Kinyau
JF-Expert Member
- Nov 24, 2006
- 921
- 726
Nina line voda na airtel kikweli voda wanajitahidi kuaa transparent ila Airtel huu uongo wa kusema umetumia 90% ya bando lako ni utoto. Kwanini wasitumie kipimo cha mb kadhaa.Wananchi tumekuwa tukilalamika sana kuhusiana na wizi unaofanywa na mitandano ya simu. Mmeziba masikio yenu kwa Vigondo. Hamsikii.Na macho yenu mmeyavalisha miwani ya Mbao. Hamuoni.
Airtel kwanza wana utaratibu ambao mimi nmeshindwa uelewa.napotaka kuangalia data bundle iliyobaki sipewi majibu. Napewa majibu ya salio la kawaida lililobaki. Data sipewi majibu yake. Lengo lao ni kuwa nisiweze fuatilia kiasi cha bundle kinachotumika.
Pili leo nmeshangaa simu ikiwa haipo online sijawasha data naletewa ujumbe nimetumia asilimia 90 ya GB 1 ambayo nliweka jana mchana na sijadownload chochote cha kufika hata MB 200. Huu ni wizi. TCRA sijajua kwa nini mnawaacha hawa wenye mitandao watuibie.
"Umetumia takribani 90% ya MB 1024 yako. Salio ya intaneti yako ni 87 MB. Bonyeza My Airtel - Apps on Google Play kupakua Airtel App kununua Bando mpya."
View attachment 1601814
Airtel wana mambo mengi wameyaficha nyumba ya gharama halisi na ndipo nilipoamua ntatumia voda kwa data kwa kuwa wana customer care kidogooo nafuu na uwazi ila Airtel wajirekebishe