TCRA mchukulieni hatua huyu Nabii Tito, channel yake ya YouTube inamdhihaki Yesu

TCRA mchukulieni hatua huyu Nabii Tito, channel yake ya YouTube inamdhihaki Yesu

vipi kuhusu mtume wenu adhalilishwe, utasema tcra haisomi quran? Kama hamjaanza kumtetea wenyewe kwa jazba.
Mimi nina mtume tena?? Mimi ni mwafrika pure. Mitume wangu ni viongozi wangu wa kimila waliokuwa na nguvu kuu ya asili na kutenda makubwa.

Leo hii mnamtetea Yesu na Mohamed utafikiri mna undugu nao. Mababu zako ambao leo hii wakifukuliwa mabaki yao wakapimwa wewe hapo una DNA zao unawaita mizimu, alafu hawa mababu wa waisrael na waarabu ambao hata huna uhakika kama walikuwepo unawaita watakatifu na kuwatetea wakisemwa vibaya upo tayari kupigana! Hiyo ni akili au tope??

Hebu turudi kwenye asili yetu waafrika.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Huyo nabii Tito ni mfuasi wa dini gani? Ikiwa ni Muislam inabidi ahukumiwe kwa kudhihaki dini ya wengine, ila ikithibitika kua ni mkristo hapaswi kufanywa lolote.

Hata wewe ukimuita baba yako mlevi, hautakua umekosea, ila sio mtu mwengone amuite baba yako mlevi, huo ni ugomvi wa kiwango cha juu sana.
 
Kwani Ndugai aliposema YESU alisafiri na mkewe.

Hao TCRA walichukua hatua gani?

TUACHE DOUBLE STANDARD, jamaa anasema anachokiamini yeye.View attachment 2002673
Uzuri wa YESU hahitaji jeshi kumpigania na kila anaye mkejeli ni kwafaida yake mwenyewe kila mtu anayo mawazo yake kuhusu huyu YESU na wote anawackiliza na kila mmoja wetu atapokea kama alivyotenda
 
Hawa wahuni akina tito washukuru Mungu kwenye ukristo hakuna munkari na jazba, wahuni wanakunya na kuharisha uharo kunuka wala hakuna mkristo anaoshughulika nao. Ole wao wangeidhihaki ile dini na mtume wao cha mtema kuni wangekiona
Siyo kweli, yule Dr wa kule Pemba aliyejirekodi Akitangaza kuwa mtu alikuwa anananihiwa mbona aliishia kufukuzwa Kazi tu na hakufanywa chochote?
Watu Hawa dawa yao Ni kuwapoteza kimyakimya tuu hakuna haja ya kusubiri serikali au kanisa au msikiti is o
 
-Pale kila dini/dhehebulitakaposema dini/dhehebu jingine linafundisha uongo ndio tutaelewa uhuru wa dini na uhuru wa mawazo. Kutokubaliana na Nabii Tito kusikufanye kuiomba serikali ichukulie hatua.

-Hapa kuna kitu kinaitwa thesis na antithesis (kupitia uchokozi wa nabii Tito unaweza kukuta anatumika kuchochea ili kutoa nafasi kuingiliwa uhuru wa dini wa watu)

-Yesu alitukanwa na kuambiwa anatoa pepo kwa Belzelbul, kutemewa mate na matusi mengine mengi, alijibu hoja kwa hoja si na alipotakiwa kukaa kimya alikaa kimya. Lakini hakuita serikali za dunia kumsaidia kutetea imani yake.

-Kuna watu wanatengeneza matukio ili kupitia tukio moja wapate kuingilia si kwa Tito tu bali dini ndogo zisizo na sauti.

-Tito kumwita Yesu majina yasio yake anatakiwa ajibiwe kwa kumfundisha kilicho sahihi/ajibiwe kwa hoja si kwa kushughulikia akaunti yake.
 
Umesahau "nabii" Mwingira alimuombea na kudai amemtoa mapepo?
 
Ifike wakati matumizi ya neno askofu na nabii yawe regulated.

