TCRA: Laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa namba za NIDA zitafungwa kufikia Desemba 31, 2019

TCRA: Laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa namba za NIDA zitafungwa kufikia Desemba 31, 2019

Wageni pia wanatambuliwa na NIDA na wana ID za nida ambazo zinataja Nationality yao ni wapi ila pia kama una passport ambayo ndio International ID unaweza kusajili line nchi yoyote bila usumbufu
Kuhusu passport hilo kwa Tz naona bado litaleta usumbufu. Fikiria wenyeji tu tunavyohangaika na wakati wanayajua mpaka makaburi ya babu zetu ila wanatusumbua, itakuwaje kwa mgeni kusiwepo na usumbufu wowote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu wananchi,kwa mamlaka niliyopewa na Katiba chini ya ibara ya 13 section 17b ya mwaka 2018 sheria ya Mitandao ya kijamii..

na kwa kuzingatia ya kwamba mitandao ya kijamii ni kiwanda kidogo cha mkononi

natangaza kuongeza muda wa kusajili line kwa Siku 20 zaidi

watuu weeeweeeeeee.!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...
...
Aidha, alisema hakuna mtoa huduma atakayeruhusiwa kufunga au kukatisha mawasiliano ya mtumiaji yeyote kabla ya muda uliopangwa.
...
...
Huu ni UONGO,

Juzi watumiaji wa AIRTEL tumefungiwa mawasiliano kwa kile kilichoelezwa kua hatujasajiliwa.

Tumepata Usumbufu sana lakini TCRA wamekaa kimya.
 
Hivi hawa watendaji uwa wanatamka kana kwamba nchi yote ipo viganjani mwao wanasahau kwa wamepewa dhamana ya muda mfupi tu. Mkizima mna mkomoa nani? Ina maana kabla ya kuja hayo matumizi ya simu za mkononi hatukuwa tunaishi. Kwanza, mtapoteza mapato mengi na makampuni ya huduma za mwasiliano yatafilisika ghafla. Pili, nchi itabaki giza kama mlivyofanya kwenye huduma za TV na ving'amuzi. Tatu, wengi watapoteza imani na utendaji wenu na wasimamizi wenu. Pimeni hayo kwanza, kisha mzime.
 
Hili suala la TCRA na NIDA lunananitia kichefuchefu sana. Najua nitaipoteza namba yangu ya simu maana sidhani nitafanikiwa kufanya usajili kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu.
Itaniuma tu ni namba ya miaka 10+ nimekuwa nayo.
 
Wame nitumia sms zimebaki siku 12 kama vile nimewauliza zimebaki siku ngapi sijuwi hawana kazi!?

Mimi ni mteja mkubwa wa Mpesa..Sasa siku moja wakanipigia wakaniambia mbona hujasajili line yako kaka? nikawaambia line ni ya kwangu kama ikifungiwa ni mimi nitaathirika wakasema jitahidi usajili bwana. nikajibu sisajili kama ni kufunga wafunge tu.


Kujipendekeza tu.
 
Mimi uwa wananitumia SMS na wananiambia Namba yako ya NIDA ni xxxxxx nenda kasajiri.

Sijui wameipata wapi? Ila ni kwasababu nimesajiri laini 1 tu na nina laini kama 6.
 
Back
Top Bottom