TBT: Mnawakumbuka hawa jamaa..?

TBT: Mnawakumbuka hawa jamaa..?

Niliibiwa kisalfeti changu kilichojaa daftar za shule.. ili home wasijue nilikua naingia kininja natoka kininja. Nilikaa kama wiki mbili siandiki ila naenda shule kuiba daftar tu! Nilimilisha zimefika daftar 20 mpya... daftar zikimwaga kutoka kusahushwa nami najichanganya
Nikiwa darasa la 4 niliibiwa kitabu cha sayansi na mwalimu akatoa vitisho kuwa lazima aliyepewa kitabu arudishe mwisho wa muhula kabla hatujafunga shule.

Nikakitafuta pasipo mafanikio, nikasema isiwe tabu nikaiba vitabu vyote vya sayansi, vilikuwa 12 nikapeleka nyumbani. Nikamfuata mwalimu nikamwambia nimepata kitabu changu akasema Good. Wengine wote msala ukabaki kwao.
 
Shuleni tulikuwa tunashindana wizi wa vitu. Yaani ilitakiwa utumie akili uingie darasa lingine uibe na urudi na kitu darasa kwenu uoneshe wenzako kuwa umeiba darasa fulani.

Sasa vijana tukajifanya Scofield na kuanza kutumia akili na kweli wengi wao walifanikiwa mimi nawachora tu. Siku moja nikawaambia mimi siwezi kuiba humu madarasani kwa sababu hakuna mwanafunzi ataweza kuruka mtego wangu.

Mchana nikazama ofisini kwa Headmaster nikampa stori nyingi za uongo na kweli akaanza kukenua meno anacheka kumbe mimi nataka nitoke na kitu chochote ofisini kwake nikawaoneshe darasani. Kama dakika 5 mzee akajaa kwenye 18 nikapiga kalamu yake nyekundu nikamuaga Mwl mimi narudi darasani.

Nikafika class nikawaonesha na kutaka mtu alipe nilichofanya, hakuna aliyeweza. Basi nikawataka waache wizi maana hawajui kuiba.