Nashangaa sana yule mkandamizaji kujiita askofu.
Tanzania kuna Uhuru wa maoni,yuko kwa mtazamo wake.kavunja sheria gani kuandika alivyo andika
 
Ewalaaaàaaaa umenena
 
Nabii Tito!

Nalog off

FDhVvGBWQAIr1RO.jpg
 
Huyu nabii Tito anamuita Yesu ni shetani kule nabii billionaire Shilla anamuita Yesu mwizi..basi ni tafrani
Kuna agenda ya kudhalilisha Yesu kwa kukufuru ili watu wapandishwe mivyeo huko Freemasons waliko

Mojawapo ya hitaji huwa Ni kukufuru.Unakufuru kwenye public Ndipo upande

Alianza spika Ndugai kukufuru akasema Yesu alikuwa na mke

Akaja Nabii Shilla akasema Yesu alikuwa mwizi

Sasa huyu Nabii Tito naye ndio anakuja na lake la kukufuru kuwa Yesu Ni Shetani

Ni agenda maalumu ya kumchafua Yesu kwa maslahi ya kidunia
 
TCRA na vyombo husika mchukulieni hatua huyu nabii Tito channel yake youtube kaandika YESU ni shetani

Hii ni hatari kwa jamii oneni wenyewe
View attachment 2002720
huyu muhuni aliombewa na gwajima akatuliza mapepo ya ushoga. Sasa amerudi kivingine. Afande murope alisema jamaa lina vyeti vya mirembe, dishi limeyumba.
 
huyu muhuni aliombewa na gwajima akatuliza mapepo ya ushoga. Sasa amerudi kivingine. Afande murope alisema jamaa lina vyeti vya mirembe, dishi limeyumba.
Kama kichaa TCRA wanatakiwa kufunga hiyo channel sababu channel zinatakiwa kuendeshwa na watu Wenye akili timamu
 
Nyie mnachukulia poa sana,, we mpaka masanja nae mchungaji na kuna yule mwingine wa kuitwa sijui nabii shillah achana na nabii frola hapo, mwanamke wa kwanza tangu kuumbwa kwa ulimwengu kupewa unabii,, sijui siku zake za kuvuja zikiangukia jumapili anaongozaje ibada,, mkiwakalia kimya hawa siku mnaweza kusikia ambaruti nae kajitangaza na yeye nabii,, huo ujinga ungekuwa upande wetu hao tushawakalia jamvini hivi tunawamezea mate ya akili ili tujue kama tunaanza kufyeka shingo au kiwiliwili,,,
 
Kagame kwake kaweka sheria kali bila ya digrii huruhusiwi kujiita hivyo...sio huku mtu akijua mistari 5 ya biblia basi askofu,nabii nk
Ifike wakati matumizi ya neno askofu na nabii yawe regulated.

Nashangaa sana yule mkandamizaji kujiita askofu.
 
Wakuu mi niko tofauti na wengi wenu hapa. Hapa nnchini kuna madhehebu mengi tu na yana mitizamo tofauti tofauti juu ya hiyo hiyo biblia moja.

Huyo tito, dogo shilla na wengine wengi wamekosa tu namna ya kuwasilisha mawazo yao. Wanayawasilisha kwa njia mbovu za kutweza utu wa watu wa dini nyingine. Ila hizo ni imani zao.

Hata Mungu mwenyewe alitupa uhuru wa kuchagua chema na kibaya ila mwisho wa siku utahesabiwa. Hata hao wana uhuru wa kuamini vile watavyoona inafaa.

Serikali iwapige rungu kwa uwasilishaji aao mbovu na wa kejeli kwa watu wengine wanaoamini tofauti na wao na lugha za matusi na kufedhehesha.
 
HILO JAMAA DISHI LIMEYUMBA TOKA KITAMBO, MSIPOTEZE MUDA KUMDISCUSS. MKITAKA KUAMINI JARIBUNI KUFUATILIA CLIP ZAKE HUKO YOUTUBE ZA TOKA KIPINDI CHA NYUMA.
 
Tanzania kuna Uhuru wa maoni,yuko kwa mtazamo wake.kavunja sheria gani kuandika alivyo andika

The guy is mocking those who believes in Jesus, Remember you are only free if and only if your freedom does not affect others.
 
Back
Top Bottom