TCRA: Laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa namba za NIDA zitafungwa kufikia Desemba 31, 2019

TCRA: Laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa namba za NIDA zitafungwa kufikia Desemba 31, 2019

Kwani kiongozi Mweshimiwa Lugola si alisema kwamba laini hazitafungwa.....this is tanzania.
...zaidi ya uijuavyo Mkuu! Raisi aliishasema, Waziri Kasema lakini ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole hazitakungwa...lakini anatokea atokako mkurugenzi na kutamba kadamnasini kuwa laini zitafungiwa tu tar 31...hata heshima mdogo tu kwa rais na waziri ???[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
USHAURI WANGU KWA WAHUSIKA WA MAWASILIANO NA VITAMBULISHO VYA TAIFA, HIVI HAMUWEZI BUNI AU KUWA NA MFUMO WA MOJA KWA MOJA ULIOUNGANISHWA NA HIZI TAASISI? MFANO MTU ANAPOENDA NIDA NA KUKUBALIWA FOMU ZAKE ZOTE MPAKA UHAMIAJI NA KUPIGA PICHA NA KUHAKIKI KITAMBULISHO CHAKE KWA SOFT COPY PALE PALE OFISI ZA NIDA, KWANINI NA TCRA MSIWE NA NAKALA HIZO MOJA KWA MOJA KWENYE MIFUMO YENU IKAPOA TAARIFA HIZO KUTOKA NIDA NA KUZIWASILISHA PIA MOJA KWA MOJA KWENYE MITANDAO YA SIMU IKAWA NJIA YA JUU KWA JUU MAMBO YA KAISHA. ALAFU WALE AMBAO FOMU ZAO ZILIKATALIWA NIDA NA UHAMIAJI KWA SABABU MAALUM NA WAKAPEWA MDA WA KUREKEBISHA NA WASIPO TUMIA MDA HUO VIZURI NDIO MKAPAMBANA NAO KWA KUFUNGIA LINE ZAO.

KWASABABU MDA HAUTOSHI NA BADO WALIOFANYA UTARATIBU WA KUJAZA NA KUKABIDHI FOMU ZAO NIDA TANGU MIEZI MINGI NYUMA NA MAPAKA SASA HAWANA KADI NA HATA NAMBA IMEKUWA CHANGAMOTO KUPATA, TAREHE 31 MNAWAFUNGIA KUNDI KAM HILI MAWASILIANO NA TAYARI WAMESHAMALIZANA NA UTARATIBU MZIMA WA NIDA HAMUONI KUWA MTALETA HASARA NYINGINE NA MALIMBIKIZO YA HATA KESI ZA WATU KUWAPOTEZEA PESA AU HUDUMA NYINGINE KWENYE MIFUMO YAO YA KIKAZI AU BIASHARA ILHALI WAKO SAHIHI. NINGEPENDA WAHUSIKA WA VITENGO HIVI AMBAO NI WANA JF WENZETU MTUFIKISHIE MAWAZO YETU HUMU.
 
Hakika nimeshtushwa na taarifa za TCRA kuwa ifikapo Desemba 31,2019 laini ambazo zitakuwa hazijasajiliwa kwa kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho zitafungiwa.TCRA mnapaswa mjue kuwa wananchi wanahangaika sana kupata vitambulisho au namba ya utambulisho.

Kitambulisho na namba ya utambulisho vinatolewa na NIDA kwa kushirikians na UHAMIAJI na RITA.Taasisi hizo zimeshindwa kuwapatia wananchi huduma hiyo kwa uharaka licha ya Wananchi kukesha kwenye Ofisi zao. Nilitegemea TCRA badala ya kukimbilia KUWAFUNGIA Wananchi simu zao hiyo tarehe ni vema wangeongeza nguvu NIDA RITA na UHAMIAJI ili Vitambulisho na namba ya Utambulisho viweze kupatikana ili wananchi wasajili laini zao, kuliko kukimbilia kuwafungia laini zao wakati ucheleweshaji unafanywa ni hizo Taasisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na tetesi zinazozuma kwa kasi saizi ni kwamba hawa jamaa wanafunga line kimya kimya yani hadai kufikia hiyo 31 basi watakua wamekamilisha zoezi lao

Jana kuna mtu kafungiwa line ya airtel kwasababu hiyo hiyo, kama kuna line yako ya airtel jana uliona inazingua na hukuwahi ku verifiy basi ujue ndio tayali nida washa pita nayo
 
Hivi kwa wageni ambao sio raia na hawana kitambulisho cha taifa na wanatumia simu utaratibu wao wa kusajili kwa alama za vidole unakuwaje...?
 
hii nchi bana, raisi anasema hivi tcra nao wanasema hivi ina maana wanampinga raisi sasa wasubiri rungu kama halijawadondokea
 
Naona airtel wameanza majaribio. Kweli fedha walizovuna zinawapa jeuri hata wakibaki na wateja 500.

Usajili wa line umekuwa mwepesi sana,pongezi kwa kampun zote za simu kwa kufanya juhudi za makusudi.

Tatizo ni upatikanaji wa vitambulisho vya NIDA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona Mimi toka Jana Airtel washanifungia kupiga Simu na leo Airtel Money wameshaniblock na tarehe 31 bado
 
Back
Top Bottom