CCM wanakimbia majukwaa ya kampeni kujibu hoja za ushindani, sasa wanatumia "preemptive approach" ili kuzuia wapiga kura wasifunguliwe akili zao kuhusu uchakavu wa sera za CCM. Wanajaribu kuzuia mafuriko kwa mikono kitu ambacho kamwe hakiwezekani.
Kwa kadiri wanavyofanya hila kwa vyama vya upinzani, hasa kwa Rais Mtarajiwa Tundu Lissu, ndivyo ambavyo watu wengi wanajenga shahuku ya kutaka kuzisikia nondo zake. Huyu Tundu ni mfano hai kabisa wa madini ya thamani kubwa kutokana na ubora wa chama chake na uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja awapo jukwaani.
Ukweli utabaki kuwa, uwepo wa mgombea wa CCM kisera na kihoja, ni sawa tu uwepo wa wingi wa madini ya chumvi ambayo bei yake sokoni ni ya chini mno, lkn mgombea wa CDM ni sawa na madini ya dhahabu, ambapo mchakato wake wa kuyapata na uchache wake huyapa thamani kubwa sana yawapo sokoni. Wana CCM ikumbukeni sana hii namba, yaani ushindi wa Lissu wa 65% kwa yenu ya 30%
Hesabu siku zote haziongopi. Baada ya kufanya kampeni kwa kilugha, sasa itawapasa kuva kaniki ili muonekane kuwa na nyinyi ni wanyonge kutokana na sera mnazozihubiri kwa watu wasiokuwa na uelewa wa kutosha wa mambo ya kisiasa.