TCRA yawafungia Wasafi FM kwa kutumia lugha za matusi

Mi najiuliza kwanini wafungiwe baada ya kufungiwa clauds Hali yakuwa wasafi ndio walioanza kutenda kosa?
 

..mbona Jpm anatukana waziwazi lakini hakuna hatua zinazochukuliwa?

..Baba Levo angekuwa amewatukana wapinzani asingechukuliwa hatua.
 
Safi Sana TcRA na nyimbo zao za matusi matusi za Yako na Yangu Zikigusana Nalegee Fungia. Na Baby Come into my Bedroom I Wana show you Love Fungia. I wish TcRA mngekuwa Baraza la Sanaa haya mamusic ya Ngono mngeshafungia na kufuata mitandaoni. TcRA keep it up hawa watanngaza Ngono hadharani Wakome.
 
Kamanda mbona kichwa maji hivyo? Umejua wamekiuka sheria gani na wamekosea nini?
Wametumia lugha isiyofaa kimaadili(lugha ya matusi)

Je unajua hasara ya kufunga kituo cha habari kwa siku 7 na matangazo ya biashara ya wadhamini kutoenda hewani kwa siku hizo?

Mimi naamini walipaswa kupigwa fine kubwa tu ya maana ila sio kufunga kituo cha radio kurusha matangazo.

Wakati hizi sheria mpya kandamizi zilivyokua zinapitishwa na maCCM walichekelea wakadhani zitaishia kufungia Tanzania daima.
 
Hivi hawa tcra hawana adhabu ya onyo kwanza mbona wanakimbilia kutia watu hasara bila ulazima? Hivi Nchi zingine ndo vyombo vya habari hufanyiwa hivi au ni sisi tu? Nmeamini kumbe hata kuunga mkono juhidi hakusaidii.
 
Sure....
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Tatizo Mnaliangalia Kwa Jicho Tofauti...

Watu Wametukana HADHARANI waachwe?!!!

Bila ya KUSIMAMIA MAADILI,WELEDI NA TAALUMA ya habari tutafika Kweli?!!!

TCRA Wamefanya JAMBO SAHIHI!!!
 
Hapana tutaweka sheria ya kuwajibisha wakosaji na sio sheria za kukomoana kama tupo North Korea.
Mkuu Sasa Hapo Wamekomolewa Nini?!!!

Nina hofu na Serikali Yenu.... Kwani Siku Mkiingia Madarakani, Basi kila mtu atafanya atakalo na kuwa zaidi ya RUKSA ya Mzee Wetu Ali Hassan Mwinyi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…