Network ilikuwa hakuna kijijini kwetu, ilikuwa lazima upande mlimani,siku hiyo yametangazwa kulikuwa na mvua nyingi yenye radi sana, lakini kwa hamu ya kupata siku hiyo hiyo,nilimfuata Hakimu mmoja hivi (R.I.P SIKAZWE) alikuwa rafiki yangu na alipenda mafanikio yangu na alinisupport,akanipa Simu na mvua nikaanza safari ya kupanda mlima huku simu ikiwa kwenye mfuko wa rambo,nilipofika juu mvua ilikuwa imepungua ila radi nyingi,nikampigia kaka aliyekuwa DSM kwa wakati ule hatukuelewana na vocha ikaisha na sikujua kuandika meseji kwenye ile Motorola jeneza,bahati nzuri kaka akapiga nikasikia tu umefaulu,nikaanza kushuka Kwa furaha bila kuelewa nimepata division ipi 😀😀😀 baadaye kesho yake Mama akaja na info zote.........safari ya Malangali high school ikawa imefika😀