TCRA yatoa onyo kali kwa makampuni na watu binafsi wanaosambaza visimbuzi vya CANAL PLUS

TCRA yatoa onyo kali kwa makampuni na watu binafsi wanaosambaza visimbuzi vya CANAL PLUS

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
images (1).png

TCRA imetoa onyo kali kwa Makampuni na Watu binafsi wanaoingiza nchini vifaa vya mawasiliano vikiwemo visimbuzi vya CANAL PLUS na kufanya biashara ya kutoa huduma za Televisheni kupitia satelaiti bila kuwa na leseni, imesema visimbuzi hivyo havijaidhinishwa.
 
View attachment 2464442

Uwezi kuzuia utandawazi labda kama kinatumia frequency za tanzania kusambaziwa.
 
Hivi haiwezekani kuwa na kisimbuzi kimoja ambacho mtumiaji ataamua mwenyewe ajiunge na mto huduma gani, either Azam, DSTV, Canal+ nk...

Hii biashara unakuta nyumba moja inavisimbuzi 40 na dish 40, ni uchafu tu.
kwanini usitumie dish moja na kisimbuzi kimoja ukawa na uwezo wa kupata chanell zote..
 
Walichokifanya hapa TCRA ni kama kutangaza biashara ya ving'amuzi cha Canal+ pasipo kujua, maana hata sisi tusiokijua hicho king'amuzi tunaweza kukisaka ili tukipate.

Halafu hao TCRA wamekaa kichawi sana, wanaacha kufuatilia mambo ya msingi yanayotuumiza sisi walalahoi, wao wanakimbizana na vitu vingine ambavyo ni msaada kwa walalahoi. Katika hili TCRA walipaswa kukaa kimya kimtindo.
 
Canal+ ina nini kipya kuzidi akina DStv, Azam, et. al? Mwenye kufahamu please.
Bei ya kifurushi ipo chini. Ukilipa elfu 36 kwa mwezi unatazama ligi mbalimbali za Ulaya ikiwemo England, Uefa, Ueropa, nk, tofauti na Supersport gharama ipo juu.

Vibanda umiza wanavitumia sana. Wanatuma hela wakala yupo Burundi ndio anawanunulia vifurushi.

Kwa nini gharama za vifurushi vya ving'amuzi bongo ipo juu sana? mana naskia hata Supersport ya South Africa ipo chini. Azam ya Burundi pia ipo chini!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom