TCRA inachunguza mabadiliko ya mabando ya simu yaliyofanyika kimyakimya

"endapo mtumiaji amenunua kifurushi halafu akapata tofauti na alicholipia, awasiliane nasi"

Kesi yote imeishia hapa, lao moja.
Yaani mtandao wa simu utakuwa na kosa endapo tu kwenye menu watakuonesha kwa TZS 500 unapata MB 500, halafu ukanunua ukapata mb 120.

Ila kama kwenye menu wamekuonesha kwa tzs 500 unapata MB 120 na ukanunua ukapata kweli hizo MB 120, huo ni mzigo wako na hakuna kesi.
 
Wewe bado upo gizani, wizi mwingine mimi sijawahi kumaliza bando langu mpaka zero, zikibaki mb 50 tu sunema zinaanza mwenyewe hata uwe kauzu utarecharge tu, na ukikomaa zikibaki mb 30 utaishia Facebook na picha haziload, JF ndio sahau kabisa haifungui, huu ni uharamia.
 
Inafuatilia for how long ina maana wao hawatumii hizo huduma? Au hawana mifumo inayosoma kinachoendelea huko?
 
Ngoja niwakumbushe mwaka Jana kabla ya JPM kutuacha ilikuwa hivi

1000gb1
2000gb3
3000gb4
5000gb7
10000gb15
Halafu hiyo ilikuwa ni tigo na halotel
Tigo,, Halotel,,Airtel,walikuwa na kifurush Cha usiku 1500 gb15
Lakini baada ya mazishi mambo yakadilika hapo hapo baada ya kupata Actor wa sinema hii nchi Bora iuzwe tu
 
Ngoja niwakumbushe mwaka Jana kabla ya JPM kutuacha ilikuwa hivi

1000gb1
2000gb3
3000gb4
5000gb7
10000gb15
Halafu hiyo ilikuwa ni tigo na halotel
Tigo,, Halotel,,Airtel,walikuwa na kifurush Cha usiku 1500 gb15
Lakini baada ya mazishi mambo yakadilika hapo hapo baada ya kupata Actor wa sinema hii nchi Bora iuzwe tu
 
Sasa hivi hapa nimenunua kifulushi Cha 2000 ilikuwa tunapata gb 1.500 now imekuwa gb 1.300
 
Kwani unafikiri hawajui?

Hii nchi ina uzembe sana
 
Very unprofessional regulatory action kutoka TCRA! Kwahiyo TCRA haina mfumo uliounganishwa na kampuni za simu kutrace bills za matumizi anazochajiwa mteja hata wasubiri sms za wateja? Infact, hili si suala la kuchunguzwa, huenda kuchunguza ni plan ya kufunika kombe.
 
Huwa nanunua kifurushi cha 20,000 kwa Gb 15 sasa imekuwa 13. Hali mbaya
 
Awasiliane nanyi kwa namba isiyojulikana wakati mnao uwezo wa kuona mauzo yaliyofanyika! Huo ni usanii wa kuwafanya walalamikaji ni mabwege.
 
Uku mtaani chapati ya shilingi elfu 1 ilikuwa kubwa sasa hivi imepunguzwa ukubwa imekuwa nyepesi kwa bei hiyo hiyo ya elfu 1
 
Vodacom 50,000 ilikua 50GB, ikashushwa kua 37GB na leo ni 32GB.

Hii inatokea ndani ya muda mfupi wa serikali ya Royal Tour.

Hadi kufikia 2025 tutakua tumeipata fresh.
Hao voda ni washenzi sana ....hizo zitqshuka mpka 10gb tunakoenda...maana mwanzo zilikuwa 50gb
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…