni mchanga halisi!!
 
Watu wanabishana na majibu ya maabara. TRA wanashupaa sana kutaka kumfurahisha bwana yule, mwisho wa siku wanaonekana ni wapuuzi wasio jua kazi. Anaejua aina za mafuta ni TBS na ndio mwenye maabara za upimaji.
 
Watakua wanapga mkwala ili wapate cha juu hapo.

Mh. rais inabd uwatizame hao jamaa wa mapato kwa jicho pevu zaidi
 
Ni vema yawe Ghafi ikiwakinyume wamekwisha na kazi zao za mazoea.
 
Lakini ujue TRA wanakitengo cha uchunguzi kuna uwezekano wametonywa na wasiri wao kuwa mzigo ni semi refined!!
 
Watu wanabishana na majibu ya maabara. TRA wanashupaa sana kutaka kumfurahisha bwana yule, mwisho wa siku wanaonekana ni wapuuzi wasio jua kazi. Anaejua aina za mafuta ni TBS na ndio mwenye maabara za upimaji.
Mkuu huo ni mtego umenasa, nikama Makinikia vile.
We subiri uone movie, watu wataumbuka.
 
TBS anasimamia Viwango na Ubora wa bidhaa zote zinazozalishwa nchini na zinazoingizwa nchini na jukumu la TFDA ni kusimamia Usalama kwa mtumiaji kwa bidhaa za chakula na madawa
Ni kama vile kuna conflict of duties kati ya TBS na TFDA. TBS akishasema bidhaa hii kimekidhi ubora unaotakiwa TFDA anasimamia usalama gani tena wakati tayari chakula hicho ni bora na ni salama?
 
Tani 62000/620000
Nasema hivo sababu East Coast Oil and Fats kina uwezo wa zaidi ya tani 1000 kwa siku/ 23hrs

Hapo TRA hawatumii akili zao, wanafata tamko la bosi pale Ikulu siku ya wafanyabiashara
 
Hapo penye uzito ni sawa? Nadhani tani 62 ni uzito mdogo kwa meli. Labda tani 62'000 kwa meli mbili!
 
Hicho ni chakula muhusika hasa ni TFDA, aje atuambie hicho ni nini hasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…