TBT: Foleni ya kwenda kwa Babu wa Loliondo

Ipi ilikuwa ni race kubwa kati ya hao Wazungu, Wachina na Watanzania?

Hata kama wengine walienda kwaajili ya kutalii lakini ukweli ni kwamba wengi walienda kule kwaajili ya kunywa Kikombe cha Babu

Pamoja na Utanzania wangu, lakini haindoi kusema madhaifu yetu ya Ujinga na maradhi

Haiwezekani umtoe mgonjwa hospitali ya Taifa Muhimbili kisha umpeleke akanywe Kikombe eti ndiyo apone

Kama una akili timamu na umeelimika hauwezi kufanya huo Ujinga
 
huyo babu aliibuliwa na serikali na hakuna alichokuwa anatibu.

Wagonjwa wengi walioenda kwake walikuwa ni wagonjwa wenye ukimwi.

Na hawa wenye ukimwi ndo walisambaza hizi taarifa kuwa wamepona hili na wenzao wakapoteze kama wao.

Issue ya wazungu na wachina -hao wazungu wenye akili za kijinga wapo wengi sana na wachina pia hawa wanaoleta kamari.


Kizazazi cha 1950-1980 ni kizazi cha hovyo Sana

Unafikiri vijana wa 1990s unaweza kuwaletea huu ujanja ,mwaposa hadi Leo anawakamua Hicho hicho kizazi.
 
Miaka ijayo tutaona na za kwenda kwa mwamposa
 
Haya mambo bado yapo na hawa watu wanatengenezwa ana wazee wa kijani.. sasa hv watu wanakodi magari kutoka mwanza, bukoba n.k ili j2 wawe kwa yule mchungaji mwamposa then wanarudi walipotoka.
Ni aina nyingine ya kuwehuka
 
Ambilikile Mwasapile (Babu wa Loliondo)

Kuna dogo mwingine aliibuka Mbeya Mjini- Mabatini nae alitoa kikombe alipata maokoto akaishia kununua pikipiki na kuangukia kwa warembo
 
Mzee alikufa bila kutaja formula
Ameacha wasaidizi nazani formula watakua nayo kama wataalamu wapya wanaweza fanya research ya huo mzizi kwa kina zaidi tunaweza pata kitu gani Babu aliona kwenye huo mzizi,and why huo tu na si mzizi mingine,je alionja yeye kwanza ndiyo akaileta kwa wananchi au aliileta bila kujaribu!? Je kama ingekua ni sumu nani angekufa kwanza!!??
 
Kweli ni kweli mzee nyie kizazi chenu mlikuwa mnapenda Sana chini ? Au tetesi tu?
Haikuwa sana kama nyie

Miaka yenu hii maeneo ya kufanyia matukio yamekuwa mengi, iwe ni kwenye gari/beach/lodges/hotel n.k

Miaka yetu ilikuwa hadi umvizie shambani ama akiwa anaenda kuchota Maji kisimani
 
Sio suala la mshahara wa madaktari tu pia kipindi hicho ndo social media zinaanza kushika kasi (miaka hiyo ndo wengi walianza kufuatilia mitandaoni na ishu za kisiasa zilizoshika kasi sana kipindi hicho ni ishu ya kigogo mmoja wa B. O. T ambaye inasemekana alihusika na wakubwa flani kwenye upigaji wa pesa ndefu kisha alidaiwa kufariki akiwa ughaibuni na kuzikwa huko kimya kimya lakini baada ya siku chache tu zikaibuka taarifa kwamba mwamba yuko hai huko ughaibuni anajitafunia cake ya taifa kimya kimya bila nzi kumgusa na kuna watu wakajitokeza kudai wanajua mpaka anapolala!
Hilo na mengine mengi ya upigaji kipindi hicho ndo ikabidi itafutwe ishu mbadala ambayo itahamisha upepo wa fikra za wananchi na vyombo vya habari vyote habari kubwa iwe moja
Ndo ukasukwa mpango kabambe wa babu wa loliondo ambapo viongozi wakubwa serikalini ndo walianza kwenda kunywa dawa kwa babu Kisha maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya nchi wakafurika kijijini hapo kupata "tiba" hiyo ya mchongo!
Finally deal done.!!! Vyombo vyote vya habari na mitandaoni habari kuu ikawa babu wa Loliondo zile ishu zote za mwanzo ikiwemo ya "marehemu aliyefia ughaibuni kufufuka" zikasahaulika mpaka leo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…