Hahaha kaka we fundi sana ila lipa hii

Mi nliwaahidi kutoka na mwalimu amina na mtoto wa head mistress
 
Simulizi za Esopo
HADITHI ZA ESOPO....
KISA CHA MCHEKESHAJI NA MWANAKIJIJI
Hapo zamani kulikuwepo mtu mmoja tajiri aliyeheshimika sana na watu wa jamii yake. Bwana huyo alifungua majumba ya maonyesho ya sanaa na watu wote waliruhusiwa kuingia bure. Wake kwa waume, watoto na wakubwa. Ikawa baada ya kazi nyingi za kutwa za kujitafutia riziki, Wananchi wakapata burudani na kufurahi pamoja.
Ila kwa kuwa maonyesho yalifanyika mara kwa mara, na wasanii walikuwa ni wale wale, na burudani ni zilezile zikijirudiarudia, siku zilipopita mambo yalianza kwenda doro kwa idadi ya wahudhuriaji kupungua na msisimko nao kushuka.
Yule tajiri alifikiri namna ya kufanya ili kuwarudisha watu katika uchangamfu kama awali.
Siku moja alitoa tangazo kwa umma akiahidi kutoa zawadi nono sana kwa mtu yeyote atakayeweza kufanya uvumbuzi wa aina mpya kabisa ya burudani jukwaani.
Watu kemkem wenye uzoefu katika tasnia ya kuburudisha umma kwa nyimbo, maigizo, vichekesho nk; walijitokeza kuishindania zawadi ile.
Miongoni mwao alikuwapo Mchekeshaji ambaye alikuwa maarufu sana kutokana na vichekesho vyake mahiri.
Alijitokeza na kusema kuwa yeye ana aina mpya kabisa ya burudani ambayo haijawahi kuonyeshwa jukwaani kabla. Na wala hakuna mtu yeyote atakayeweza kushindana naye. Alijigamba, na walio wengi walimwamini.
Habari ile ilisambaa kama upepo na kuleta hamasa kubwa, ikawa gumzo kila pahali. Na siku ya shindano ilipofika ukumbi ulijaa ukatapika. Waliochelewa kufika walilazimika kusikiliza wakiwa nje.
Kila kitu kiliandaliwa vizuri na muda ulipofika mambo yakajiri kama ilivyopangwa.
Baada ya wengine kutoa burudani zao, kila mtu akishangiliwa na kutuzwa kwa kadiri yake, ikafika zamu ya yule aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu.
Mchekeshaji alitokea jukwaani peke yake, bila kifaa cha aina yoyote wala washirika. Shauku kubwa ya matarajio chanya vilipelekea ukumbi kugubikwa na kimya kikuu. Watu wakisubiri kwa hamu kushuhudia kichekesho kipya walichoahidiwa na msanii yule nguli. Akiwa amevalia joho lake refu la rangi ya hudhurungi, ghafla alijipinda na kuinamisha kichwa chake kuelekea tumboni, kisha akatoa sauti kali ya kuiga mlio wa kitoto cha Nguruwe. Mlio huo aliouiga kwa sauti yake ulikuwa wa kupendeza kiasi kwamba hadhira ile ikamshuku kuwa huenda alikuwa ameficha kitoto cha Nguruwe kwenye vazi lake pana. Wakadai akaguliwe ili kuhakikisha, kabla hawajampa sifa na kumtawaza kuwa ni mshindi halali wa zawadi inayoshindaniwa.
Baada ya kufanya hivyo na kukutwa hana kitu chochote alichoficha, ukumbi ulilipuka kwa mayowe ya furaha na kushangilia usanii ule mpya.
Mwanakijiji mmoja miongoni mwa hadhira alipoyashuhudia yale yote, alipata wazo na kusema, “Nisaidieni enyi wakuu, mimi pia naweza, najua hawezi kunishinda katika kuiga sauti kama hii.” Na hapo hapo alitangaza kuwa ataigiza sauti kama vile siku inayofuata, na itakuwa kwa ubora na uhalisia zaidi. Na akawaomba wananchi watulie kwani mshindi wa kweli wa zawadi ile atatambulika baada ya yeye pia kupewa nafasi ya kusikilizwa.
Kesho yake umati mkubwa zaidi ulifurika kwenye jumba la maonyesho, wakiwa na mapenzi na ushabiki kwa Mchekeshaji, na wengi walikuja kwa lengo la kutaka kumdhihaki na kumsuta Mwanakijiji, na sio kushuhudia uwezo wake wa kuiga sauti vizuri kuzidi ile ya msanii aliyepita.
Wasanii wote walitokea jukwaani. Mchekeshaji alikuwa wa kwanza, alijiinamia tumboni na kuiga sauti ya kitoto cha nguruwe, kama siku iliyopita, na hadhira ilimshangilia sana kwa mbinja na vifijo.
Ndipo Mwanakijiji akapewa nafasi, akainama na kujifanya kama ameficha kitoto cha nguruwe kwenye vazi lake (ambapo ni kweli alikificha, ila hakuna aliyemshuku) alishika na kuyanyonga masikio, na mlio mkali wa kitoto cha nguruwe ulisikika.
Watazamaji, hata hivyo, walipaza sauti kwa pamoja wakisema kuwa yule Mchekeshaji aliyepita ndiye mshindi kwani aliiga mlio wa kitoto cha nguruwe kwa ufasaha zaidi. Wakataka Mwanakijiji aburuzwe nje ya jumba lile. Ndipo yule mshamba akakitoa kitoto halisi cha nguruwe kwenye mavazi yake, na kuionyesha hadhira ushahidi chanya kuhusu upotofu wa hukumu waliyotoa.
“Tazameni,” alisema, “hii inadhihirisha wazi ninyi ni aina gani ya mahakimu!”
FB_IMG_1566462285716.jpeg
FB_IMG_1566462281819.jpeg
 
Nikiwa darasa la 4 niliibiwa kitabu cha sayansi na mwalimu akatoa vitisho kuwa lazima aliyepewa kitabu arudishe mwisho wa muhula kabla hatujafunga shule.

Nikakitafuta pasipo mafanikio, nikasema isiwe tabu nikaiba vitabu vyote vya sayansi, vilikuwa 12 nikapeleka nyumbani. Nikamfuata mwalimu nikamwambia nimepata kitabu changu akasema Good. Wengine wote msala ukabaki kwao.
Hahaaaaaaaa mkuu hiyo dhambi mkuu.. mimi darasa la sita ndio nilipoteza kitabu cha sayansi sikua na amani kabisa na shule ila ticha sijui alinipotezea au vipi
 
Hahaha kaka we fundi sana ila lipa hii

Mi nliwaahidi kutoka na mwalimu amina na mtoto wa head mistress
Hapana sikuwa na mambo ya ngono ngono mkuu nikiwa shule hata katika ujana wangu. Nilikuwa busy na mpira na uchokozi ila huko nilikuwa mtazamaji tu mkuu. Na lilipokuwa linakuja kwenye suala la kutumia akili nilikuwa najiweza sana kufanya kitu na ushahidi usibaki.
 
