TBT: Ajali ya moto Morogoro (2019), ni lipi la kujifunza?

TBT: Ajali ya moto Morogoro (2019), ni lipi la kujifunza?

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
673
Reaction score
1,318
Kwenye tarehe 10 Agosti 2019, Tanzania ilikumbwa na tukio la kusikitisha na kutisha ambalo limebaki kuwa kumbukumbu mbaya kwa wengi.

Ajali ya moto iliyotokea mjini Morogoro, karibu na eneo la Msamvu, ilihusisha lori la mafuta lililopinduka na kulipuka, na kupelekea vifo vya watu zaidi ya 100. Tukio hili lilitokeza huzuni na mshtuko kwa taifa na kuacha alama isiyofutika kwenye historia ya nchi.
IMG_8294.jpeg
Tukio lilianza pale ambapo lori la mafuta lilipata ajali na kupinduka. Baada ya kuanguka, watu wengi walikusanyika kwa haraka kuchota mafuta yaliyokuwa yakimwagika kwenye eneo la tukio. Watu walijitokeza kutoka maeneo mbalimbali wakiwa na ndoo, madumu, na chupa ili kupata mafuta. Baadaye, ghafla moto ulilipuka kwenye eneo hilo, na kusababisha maafa makubwa kwa waliokuwa karibu.

Pamoja na kwamba haijathibitishwa chanzo rasmi cha moto, baadhi ya mashuhuda walieleza kuwa ulitokana na cheche za moto kutoka pikipiki au sigara iliyokuwa ikivutwa karibu na eneo la tukio. Mlipuko huo ulitokea ghafla na kuteketeza eneo zima, ukiwaacha watu wakiwa wamejeruhiwa vibaya na kuharibu mali zao.

Mara baada ya tukio hilo, viongozi wa kitaifa walitembelea eneo la ajali ili kutoa pole kwa waathirika na kushuhudia hali ya kusikitisha iliyotokea. Rais wa wakati huo, John Pombe Magufuli, alitangaza siku ya maombolezo ya kitaifa kwa heshima ya waliopoteza maisha. Viongozi wa kidini na wa kijamii pia walitoa misaada na ushauri kwa familia za waathirika na walitoa wito kwa Watanzania kuwa makini na ajali kama hizi.

Ikiwa leo ni alhamisi ya TBT, tukio la moto la Morogoro limebaki kuwa la kihistoria kwa taifa. Kwa pamoja, tunapaswa kujifunza kutokana na ajali kama hizi, kuwa makini na tahadhari, na kuhamasisha jamii kuhusu hatari zinazoweza kutokea. Em tuambie, Ulipata Funzo gani kutokana na Ajali hii?

Mwisho, napenda kutoa pole kwa familia zote ambazo zilipoteza wapendwa wao kwenye ajali hii na tunaiomba serikali iendelee kuchukua hatua kuhakikisha usalama wa raia wakati wa dharura kama hizi.​
IMG_8295.jpeg
 
Watu wachache Sana ambao wamepata funzo kutokana na tukio hilo baya. Elimu ya kujihami na majanga au ajali za namna hiyo bado haijawafikia Watu wengi.

Na kwa bahati mbaya zaidi, kwa hapa Tanzania kuna maandalizi makubwa Sana ya kutengeneza ajali za namna hii humu majumbani mwetu kupitia maamuzi mabaya yaliyofanywa na Serikali ya kuhamasisha na kuanzisha kwa ghafla kwa matumizi ya majiko ya gesi bila ya kuanza na hatua muhimu sana na ya LAZIMA ya Utoaji wa Elimu sahihi juu ya matumizi ya majiko hayo ya gesi.

Wananchi wengi Sana wanaishi na Vilipuzi au Mabomu (Majiko ya Gesi) kwenye vyumba na nyumba zao wanazoishi huko mitaani. Watu wengi Sana hawana uelewa au elimu ya kutosha kuhusiana na suala zima la usalama wao binafsi, uhifadhi na matumizi sahihi ya majiko ya gesi.
 
Ndani ya mwezi huu october 2024 nigeria na uganda wamepotea watu karibia 200 kwa kuchota mafuta.

Umaskini wetu unasababisha watu kutowaza athari zinazoweza kutokea bali kufikiri tu fursa iliyopo mbele yake.
 
Hatuna madaktari Tanzania, tuna wahuni wenye kujua kuchoma sindano tu.

Wagonjwa walilazwa kwenye vitanda kwa zaidi ya wiki nzima ndipo wakaanza kufa mmoja baada ya mwingine mpk wakaisha wote. So sad!

Nililaani sana kitendo hiki cha serikali kulazimisha majeruhi wa moto watibiwe kwenye hospitali zetu hizi duni zenye wataalamu duni na vifaa duni.

Daah!
Nachokumbuka kabla ya tukio siku kadhaa nyuma US tahadhari kuhusu tukio la ugaidi.
 
Hatuna madaktari Tanzania, tuna wahuni wenye kujua kuchoma sindano tu.

Wagonjwa walikalishwa kwenye vitanda kwa zaidi ya wiki nzima ndipo wakaanza kufa mmoja baada ya mwingine mpk wakaisha wote. So sad!
Inaumiza sana🥹
 
Poleni sana kwa wote waliopitia masahibu haya ya mlipuko WA Lori Hilo la mafuta
 
Msemo wa "kuchomoa betrii" ulianzia kwenye hili tukio.

Moto ulisababishwa na mtu mmoja kutaka kuondoka na batteries za gari. Cheche halafu booooooom!
RIP wahanga.
 
Waafrika hatuna la kujifunza, tukio linatokea Leo, tutasikitika, Kisha tutasahau. Tukio kama Hilo likitokea tena, majanga yatajirudia vile vile.

Nakumbuka muda mfupi tangu tukio la Morogoro kutokea, ikatokea Tena Kagera Lori la mafuta ya petrol likapinduka. Bila vyombo vya usalama kuwahi katika eneo la tukio, wananchi wa eneo husika walikwenda na madumu kuchota mafuta. Tafsiri yake, janga lilelile la Morogoro lingetokea Kagera ndani ya muda mfupi.

Mifano mingine ni kutoka nchi jirani: Kenya imetokea, Nigeria wiki chache zilizopita limetokea, Uganda imetokea, DR Congo imetokea. Mazingira ya matukio yanafanana: Gari la mafuta kupinduka=>Mafuta kumwagika=>Wananchi kukimbilia kuchota mafuta=>Moto kulipuka=>Watu kufa.

Hatujifunzi kutoka Kwa waliyowakuta majirani zetu, hatujifunzi Kwa yaliyotokea miaka ya nyuma.

Binadamu (hususani Waafrika) ni wepesi kusahau, hatuna utamaduni wa kutunza kumbukumbu ya madhara ya matukio yaliyopita. Huwa tunajifariji kwamba "ilikuwa ajali kazini".

Tafakuri yangu: "Hiyo yote ni Kwa sababu ya umaskini mkubwa uliopo katika jamii nyingi za kiafrika".
Na ndiyo sababu ya watu kutojali kuhusu kumbukumbu, hawajali kuhusu kujifunza ya Yale yaliyotokea kipindi Cha nyuma.
 
Umeongea point sanaa, umasikini unatufanya turisk sana maisha yetu🥹​
 
Back
Top Bottom