TCRA: Laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri, Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama

TCRA: Laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri, Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama

Una weza opt kuto kua na passoword
Ndugu Mteja, laini zote za simu zitakazotolewa kuanzia Julai 1 zitakuwa na Neno la siri ambalo Mteja atatakiwa kulibadili ili kutumia laini mpya yenye usalama.

I smell a fish juu ya laini hizi. Nitahakikisha sipotezi laini ilikuepuka kurenew laini nakuingia huku.
 
Hiyo code inakuwa linked na TCRA kwahiyo ukifanya kimeo chochote hawahangaiki kukupata
Wazee mnawaza kizamani, laini umeisajili kwa vitambulisho chako bado uwe na hofu na hili tena, basi hata kusajili laini ungeacha kabisa kama wewe ni mtu wa matukio.
 
Iko mda tu mbona mi laini zangu zote Airtel na Vodacom nilirenew ili iwe za 4g zote lazima uingize pin Kwanza.
 
Hivi ni kwa nini wako busy kujaza ma security kila kona...mara FINGERPRINT, sasa wanalzimisha nikizima simu nikiwasha lazima niingize code? Y? Mbona nchi zilizoendelea hawana huu ushamba... nahisi mule kuna watu wamesoma IT zao sasa hawana kazi ndo wanabuni buni mambo tu.
 
Hiyo code inakuwa linked na TCRA kwahiyo ukifanya kimeo chochote hawahangaiki kukupata

Kukupata hawahitaji kufanya ivo ni easy tu
CDR inasomwa kirahisi sana mkuu Serikali ikikutaka inakupata anytime labda uache kabisa kutumia simu maishani
 
Hiyo code inakuwa linked na TCRA kwahiyo ukifanya kimeo chochote hawahangaiki kukupata
Acha upotoshaji.
Laini kuwekewa PIN inazuia mtu mwingine asiitumie kufanya uharifu.

Ukifanya kosa wakikutaka wanakudaka mapema maana tayari uko kwenye system yao
 
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema ifikapo Julai mosi, laini zote zitakazotolewa zitakuwa na neno la siri ambalo mteja atatakiwa kulibadilisha ili kutumia laini mpya yenye usalama.

Kwa mujibu wa ujumbe uliosambazwa jana kwenye simu za wateja mbalimbali ambao ulithibitishwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa TCRA, Semu Mwakyanjala, utaratibu huo utalinda wateja.

Alisema utaratibu huo una lengo la kuwalinda wananchi kwenye matumizi ya mawasiliano.

“Laini inapopotea ikachukuliwa na mwingine anaitumia vibaya lakini kwa kuwa na neno la siri, itamlinda mtumiaji na kuondokana na utumiaji usio salama,”alisema.

Mwakyanjala alisema utaratibu huo ni kwa mujibu wa sheria ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010 na kanuni zake za 2018.

“Tunataka matumizi bora ya mifumo ya simu si kwa ajili ya kuongea bali kama benki, hivyo usalama ni muhimu kwa ajili ya kuwalinda watumiaji, watu watumie simu kwa biashara na maendeleo kuliko kufanya uhalifu,”alisema.


Ippmedia
 
Hizo PIN zilikuwapo tokea zamani ila hazikua activated by default.
 
Screenshot_20210221-131224.png

Ndio hawa!
 
Wakulungwa hii ina tofauti gani na Sim Pin Code?! Au hii hutokuwa na uwezo wa kuidisable?!
 
Back
Top Bottom