TCRA: Laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri, Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama

TCRA: Laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri, Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama

Sa 7 mchana

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2018
Posts
5,214
Reaction score
10,276
Ndugu Mteja, laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri ambalo Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama.

I smell a fish juu ya laini hizi. Nitahakikisha sipotezi laini ilikuepuka kurenew laini nakuingia huku.

--
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema ifikapo Julai mosi, laini zote zitakazotolewa zitakuwa na neno la siri ambalo mteja atatakiwa kulibadilisha ili kutumia laini mpya yenye usalama.

Kwa mujibu wa ujumbe uliosambazwa jana kwenye simu za wateja mbalimbali ambao ulithibitishwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa TCRA, Semu Mwakyanjala, utaratibu huo utalinda wateja.

Alisema utaratibu huo una lengo la kuwalinda wananchi kwenye matumizi ya mawasiliano.

“Laini inapopotea ikachukuliwa na mwingine anaitumia vibaya lakini kwa kuwa na neno la siri, itamlinda mtumiaji na kuondokana na utumiaji usio salama,”alisema.

Mwakyanjala alisema utaratibu huo ni kwa mujibu wa sheria ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010 na kanuni zake za 2018.

“Tunataka matumizi bora ya mifumo ya simu si kwa ajili ya kuongea bali kama benki, hivyo usalama ni muhimu kwa ajili ya kuwalinda watumiaji, watu watumie simu kwa biashara na maendeleo kuliko kufanya uhalifu,”alisema.

Chanzo: IPP
 
Ndugu Mteja, laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri ambalo Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama.

I smell a fish juu ya laini hizi. Nitahakikisha sipotezi laini ilikuepoka kurenew laini nakuingia huku.
Sasa fish gani umem-smell, kilakitu sasa cha hii serikali mnakichukulia in negative way
 
Kwanini itoke TCRA na sio Mitandao ya Simu ; Utata upo hapo (Mitandao ya Simu inatoa Line kuongeza ufanisi wa biashara yao) TCRA motive yao ndio inayoleta ukakasi... Hususan nyakati hizi ambapo watu hatuaminiani
Hizi mamlaka kuna muda sielewi majukumu yake. Kwa hii issue kwamba unakuta line ina pin alaf unabadilisha unaweka yako au... kama ni hiv ina tofaut gan na ile unapewa namba ya siri ya M pesa au tigo pesa alaf unaweka yako.

Kwa upande mwingine kama hawaamin haya makampuni ya simu hiv🤔 Hii michezo nilishtukiaga kipind wanasisitiza issue za finger prints kwa kila kitu. Kusajili line finger print, Wanachuo na mikopo yao finger print, Polisi kule finger print, watoe tu sababu maan dah
 
Ndugu Mteja, laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri ambalo Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama.

I smell a fish juu ya laini hizi. Nitahakikisha sipotezi laini ilikuepuka kurenew laini nakuingia huku.
Kuna kaharufu fulani hivi ka kudukua taarifa za watu, hasa wakosoaji wa serikali
 
Back
Top Bottom