TBT: Ulipokea matokeo yako ya Form Four ukiwa wapi, na ilikuwaje?

TBT: Ulipokea matokeo yako ya Form Four ukiwa wapi, na ilikuwaje?

2008 nilikuwa mgonjwa sana sijiwezi
1994 nilikuwa mgonjwa kwelikweli, nipo nimelazwa kabisa nakula zangu sindano. ilikuwa ngumu sana enzi hizo kupata matokeo, hadi yabandikwe shuleni au kama upo mbali na shule yako,ilikuwa ni mpaka ubahatike kupata kitabu cha matokeo ilikuwa azania nashukuru nilitusua nikaenda tambaza.
 
1994 nilikuwa mgonjwa kwelikweli, nipo nimelazwa kabisa nakula zangu sindano. ilikuwa ngumu sana enzi hizo kupata matokeo
hadi yabandikwe shuleni au kama upo mbali na shule yako,ilikuwa ni mpaka ubahatike kupata kitabu cha matokeo
ilikuwa azania
nashukuru nilitusua nikaenda tambaza
Azaboys kumbe tupo wengi πŸ‘πŸ™Œ
 
H
1994 nilikuwa mgonjwa kwelikweli, nipo nimelazwa kabisa nakula zangu sindano. ilikuwa ngumu sana enzi hizo kupata matokeo
hadi yabandikwe shuleni au kama upo mbali na shule yako,ilikuwa ni mpaka ubahatike kupata kitabu cha matokeo
ilikuwa azania
nashukuru nilitusua nikaenda tambaza
Hongera sana
 
Mi nikisema matokeo yangu hapa afu nikasema yalivyotoka nikalia asimilia 99 hapa hawawezi kuamini, yaani nililia kisa watu wawili walinipita. Demu wangu mmoja na mshkaji wangu nilikua nasoma nae.

Jamaa alijitapa sana maana nilikua nampigaga pindi aisee necta akaninyoosha. Hapo acsee tulienda nae shule Moja Nilimnyoosha.

Ila sasa tunafanya kazi ambazo hata hazihusiani na tulichosomea chuo, hii ndo bongo bana. Unakua kipanga darasani Kuna majamaa ulikua unayaona majinga kwenye maisha yame make kinoma
 
Mimi ilikuwa mwaka 20__.
Nilikuwa zangu nyumbani nimetulia naperuzi tu.

Ila nilifurahi sana
Yako yalikukutia wapi, na ilikuwaje?
Nlikua nyumbani ilikua mida ya jioni nikapigiwa simu na mama yangu mdogo matokeo yametoka aiseee tumbo lilivuruga sababu ya mchecheto hapohapo nikaenda kuendesha Baadae nikaenda internet cafe
 
Nilikuwa home, Wala sikuwa na presha,maana nilishagawa namba yakitoka waniangalie,

NB;kuna ka kauli haka hapa ka kujifariji,(KUFELI MTIHANI SI KUFELI MAISHA.)
 
Nilikuwa home, Wala sikuwa na presha,maana nilishagawa namba yakitoka waniangalie,

NB;kuna ka kauli haka hapa ka kujifariji,(KUFELI MTIHANI SI KUFELI MAISHA.)
Kuna jamaa nilisoma o level alikua mhindi, alipata div 4.. hakuendelea na shule akapewa mtaji akafungua duka lake mjini.... Nikiwa advance likizo nikawa naenda dukani kwake tunapiga story jamaa namuonea huruma naona kama maisha kafeli sana yani... Hapo najiona mjanja kukariri physics, ma organic chemistry huko na calculus inapanda najiona maisha nimeyapatia

Jamaa sa ivi yupo level zingine kabisa siwezi hata kumgusa, ndo unaambiwa kufeli mtihani sio kufeli maisha
 
Back
Top Bottom