TCRA kulazimisha laini moja tu kwa kila mtandao kwa Raia si sahihi!

Kwa hiyo kuna zoezi kingine la kutufungia sie wenye laina zaidi maoja kwa mtandao mmoja.

Hii serikali kwa nini imewekeza sana kwenye kudhibiti mawasiliano ya wananchi wake.
Imeelezwa wazi,mwisho tarehe 30 June,baada ya Happ usigonje ufungiwe, deactivate mwenyewe au andaa faini
 
Kanuni mpya za usajiri wa *Laini za Simu* za mwaka 2020 zimetangazwa kwenye Gazetti la Serikali la tarehe 7 February, 2020 kama Tangazo la *Serikali No. 112 la 2020*. Jina fupi (short title) la Kanuni hizo ni *the Electronic and Postal Communications (SIM Card Registration) Regulations, 2020*.

Baadhi ya maswala kadhaa ambayo yamejitokeza katika Kanuni za Usajiri wa Laini za Simu hizi mpya ni yafuatayo;

(1) Kwa sasa ni lazima kisheria kusajiri Laini ya Simu kwa alama za vidole.

(2) Usajiri wa Laini ya Simu kwa alama za vidole utafanywa kwa kutumia Kitambulisho cha Taifa kilichotolewa na NIDA au Namba ya Kitambulisho cha Taifa.

(3) Ni marufuku kwa mtu (binadamu) kusajiri *Laini ya Simu zaidi ya moja* (1) kwenye mtandao mmoja wa simu kwa ajiri ya matumizi ya kuwasiliana kwa njia meseaji, kuongea na data. Kwa mfano, ni marufuku kuwa na laini mbili au zaidi za Vodacom, unapaswa kuwa na laini moja tu ya vodacom.

(4) Mtu anaruhusiwa kumiliki laini za simu ambazo hazizidi *4* kwa matumizi ya vifaa au mashini za mawasiliano ya kieletroniki. Kwa mfano, kutumia laini ya simu kwenye modemu.

(5) Kampuni (mtu kisheria) inaruhusiwa kumiliki laini za simu ambazo hazizidi *30* kwa ajiri ya matumizi ya kuwasiliana kwa njia meseaji, kuongea na data.

(6) Kampuni (mtu kisheria) inaruhusiwa kumiliki laini za simu ambazo hazizidi *50* kwa matumizi ya vifaa au mashini za mawasiliano ya kieletroniki.

(7) Mtu ambaye anamiliki laini za simu mbili au zaidi za mtandao mmoja wa simu amepewa muda mpaka tarehe *30 June, 2020* kuchagua laini moja tu atakayotumia.

(8) Mtandao wa Simu unawajibika kuzima laini ya simu ambayo haijasajiriwa kwa njia ya alama za vidole.

(9) Kila laini ya simu lazima iwe na *PIN* ambayo lazima iwekwe kwenye simu au kifaa cha kieletroniki kila wakati simu au inapowashwa au inapobadilishwa.

(10) Laini ya Simu isipotumika kwa siku 90 mfululizo lazima ifungwe.

(11) Taarifa yoyote iliyowasilishwa kwenye mtandao wa simu ikibadilika lazima mmiliki wa laini ya simu atoe taarifa ndani ya siku 14 zikiesabika tokea siku ambayo mabadiliko hayo yametokea.

(12) Ukitokea wizi au upotevu wa laini ya simu lazima mmiliki wa laini ya simu atoe taarifa police.

(13) Ili mtu apewa laini mpya kutokana na upotevu au wizi lazima apeleke kwenye mtandao wa simu Loss Report au taarifa ya uchunguzi wa awali kutoka polisi.

(14) Mtu ambaye atakiuka masharti yoyote ya Kanuni za Usajiri wa Laini za Simu, 2020 atakuwa ametenda kosa la jinai na adhabu zake ni kifungo cha kuanzia mwaka 1 mpaka miaka 10 au fine kati ya Tsh 300, 000 mpaka Tshs 30 Million kulinga na kosa husika au vyote kwa pamoja kifungo na faini.
 
Hilo halitawezekana milele, CCM tuko makini sana, usihofu
 
mimi niko na router nahitaji line ya voda, pia kwenye simu natumia line ya voda means nitakuwa nimesajili line 2.

kwa mujibu wa hii sheria mpya mimi tayari nimevunja sheria.

Nchi ngumu sana hii.
 
Hizi tabia za kudhibiti binadamu sio endelevu. Haya yote ya kijinga yataondolewa siku wanasepa
 
Yaani mie hapo nimeingiza na moderm zangu 4 za makampuni yote,
 
Hii ni hatari kwa ustawi wa nchi na raia
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo usajili wa alama za vidole haujakidhi matamania yao ya kudhibiti mawasiliano siyo.
 
Wote tunajiuliza hilo. Cha ajabu techjology inavyo kua , line za sim zitakuaja kuachwa na tutatumia simu ambazo hazina laini.

Huwezi shindana na technology
Kwa hiyo usajili wa alama za vidole haujakidhi matamania yao ya kudhibiti mawasiliano siyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo na wewe ni GT?

Je kama una modem na unataka utumie same provuder inabidi ufanyeje? Tumia ubongo zaidi kutafakali zaidi!
 
Acheni kupotosha watu kwa taarifa zisizo sahihi Kisha mnamsingizia ccm! We vyovyote utakavyoniona ni
Kwahiyo na wewe ni GT?

Je kama una modem na unataka utumie same provuder inabidi ufanyeje? Tumia ubongo zaidi kutafakali zaidi!
Mkuu Mimi ni kenge wewe je..?
 
Acheni kupotosha watu kwa taarifa zisizo sahihi Kisha mnamsingizia ccm! We vyovyote utakavyoniona ni
Mkuu Mimi ni kenge wewe je..?
Nani kakuita wewe kenge? Mbona una Changanyikiwa,!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…