Uchaguzi 2020 TCAA yawajibu CHADEMA, yasikitishwa na upotoshaji wao

Uchaguzi 2020 TCAA yawajibu CHADEMA, yasikitishwa na upotoshaji wao

.... lakini hiyo article hapo juu imeonyesha baadhi ya Nchi duniani kutokana na upungufu wa pilots katika Nchi zao wameongeza umri huo hadi miaka 67 na Nchi nyingine ziko mbioni kuongeza umri huo.

Sasa wewe kichwa maji unajadili mapendekezo ya sheria au mabadiliko ya sheria au una jadili swala lililo mezani? Sheria yetu hairuhusu na hatujafikia kwenye huo upungufu
 
Kichwa maji soma vizuri waliomba kibali cha msamaha wa kutumia rubani wa zaidi ya umri ulio wekwa kisheria na wamekataliwa kwakuwa ni kinyume cha sheria kutumia rubani mwenye umri wa zaidi ya 65 years!

Mnapaswa kuwaomba radhi Mamlaka ya anga muache kuropoka ropoka

Hawawezi kuomba radhi kwani hawana maadili yenye kuwakumbusha umuhimu wa kufanya hivyo.

Wanajenga siasa za kitoto za kudeka na anayedeka siku zote anajiona ni mkamilifu.
 
Maandiko yanasema ficha upumbavu wako usiifiche hekima yako, hiyo sheria ipo na inatumika miaka yote kwa nini hamkuhoji? nani kawadanganya kwamba nyie ni special sana? sio nyie kila uchao mnalalamikia uvunjwaji wa sheria na vyombo, taasisi au watu kadhaa? wakifuata na kusimamia sheria pia ni kosa? hamjui hata mnataka nini, jiandaeni na 5% ya kura zote 28 October.

JPM anachana mikoa miwili kwa siku na anahutubia karibu kila kata, acheni uvivu, tembeeni barabarani muone kero za wananchi ili msijeropoka tena kwamba Magufuli anajenga miundombinu tu.

Hizo taasisi hazioni matumizi ya kisukuma kwenye kampeni?
 
CCM wanakimbia majukwaa ya kampeni kujibu hoja za ushindani, sasa wanatumia "preemptive approach" ili kuzuia wapiga kura wasifunguliwe akili zao kuhusu uchakavu wa sera za CCM. Wanajaribu kuzuia mafuriko kwa mikono kitu ambacho kamwe hakiwezekani.

Kwa kadiri wanavyofanya hila kwa vyama vya upinzani, hasa kwa Rais Mtarajiwa Tundu Lissu, ndivyo ambavyo watu wengi wanajenga shahuku ya kutaka kuzisikia nondo zake. Huyu Tundu ni mfano hai kabisa wa madini ya thamani kubwa kutokana na ubora wa chama chake na uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja awapo jukwaani.

Ukweli utabaki kuwa, uwepo wa mgombea wa CCM kisera na kihoja, ni sawa tu uwepo wa wingi wa madini ya chumvi ambayo bei yake sokoni ni ya chini mno, lkn mgombea wa CDM ni sawa na madini ya dhahabu, ambapo mchakato wake wa kuyapata na uchache wake huyapa thamani kubwa sana yawapo sokoni. Wana CCM ikumbukeni sana hii namba, yaani ushindi wa Lissu wa 65% kwa yenu ya 30%

Hesabu siku zote haziongopi. Baada ya kufanya kampeni kwa kilugha, sasa itawapasa kuva kaniki ili muonekane kuwa na nyinyi ni wanyonge kutokana na sera mnazozihubiri kwa watu wasiokuwa na uelewa wa kutosha wa mambo ya kisiasa.

Wewe kichwa maji umeshindwa kusoma hata hiyo habari hapo juu sheria hairuhusu kutumia rubani mwenye umri wa zaidi ya miaka 65 ! Mlitaka mkaanguke ili msingizie CCM nyie wenye midomo mirefu
 
Je, TCAA walifanya tathmini ipi ya huyo rubani wa zaidi ya miaka 65 kwamba atahatarisha usalama wa wasafiri?

Mara ya mwisho huyo rubani kurusha helicopter akiwa above 65 YO ilikuwa lini?
Sharia haitaki sio tathimini unatathimini nini wakati sheria hairuhusu?
 
Mbona barua imeweka wazi kuwa rubani aliyekataliwa kibali ana zaidi ya 65!

Uko sahihi sana, je mara ya mwisho huyo rubani kurusha hiyo helikopta ni alipokuwa na miaka 65, na hajawahi kurusha tena?
 
Nimewaelewa Mamlaka ya anga . Sasa huyo rubani mzee kibali huwa anapata wapi au nyie hamuhusiki na vibali vya marubani ? Hamjui kuwa hao watoa huduma za helcopter wana rubani mzee ?

Halafu namshauri tu TL atumie magari tu maana bado tunachanga michango ya kampeni huku kitaa ameanza kukodi helcopter it is not fair 😂😂😂😂😂😂😂
 
Kisukuma ni mojawapo ya lugha 120 za Tanzania. Ina haki kutumika.

Ingawa naona kama vile umeingiza mada katika uzi tofauti kabisa.

Niliyemqoute kasema taasisi za nchi hii zinasimamia sheria, ndio nikatao mfano wa kuongea kisukuma. Hakuna anayekataa kisukuma kutumika, ila sheria za uchaguzi ni marufuku kutumia kilugha nje ya kiswahili.
 
Mbona barua imeweka wazi kuwa rubani aliyekataliwa kibali ana zaidi ya 65!
Kiinglish wanafahamu wakina matonya tu, Wacha chichi tiliesomea ngumbaru tunyamaze. Khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Je, TCAA walifanya tathmini ipi ya huyo rubani wa zaidi ya miaka 65 kwamba atahatarisha usalama wa wasafiri?

Mara ya mwisho huyo rubani kurusha helicopter akiwa above 65 YO ilikuwa lini?
unaelewa lakini au ni ubishi tu, mnataka wabatilishe kanuni na taratibu zilizowekwa? madhara yakitokea mtarudi hapa na lugha nyingine
 
Back
Top Bottom