TCRA kulazimisha laini moja tu kwa kila mtandao kwa Raia si sahihi!

Sawa

Ila na wewe mkuu ujanielewa maana nilimjibu mtu ambaye analahumu TCRA kuhusu katazo la kutosajiri ndugu na jamaa kupitia kitambulisho chake cha NIDA.

Kusajiri laini kwa vidole ni kuhakiki kile ulichokifanya NIDA kama kipo sahihi na pia kuweka kumbukumbu sawa kwenye mitandao ya simu.

Ndio FRAUD itapungua na kuisha kabisa maana watu walikuwa wanasajiri kwa namba upya baada ya kufanya tukio la kihalifu.

Kwani sekta binafsi imezuiwa kufanya biashara nchini?

Ni uongo na upotoshwaji kuhusu kusajiri simcard moja mtandao mmoja,kwamba ni ruhusa kumiliki simcard mbili kwa mtandao mmoja ila zaidi ya mbili kwa mtandao mmoja unapaswa ujaze fomu maalumu ueleze sababu za kuhitaji kumiliki simcard zaidi ya mbili.
 
Hapo sawa.. na sheria inayo takiwa ni kutotuhusiwa kutumia laini ambayo haijasajiliwa kwa jina la muhusika
Sawa

Ila na wewe mkuu ujanielewa maana nilimjibu mtu ambaye analahumu TCRA kuhusu katazo la kutosajiri ndugu na jamaa kupitia kitambulisho chake cha NIDA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iwe kama China huwezi kuwa na laini 2 bila sababu.
Pia tupewe namba za simu zinazodumu milele, tusiweze ibadilisha kamwe hata UFE

Sent using Jamii Forums mobile app
China hawana utitiri wa kampuni za simu za mikononi wana kampuni mbili pekee, lakini kwa Tanzania kuna kampuni nyingi za Simu kuliko hata America na mataifa mengi Duniani na tunasikia sasa Azam anakuja na kampuni ingine ya simu, wakitaka Line moja wafute kampuni zote za simu wabakize moja tu
 
Mshauri mkuu wa mtukufu ni Daud Bashite na hana vyeti unategemea nini?
 
Wapunguze kampuni za Simu Voda wainunue Halotel na Airtel iwe kampuni moja na Tigo wazinunue zingine zote zilizosalia ikiwemo TTCL zibakie kampuni chache mbili tu hapo hakutakuwa na ujinga wa kuwazia juu ya utitiri wa Line za Simu
 
Kampuni za simu waungane kama ule umoja wa mabenk
 
Laini moja kwa kila mtandao mmoja kwa ajili ya data, simu na sms

Laini 4 kwa kila mtandao mmoja kwa ajili ya mawasiliano ya vifaa kwa vifaa.
 
Hivi kwa nini wanakunyang'anya namba kama hujaitumia kwa siku 90? Mtu ukipata kozi ya zaidi ya siku 90 basi line yako unapoteza? Wengi gharama za ku roam haziwezi. Hizi namba tunawapa wengi na ukiipoteza ni usumbufu mkubwa! Na kuna raia wanaishi nje na wanamiliki laini za simu kuwarahisishia mawasiliano wanapokuja kuwatembelea ndugu zao. Hawa nao wanatakiwa waombe line mpya kila wanapokuja?

Amandla........
 

tunashukuru tu Mungu hatuwezi kua na kiongozi kama wewe! we unadhan kila mtu akiruhusiwa afanye anachotaka hii dunia utaipenda? kuna mda mwingine inakubidi tu kama kiongozi ufanye maamuzi magumu despite utapata lawaama! huezi jua wameona nn kwenye kua na laini mbili na wameshuhudia nn na nn mpaka wameamua hivi, sasa you better respect that!
 

akili zingine bana! kuropoka tu, una uhakika na unachoongea au ni basi tu umepewa sehem ya kuongea
 
Kama ni kweli waache upuuzi wao .

Sent using Jamii Forums mobile app
 

its too much! kuna vitu vingine sasa i can even say ni dhambi, kumbuka kuna sheria inasema usimshuhudie mwenzako uongo! kitu hauko sure nacho like a grown up you wait for evidence sasa kila kitu magu, sjui nini kimeenda vibaya, mtu kaachana na mke wake magu! WTF, vitu vingine ebu muogopeni Mungu bana! ana mapungufu yake ndio lakini sio kwa kiasi iki mnacho potray,

to disapper aende wap? he still has more years ahead! ni vile tu ile ishuw ya kuongezewa mda aliikataa mapema lakini nlikua naunga mkono lile swala
 

privacy gan? there is nothing like privacy in this world, ata apa jamii forum you can still be traced vizuri sana with just a photo na ukapatikana vizuri sana
 
Sasa atawezaje kujua wameona au wameshuhudia nini bila wenye kufanya maamumizi kutoa sababu za kuyafanya?

Amandla....
 
Laini moja kwa kila mtandao mmoja kwa ajili ya data, simu na sms

Laini 4 kwa kila mtandao mmoja kwa ajili ya mawasiliano ya vifaa kwa vifaa.
Kama inakuja inakataa hivi!
 
Muda wa kampeni ukifika hili suala litafutwa ili watanzania waelezwe kuwa kuna watetezi wa wanyonge... Sasa ni free kusajili laini kadri unavyotaka....Tanzania nakupenda sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
C
Sote tutumie TTCL basi
 
Unaona usivyoelewa?
Nimeandika wapi kwamba "---kila mtu akiruhusiwa afanye anachotaka---"? Unashindwa kujjibu hoja unarukia yasiyokuwepo kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…