TCRA mmeamua kuuza utu wetu kwa wahuni wa App za mikopo mtandaoni

naomba kutukana hapa JF kuwa TCRA ni kinyeo cha ccm wakijibu nijibu ili kuwa sio idara ya mawasiliano na cyber
 
Mkuu,napingana na wewe kwa kitu kimoja hapa. Wewe mwenyewe huwezi kuandaa mashitaka. Haiwezekani. Kwani wanaotumia wanasheria hawana akili?
Mahakamani ni sehemu nyingine, na haushindi ukweli tu. Kuna vigezo kibao. Kuanzia uandaaji na misamiati inayotumika.
Labda ungesema utamtafuta mfungwa akusaidie. Wanapokuwa mle ndani,wamo wanasheria,wamo waliofungwa mara kibao,wamo waliosimama mbele ya mahakama.

Na huku wamo wengi wa kukupa muongozo,ila jera,wapo vizuri kwenye shelia. Ukimpa kama hii,lazima pesa iingie.
 
Yeye alikuweka kama mdhamini wake.Akishindwa kulipa unafuatwa wewe.Laumu huyo ndiguyo aliyekuweka kama mdhamini wake
 
Yeye alikuweka kama mdhamini wake.Akishindwa kulipa unafuatwa wewe.Laumu huyo ndiguyo aliyekuweka kama mdhamini wake
Kama elimu na uwezo wako ni mdogo huwezi hata kusoma ukaelewa sina namna ya kukuelewesha zaidi? Unajua maana ya mdhamini? Mdhamini anawekwa? kivipi yani? Dhamana inatambulika endapo mdhmini ameridhia kwa kuweka sahihi,picha, kitambulisho na utambulisho kutoka serikali ya mtaa wake anakoishi huo ndo udhamini. Siyo huu ujinga na upuuzi ambao wewe unaona ni udhamini.
 
Unadhani basi hata alikuwa serious, alikuwa anachangamsha tu kijiwe. Kesi unadhani mchezo.
Usichokijua wewe nyamaza tu, hili suala limeenda mbali mno kwa taarifa zako na hata google wenyewe wanataarifa, achilia mbali BOT au hukuona BOT na hata polisi wamefanya press kuhusiana na hizi App?? Mimi siyo miongoni mwa wale wanaopuuza jambo, kifupi sina jambo dogo hasa ninapoona linahusisha upuuzi
 

mkuu kuna mahali nilisoma usibishane na shetani mpuuze utapoteza mda wako, usipokee simu zao sababu wewe binafsi unajua hao ni matapeli usijibu sms zao, na kama hawajaingilia mawasiliano yako hakuna tatizo nchi hii matapeli wengi utabishana nao wangapi labda kama huna kazi za kufanya.
 
Usijali kila ninapopata muda wa kuwajibu nitawajibu hawa wajinga wachache ambao wanahisi wanajua saana, ili hali wanasoma kichwa cha habari na kucoment bila hata kuelewa dhima nzima ya mwandishi
 
Mimi pia ni mhanga wa group la whatsapp la matusi makubwa sana kuandikwa hapa. Niambie umefika wapi na mimi nichukue hatua boss
 
Naomba muendelezo nataka tuungane dhidi ya huu mtandao wa wahalifu umefikia wapi.
 
Mimi pia ni mhanga wa group la whatsapp la matusi makubwa sana kuandikwa hapa. Niambie umefika wapi na mimi nichukue hatua boss
Kumbe ndio wewe ulioanzishiwa group la Whatsapp kuwa una uza........... ili upate pesa ya kulipa deni la Mkopo wa Mtandaoni?
 
Kabla hujaenda mahakamani hakikisha unasoma terms & condition zao. Kumbuka wewe ndo umekopa kwao kwa hiyo ulikubaliana na masharti yao aidha kwa kujuwa ama kutokujua.
Tusikurupie hii mikopo ya mitandaoni maana policy zao sio rafiki, haziko kukunufaisha wewe!
 
Chukua pesa zao then piga kimya..pesa za burebure hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…