mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 88,759
- 123,368
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa wiki unatumia mapesa mengi kwa ajili ya intaneti tu! ili iweje?Aisee nimeipenda hii kanuni mkuu,Nani naichukua nadhani itanisaidia pia...[emoji106][emoji851]
Usajli wake upoje?Orange, MTN, Safaricom zote zinapiga kazi Tanzania, na tayari wengi wameanza kuzitumia
Mamlaka hiyo imesema kwamba hakuna laini ya simu itakayofungwa kabla ya tarehe hiyo.
Aidha, imesema wananchi wanatakiwa kwenda kusajili laini zao kwa kutumia vitambulisho vya uraia, na kuthibitisha usajili huo kabla ya muda uliowekwa kwa kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya kuzifunga.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Kaimu Meneja Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakanjala, alisema hadi sasa laini za simu milioni 20 zimesajiliwa.
“Hakuna mabadiliko yaliyotolewa ikifika Disemba 31, mwaka huu, laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa namba ya Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa) na kuthibitisha kwenye mifumo zitafungwa, tunawakata wananchi wasajili haraka,” alisema.
Aidha, alisema hakuna mtoa huduma atakayeruhusiwa kufunga au kukatisha mawasiliano ya mtumiaji yeyote kabla ya muda uliopangwa.
Jana kwenye baadhi ya makundi songezi (WhatsApp) baadhi ya watumiaji wa laini za simu walilalamika kukosa mawasiliano kwenye baadhi ya laini kwa kile kilichoelezwa kuwa zimezimwa kwa kuwa hawajasajili.
Mei mwaka jana, serikali ilitangaza ulazima wa usajili wa laini za simu, na kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka huu zitafungwa.
IPP Media