TBS: Wanaoongeza maji kwenye maziwa waonywa, kufanya hivyo ni kinyume cha sheria

TBS: Wanaoongeza maji kwenye maziwa waonywa, kufanya hivyo ni kinyume cha sheria

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
KAIMU Mkuu wa Kitengo Cha Uthibiti Ubora wa Shirika la Viwango nchini (TBS) Baraka Mbajige amewaonya wafugaji na wauzaji wa maziwa kuacha tabia ya kuweka maji kwa sababu ni kinyume cha sheria.

Alisema hayo katika mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na TBS kwa wafugaji wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kuwa adhabu ya mfugaji anayeweka maji kwenye maziwa ni faini ama kufungiwa.

Kwaupande wake Meneja Utafiti wa Mafunzo Sudi Mwanansela alisema kuwa TBS wamefanya mafunzo hayo ikiwa na lengo la kuwapa elimu ya namna ya usindikaji, ubebaji Ili kuweza kuyapandisha thamani sokoni na kwa mlaji kwa ujumla.

"Tutakuwa na mafunzo kwa siku mbili. hapa Kibaha ambapo tutajifunza kwa kutoa elimu na pia tutakwenda kuwafundisha kwa vitendo ambapo tutakwenda kuwatembelea kwenye maeneo ya na kuona namna wanavyofuga na kung'amua changamoto wanazozipitia Ili tuone namna ya kuweza kuwasaidia kuzitatua" alisema Mwanansela.

Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ambapo amewataka wafugaji hao kuondoka na maazimio ya kukua katika sekta hiyo ya maziwa na kuwataka wakati ujao waweze kuandaa Kongamano kubwa ambapo pia waweze kuwaita wadau wakubwa wakiwemo Idara ya Lishe ambao wataweza kujadili kwa kina suala.la udumavu na umuhimu wa unywaji maziwa.

Michuzi Blog
 
Back
Top Bottom