TCRA: Kipindi cha Shule ya Uongozi cha Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji

TV ya Maria Sarungi waliifungia hawa hawa akina Polepole

Sasa leo uonevu ule ule umemkuta

Atataka tumtetee

Shwahini wahedi kabisa
Shwaini ... Nimefurahi kusikia neno Hilo. Wewe itakuwa Mhaya, kinatumika Sana uhayani
 
Polepole anavuna matunda ya kazi yake. Ikiwezekana wasishie kumfungia tu bali wamfunge na yeye mwenyewe.

Sheria zote ovyo za awamu ya 5, Polepole alihusika. Uzuri wa sheria hizi, kwanza aufaidi Polepole, aliyezitolea jasho.
Sheria sio msaafu.

Ndo kwanza moto unawashwa.
 
Bashiru kanyamaza na Wala hawatampata. Ameamua kuwaachia CCM Yao na siasa in toto
Bashiru at least anajua wazi, alibambukwa cheo asichostahili.

Vile vile anajua fika kuwa hakuwa mwana CCM na uraia wake bado una mashaka.
 
, Habbi Gunze, NathanI ulipewa kazi hii kwa kujuwana, na sio kwa ujuzi. Unatumia madaraka yako vibaya. Hapa PolePole kafanya kosa gani? Munamwambia KAA KIMYA asiwaelemishe WATANZANIA, MUNAOGOPA NINI? Munataka kuongoza wajinga? PolePole ana haki kama mtanzania kuelimisha watanzania wengine. Hii serikali imekuwa ya uonevu badala kuwa serikali sikivu. Jamani oneni haya kwa kuonyesha uhuni wenu wazi wazi wa uonevu na kuwafanya Watanzania wengine kama wakimbizi.
 
Alivyokuwa anatunga hizi sheria kandamizi alifikiri kuwa anakomoa upinzani peke yake🐒🐒🐒
View attachment 2047400
Hawa wanawaongoza Watanzania kama ng’ombe. Hawataki waelimishwe. Wahuni hawa wamejifanya Tanzania kama mali yawo binafsi. PolePole hana kosa. Kuelimisha watanzania na kutetea haki zawo sio makosa. Serikali oneni aibu, hamukuuziwa nchi, bali mumeajiliwa na Watanzania kuwafanyisha kazi sio kuwaongoza kama ng’ombe kwenye zizi. Tusikubali uhuni huu. Lazima TUKATAE kwa pamoja
 
Kosa la Polepole ni kuunga mkono sheria hizi kandamizi zilipokuwa zinatungwa akifikiri kuwa yeye kwa kuwa alikuwa upande wa dikteta basi atakuwa yupo salama.
 
Kosa la Polepole ni kuunga mkono sheria hizi kandamizi zilipokuwa zinatungwa akifikiri kuwa yeye kwa kuwa alikuwa upande wa dikteta basi atakuwa yupo salama.
Wengi wao huwa wapo hivyo, wakiwa ndani wanafikiri kwa kutumia TUMBO ila wakitoka nje ndio wanaanza kufikiri kwa kutumia AKILI, " WHAT GOES AROUND COMES AROUND " sijui ni kwanini bandugu huwa banasahau !!!
 
Na kwakuwa sasa hana pesa,hataweza kukodi ofisi,anunue vifaa na kuajiri waandishi wa habari

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…