Mufti kuku The Infinity
JF-Expert Member
- Sep 21, 2019
- 6,053
- 10,032
Bata liliendelea, au liliishia hapo?Nilikuwa Kidimbwi nakula Bata.
KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Aisee2008 nilikuwa mgonjwa sana sijiwezi
πππIlinikuta nikiwa home nakumbuka faza alikua safarini basi akaniahidi zawadi maana sikumuangusha wazazi walifurahi sana..... Mpaka faza anarudi nilishapigwa na mizawadi kibao kila anaeulizia tokeo anatuma kazawadi kwenye bus nakumbuka hata nilipokwenda adv.... Nilisindikizwa na kundi la ndugu mpka wakawa wananiita mtot wa mama maana ukigeuka shangazi mara bibi huku Mama wakubwa yaani kalikua kamzozo ka kusindikiza mtoto wao anakwenda shule tena
Bata liliendelea kama kawa.Bata liliendelea, au liliishia hapo?
Sio KaziKweliKweli/Its not JobTrueTrue
Nakubali πBata liliendelea kama kawa.
KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Funguka ππΉDaah nimekumbuka kitu kikubwa sana hapa.
ππNetwork ilikuwa hakuna kijijini kwetu, ilikuwa lazima upande mlimani,siku hiyo yametangazwa kulikuwa na mvua nyingi yenye radi sana, lakini kwa hamu ya kupata siku hiyo hiyo,nilimfuata Hakimu mmoja hivi (R.I.P SIKAZWE) alikuwa rafiki yangu na alipenda mafanikio yangu na alinisupport,akanipa Simu na mvua nikaanza safari ya kupanda mlima huku simu ikiwa kwenye mfuko wa rambo,nilipofika juu mvua ilikuwa imepungua ila radi nyingi,nikampigia kaka aliyekuwa DSM kwa wakati ule hatukuelewana na vocha ikaisha na sikujua kuandika meseji kwenye ile Motorola jeneza,bahati nzuri kaka akapiga nikasikia tu umefaulu,nikaanza kushuka Kwa furaha bila kuelewa nimepata division ipi πππ baadaye kesho yake Mama akaja na info zote.........safari ya Malangali high school ikawa imefikaπ
Hii ilikuwa 2012, tupo mazoezini kama kawa na washikaji ile tunamsikiliza mwalimu kabla ya kuondoka kuna njemba ikaropoka matokeo yametoka. Aisee kuna jamaa alikuwa anajiamini kupitiliza tukakimbia internet cafe karibu na pale uwanjani.Funguka ππΉ
Maghayo alipofaulu darasa la 7 kijiji kikadhani ni freemason maana yeye ni Mongolian Savage wa kwanza kufaulu la 7 na kupenda elimu ,sasa akaamua akimbie mbele kuhofia usalama waka wa kukiuka taratibu za kijiji kuwa hakuna kufaulu na kusoma ninmwendo wa kuwinda maporini...
Duh, sio mchezoHii ilikuwa 2012, tupo mazoezini kama kawa na washikaji ile tunamsikiliza mwalimu kabla ya kuondoka kuna njemba ikaropoka matokeo yametoka. Aisee kuna jamaa alikuwa anajiamini kupitiliza tukakimbia internet cafe karibu na pale uwanjani.
Tulikuwa kundi la watu kama nane hivi, jamaa akawahi kwenye kompyuta moja ilikuwa na mdada mrembo sana chap akamtajia namba ya shule na namba yake, kucheki ngoma ni IV points 27 jamaa alizimia. Zoezi la sisi kuangalia lilishia pale na kuanza kutoa huduma ya kwanza.