Nime kutana na PIN kwenye line mpya ya halotel. Inakera kichizi ila naelewa kwanini imewekwa.
Tukumbuke kuwa, vitu vinawekwa kulingana na mahitaji na malalamiko.
1. Tuli lalamika wapigaji mtandaoni, wale wa tuma kwenye namba hii.
- Wakaleta fingerprint ili watu hao waweze patikana. Ukiangalia wizi wa namna hiyo, umepungua sana.
2. Tuka lalamika inakuwaje mtu akiiba au kuokota line yangu na kuitumia kwa uhalifu? Maana fingerprint ita onyesha line ni yangu na nitakamatwa mimi.
- Wamekuja na kuweka PIN kwenye line. Ili hata kama ikiibiwa, akizima au ikizima asiweze itumia.
Sasa tuna lalamika kwanini wamefanya haya mambo. Tukumbuke malalamiko yetu wenyewe.