TCRA: Laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa namba za NIDA zitafungwa kufikia Desemba 31, 2019

TCRA: Laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa namba za NIDA zitafungwa kufikia Desemba 31, 2019

Suley2019,
tcra wangelipisha elfu tano kila laini serikali ingepata bil 100 katika zoezi hili, hizi pesa wangepewa ttcl wakanunua mtambo wa 5G tungepiga hatua nzuri ya maendeleo.
3G hakuna sehemu nyingi sana unawaza 5G?

Mitambo ya 5G utaishia kuifunga sehemu chache sana. Labda mkoa mmoja au miwili.

Ingekuwa rahisi hivyo, makampuni kama Vodacom wangeshafunga 5G nchi nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hawa jamaa wanayumba sana sjui wanakwama wapi hakuna msimamo maalum.

wakae chini wakokotoe idadi ya waliopata vitambulisho na idadi ya watumiaji wa simu.

AFRICA INA WASOMI WENGI WENYE ELIMU ILA WENYE AKILI WANAHESABIKA...
 
Usajili wa laini au vitambulisho vya uraia hili ni continuity exercises huwa haliishi kwenye nchi zote maana kila siku vizazi kuchepua na kukua,na huitaji huduma hii,na wengine hufariki vitambulisho vyao hufutwa,

N.B
This should be non dead line exercises.
N.b.hela jinsi ilivyo ngumu ni nani awezaye kaa foleni masaa 7 au 8 kuivumilia speed ndogo ya watumisho wa nida.
 
AFRICA INA WASOMI WENGI WENYE ELIMU ILA WENYE AKILI WANAHESABIKA...
Hapana, tuna wasomi wengi wenye vyeti lakini kati yao walioelimika ni wachache. Just imagine, hapa kwetu Kasulu wote tulioandikishwa, ukitoa watumishi wa uma, hatujapewa hata namba za NIDA, halafu unatishia kumfungia mtu laini.
 
Binafsi nilishajiapiza kwamba nitakuwa mtu wa mwisho mwisho kabisa kufuatilia kitambulisho cha NIDA yaani mpaka pale wahusika watakapoheshimu upotevu wa muda wangu.

Suala la kufungia line yangu wafanye kweli sio kutuletea mikwara ya kichaa cha dog.
 
awali kufunga line ambazo hazijasajiliwa ilikuwa 31 Mei 2019, ndipo rais akaongeza muda hadi 31 Disemba 2019 kwa sababu idadi ya waliopata vitambulisho vya utaifa ilikuwa ndogo sana.

hili zoezi linaweza sababisha mtu kutumbuliwa hasa NIDA sababu ya kasi ndogo ya kuandikisha wananchi.

Naunga mkono hoja ya kuondoa namba zisizo sajiliwa kikamilifu
 
Back
Top Bottom