Hekaya za Abunuwasi
Kuna wakati, Abunuwasi aliamua kuwa mfuga mbuzi. Alinunua mbuzi wa kufuga huku akiwa na lengo la kujiongezea kipato chake pindi mbuzi huyo atapoanza kuzaa, ili awafuge wawe wengi na kumuwezesha kuwa tajiri kuliko wote waliokuwepo katika mji ule..

Siku moja Abunuwasi alipokuwa anampeleka mbuzi wake malishoni, alikuta kiatu kimoja kizuri sana katikati ya njia. Alisimama na kukiangalia. Kiatu kilimpendeza machoni mwake ila akasema "kiatu hiki ni kizuri lakini mbona kipo kimoja tu?" Alitafuta kiatu cha pili pembezoni mwa njia ila hakukiona. Alipoona hawezi kuvaa kiatu kimoja, aliamua kukiacha palepale. .

Abunuasi akachukuwa mbuzi wake na mbele kidogo akaona kile kiatu cha mguu wa pili. Abunuwas alishangaa na akaona bora angelikichukua kile cha mwanzo kwa sababu cha pili kimepatikana.akamua kufunga mbuzi wake pembezoni mwa barabara ili afuate kile kiatu alichokiacha.

Aliporudi pale mwanzo kukitafuta kile kiatu alichokiacha awali lakini hakukikuta tena, alijaribu kukitafuta lakini hakukiona. Basi akadhani kuna mtu amekiokota. Akarudi haraka alipomfunga mbuzi wake nako pia hakumkuta mbuzi wala kile kiatu kimoja. Mwisho akawa amemkosa mbuzi na viatu, Ndoto zote za Abunuwasi kupata utajiri zikaruka na akabaki na umasikini wake kwa sababu ya tamaa yake

TUNAPASWA TUSIWE NA TAMAA,,,,WALA KUDHARAU VITU
FB_IMG_1566462671768.jpeg
 
Hahaaaaaaaa mkuu hiyo dhambi mkuu.. mimi darasa la sita ndio nilipoteza kitabu cha sayansi sikua na amani kabisa na shule ila ticha sijui alinipotezea au vipi
Shuleni uchangamfu ni kitu kizuri sana ukibung'aa watakupanda kichwani. Licha ya kuwa mdogo ila nilikuwa sikubali kunyanyasika kizembe.

Nikiibiwa sitafuti mwizi, mimi naibia wengi ili tuonekane tumeibiwa wengi.
 
Hahaa enzi hzo tukitoka mstarini tunakimbizana kiwahi dawati sasa mm rafk zangu kama walikua washanijuloa nikiwahi nafasi wnanitkenya hadi nawaachia nachukua kipande cha tofali naenda kukaa mbele huko
 
Hahaha kaka we fundi sana ila lipa hii

Mi nliwaahidi kutoka na mwalimu amina na mtoto wa head mistress
Ilikuwa darasa la pili nakumbuka, nilichaguliwa kuwa Monitor. Kumbe darasa lile halikujua kuwa limefanya kosa kubwa sana kunipa madaraka.

Nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Juma alikuwa mkubwa kuliko mwanafunzi yeyote mle darasani, na ndiye alikuwa Mayweather wa darasa. Hivyo nikamteua awe kama msaidizi wangu kutokana na ubabe wake.

Shule yetu ilikuwa na kelele kama kundi la nzige ila darasa langu muda wote lilikuwa kimya sana kama vile hakuna mwanafunzi. Nilikuwa sina utaratibu wa kuandika majina ya wapiga kelele, mimi na Juma tulikuwa tunatembea na fimbo na ikitokea hata mtu mmoja kakohoa basi darasa zima linapigwa fimbo mbili mbili.

Hali hiyo ilifanya wanafunzi waogope utawala wangu na niliongoza kwa muhula mmoja tu baada ya hapo Mimi na Juma tukawa wanafunzi wa kawaida na kiongozi mwingine akatawala.

