Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 17,080
- 33,076
TCRA hakuna jibu hapa..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unadhani basi hata alikuwa serious, alikuwa anachangamsha tu kijiwe. Kesi unadhani mchezo.Tumia au shirikiana na mwanasheria kuongeza uhakika wa kushinda na kiwango Cha fine
Mkuu,napingana na wewe kwa kitu kimoja hapa. Wewe mwenyewe huwezi kuandaa mashitaka. Haiwezekani. Kwani wanaotumia wanasheria hawana akili?Washitakiwa hapa inabidi awe mtu niliyewasiliana naye make mimi.sijui ni nani aliyemtuma, madam namba zinazotumika ni namba binafsi mimi nataka kwanza mpiga simu apatikane akishapatikana yeye ndo atataja kampuni inayomtuma.
Mshitakiwa namba moja ni mpiga simu na mshitakiwa namba mbili ni app aliyataja kuiwakilisha
Usikariri mambo kwani kuandaa mashitaka lazima uwe mwanasheria? Na uanasheria kwako ni nini? Wafungwa huko magerezani wanajiandikia rufaa na wanashinda itakuwa huyu mpuuzi mmoja aliyeingilia mawasiliano yangu na kuniharass pasipo kuwa na makubaliano na mimi, Kwa nini anitambulishe mimi kama mdhamini wa mtu ambaye wameingia naye makubaliano bila mimi kuwepo? Unatambua vigezo vya kuitwa mdhamini?kama unavijua basi mimi namba yangu kuwa kwenye simu ya fulani haimpi mamlaka ya yeye kunitukana na kunitumia sms za matusi na vitisho kila mara
Yeye alikuweka kama mdhamini wake.Akishindwa kulipa unafuatwa wewe.Laumu huyo ndiguyo aliyekuweka kama mdhamini wakesidhani kama umesoma na kuelewa nilichoandika, suala mtu kukopa ni utashi binafsi swali langu ikiwa mtu mwingine amekopa kwa mdai aende kwenye simu ya mdaiwa na kuanza kuharass watu wasiohusika? unawezaje kuniita mdhamini kwa vile umeona namba yangu kwenye phone contact za mkopaji? huo ndo msingi wa swali langu.
Kama elimu na uwezo wako ni mdogo huwezi hata kusoma ukaelewa sina namna ya kukuelewesha zaidi? Unajua maana ya mdhamini? Mdhamini anawekwa? kivipi yani? Dhamana inatambulika endapo mdhmini ameridhia kwa kuweka sahihi,picha, kitambulisho na utambulisho kutoka serikali ya mtaa wake anakoishi huo ndo udhamini. Siyo huu ujinga na upuuzi ambao wewe unaona ni udhamini.Yeye alikuweka kama mdhamini wake.Akishindwa kulipa unafuatwa wewe.Laumu huyo ndiguyo aliyekuweka kama mdhamini wake
Usichokijua wewe nyamaza tu, hili suala limeenda mbali mno kwa taarifa zako na hata google wenyewe wanataarifa, achilia mbali BOT au hukuona BOT na hata polisi wamefanya press kuhusiana na hizi App?? Mimi siyo miongoni mwa wale wanaopuuza jambo, kifupi sina jambo dogo hasa ninapoona linahusisha upuuziUnadhani basi hata alikuwa serious, alikuwa anachangamsha tu kijiwe. Kesi unadhani mchezo.
Usichokijua wewe nyamaza tu, hili suala limeenda mbali mno kwa taarifa zako na hata google wenyewe wanataarifa, achilia mbali BOT au hukuona BOT na hata polisi wamefanya press kuhusiana na hizi App?? Mimi siyo miongoni mwa wale wanaopuuza jambo, kifupi sina jambo dogo hasa ninapoona linahu
mkuu kuna mahali nilisoma usibishane na shetani mpuuze utapoteza mda wako, usipokee simu zao sababu wewe binafsi unajua hao ni matapeli usijibu sms zao, na kama hawajaingilia mawasiliano yako hakuna tatizo nchi hii matapeli wengi utabishana nao wangapi labda kama huna kazi za kufanya.Ndugu wanajamvi, Asalaam Aleikhum.
Kama kichwa cha habari kilivo hapo juu nimejikuta na kuwa mhanga wa hawa matepeli wa APP za mitandaoni. Iko hivi kuna mtu ambaye ninafahamiana naye ama ni mtu wangu wa karibu ktk familia, kwa utashi wake binfasi alikopa kwa hawa jamaa, alikopa lini na kiasi gani sijui. Kilichotokea ni kupokea sms kutoka namba 0699 065 *** ikinijulisha kuwa kuna mtu alikopa hela na kuniweka mimi mdhamini. Na kwakuwa nilishapata taarifa za hawa watu nikawajibu kistaraabu tu kuwa huyo mtu mnayemsema simjui hivo mtafuteni wenyewe.