Sasa kwa mfano huu bado nilipofika chuoni wakajidanganya kunipa uongozi. Hili sitalisemea naweza kukoswa na teuzi za Mh.
 
Hahaa enzi hzo tukitoka mstarini tunakimbizana kiwahi dawati sasa mm rafk zangu kama walikua washanijuloa nikiwahi nafasi wnanitkenya hadi nawaachia nachukua kipande cha tofali naenda kukaa mbele huko
Mimi nilikuwa nakaa kwenye dawati kupitia mgongo wa rafiki yangu alikuwa mbabe sana.
 
teh

Hata mimi mkuu hiyo ilkua show off tu mzee

Anyway in reality mkuu mi nlkua mkimya sana aisee no talks

Few friends nmerushwa madarasa mawili la 2 to la 4

Pia la sita to form one

Mzee nlkua mkimya sana aisee
Yaani wewe una tabia sawa na zangu, mimi ni mpiga kelele hapa JF ila kihalisia ukiniona unaweza kudhani mimi ni mhamiaji haramu.
 
Ilikuwa darasa la pili nakumbuka, nilichaguliwa kuwa Monitor. Kumbe darasa lile halikujua kuwa limefanya kosa kubwa sana kunipa madaraka.

Nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Juma alikuwa mkubwa kuliko mwanafunzi yeyote mle darasani, na ndiye alikuwa Mayweather wa darasa. Hivyo nikamteua awe kama msaidizi wangu kutokana na ubabe wake.

Shule yetu ilikuwa na kelele kama kundi la nzige ila darasa langu muda wote lilikuwa kimya sana kama vile hakuna mwanafunzi. Nilikuwa sina utaratibu wa kuandika majina ya wapiga kelele, mimi na Juma tulikuwa tunatembea na fimbo na ikitokea hata mtu mmoja kakohoa basi darasa zima linapigwa fimbo mbili mbili.

Hali hiyo ilifanya wanafunzi waogope utawala wangu na niliongoza kwa muhula mmoja tu baada ya hapo Mimi na Juma tukawa wanafunzi wa kawaida na kiongozi mwingine akatawala.

Sasa kwa mfano huu bado nilipofika chuoni wakajidanganya kunipa uongozi. Hili sitalisemea naweza kukoswa na teuzi za Mh.
Hahahaaa u CR unaboa maana unaweza kwenda kumtafuta lecture yupo hukooooooo.
 
Hahahaaa u CR unaboa maana unaweza kwenda kumtafuta lecture yupo hukooooooo.
[emoji28] [emoji28] Yaani maisha yale yalikuwa ni ya furaha tupu, wakati huo hakuna mwanafunzi anaewaza kuhusu kesho yake, wote tulikuwa tunatazama siku iliyopo tu.
 
Teh ... [emoji28][emoji28]

Mkuu mimi hadi nipokee simu yako.aisee ujue wewe ni so special

Yaani dah hii tabia sijui itakwisha lini
Hii tabia ni mbaya sana nimeona athari zake, sitaki mwanangu aje kuwa na tabia ya ukimya kama wangu. Nina rafiki wachache sana na hata hao marafiki siwapi muda, napenda kuwa mwenyewe na sipendi kupigiwa simu za kukutana pasipo kuwa na kitu cha muhimu.

Siwasiliani na watu, siyo ndugu wala wafanyakazi wenzangu yaani kifupi napenda kukaa pekee yangu. Kati ya mwaka 2015 hadi 2016 nilikaa Arusha kwa mama mmoja hivi nikiwa kama mpangaji wake tangu naingia hadi natoka hakuwa kujua hata naitwa nani ndani ya kipindi cha mwaka mmoja hadi pale mtoto wake mdogo alipoamua kuniita John hadi leo hii nikienda kuwasalimia wananiita John na nimekubali lile jina.

Nilipata kuishi kwa baba mmoja pia kama mpangaji mwaka ulivyoisha nikaondoka, siku ile namkabidhi funguo ndipo yule baba anaomba hata tujuane. Sema kweli siwezi kubadilika kitabia na nikaja kuwa mtu wa kushobokea watu, nimejaribu nimeshindwa.

Mara nyingi nampenda kutumia JF kwa sababu nakuwa huru kujipa furaha.

Kuna mada iliwahi kuja humu inazungumzia Extrovert na Introvert hebu itafute uisome.
 
Back
Top Bottom