Baada ya siku moja akaibuka tena mtu mwingine mwenye namba 0622 297*** huyu yeye tofauti na yule awali alipiga simu hoja zikawa zile zile kuwa nimemdhamini mtu mkopo na amewatapeli hivo nami nimhusika wa huo utapeli. Nikamwuliza unajua sifa za mtu kuitwa mdhamini? Na je kabla ya kukubali kwamba mimi ni mdhamini mlipata consent yangu? kuna mahali nilisaini? Baada ya hapo kilichofuata ni matusi ya nguoni. nilichofanya na kwa kuwa nilitarajia atatukana hivo nilirekodi kila kitu. Baada ya hapo nikaenda kweny App husika iliyotajwa kwa jina la Ustawi Loan, nikapitia privacy Policy nikagundua uhuni mwingi sana kwenye hizi App, uhuni mmoja nikuingilia mawasiliano ya watu, hizi App zinachukuwa taarifa za mkopaji kwa maana ya sms na ku access camera.
Swali ni moja tu kwa nini TCRA imerhusu huu ujinga, yaani usalama wetuuko wapi kama mhuni mmoja kutoka makumbusho akisimamiwa na wachina ana uwezo wa kuingilia mawasiliano ya faragha ya watu kisa kuna mtu amekopa kwao. Fine mtu amekopa kwa nini third party nihusishwe na huu upuuzi.
Haya leo tena mjinga mmoja katuma sms akitumia namba 0789 713 *** huyu naye kajitambulisha eti anatoka PESA CASH naye hoja zake ni zile zile nimejaribu kumwuliza mhusika ulikopa shilingi ngapi na lini? anasema alikopa shilingi elfu 50 wiki moja iliyopita lakini mpaka jumatatu iliyopita alikuwa anadaiwa 130K haya kuhusu hii App ya pili yeye anasema hajakopa chochote kwao lakini wao wanasema wanamdai 168K kwa uchunguzi wangu mfupi nimegundua hizi APP zaidi ya 30 ziko chini ya mwamvuli mmoja.
Ikiwa wako kisheria mimi sina shida nao, shida yangu ni kwa nini TCRA wameruhusu wahuni kuchezea Privacy zetu? Na hawa walivowajinga wanatumia namba walizosajili wao binafsi. Kwa takribani wiki nzima natafuta mawasiliano na TCRA lakini kila nikipiga simu naishia kusikilizishwa mziki tu.
Najipanga kuwashitaki mimi huwa sina issue ndogo very soon mtanisikia nikiwa nao mahakamani. Katika hili wala sihitaji mwanasheria nasimima nao mwenyewe.
Mrejesho kuhusu kesi yangu na app za mikopo
Kama nilivoahidi kuwa leo Jumatatu tarehe 26/02/2024 naanza mchakato wa kuwashitaki hawa watu. Nimeanzia TCRA ambako nimepeleka malalamiko yangu, Majibu ya TCRA ni kwamba wao hawahusiki kwa sababu hasimamii watu bali wabasimamia makampuni ya mawasiliano. Hii kidogo imeshitua hivo ikabidi niende...www.jamiiforums.com
Usijali kila ninapopata muda wa kuwajibu nitawajibu hawa wajinga wachache ambao wanahisi wanajua saana, ili hali wanasoma kichwa cha habari na kucoment bila hata kuelewa dhima nzima ya mwandishimkuu kuna mahali nilisoma usibishane na shetani mpuuze utapoteza mda wako, usipokee simu zao sababu wewe binafsi unajua hao ni matapeli usijibu sms zao, na kama hawajaingilia mawasiliano yako hakuna tatizo nchi hii matapeli wengi utabishana nao wangapi labda kama huna kazi za kufanya.
Naomba muendelezo nataka tuungane dhidi ya huu mtandao wa wahalifu umefikia wapi.Usichokijua wewe nyamaza tu, hili suala limeenda mbali mno kwa taarifa zako na hata google wenyewe wanataarifa, achilia mbali BOT au hukuona BOT na hata polisi wamefanya press kuhusiana na hizi App?? Mimi siyo miongoni mwa wale wanaopuuza jambo, kifupi sina jambo dogo hasa ninapoona linahusisha upuuzi
Kumbe ndio wewe ulioanzishiwa group la Whatsapp kuwa una uza........... ili upate pesa ya kulipa deni la Mkopo wa Mtandaoni?Mimi pia ni mhanga wa group la whatsapp la matusi makubwa sana kuandikwa hapa. Niambie umefika wapi na mimi nichukue hatua boss