Teach Men Fashion: Kuna baadhi ya Mavazi "Mwanaume" sio vema kuvaa na Kutoka Nje

Teach Men Fashion: Kuna baadhi ya Mavazi "Mwanaume" sio vema kuvaa na Kutoka Nje

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Wakuu.

Hii nchi ni huru, kila mtu ana ruksa ya kuvaa nguo yoyote anayopenda kikubwa asivunje sheria tu za nchi.

Ila kuna baadhi ya mavazi, mwanaume sio vizuri kuvaa na kutoka nje kutembea nje mbele ya kadamnasi. Hapa ni baadhi ya mifano mitano (5):

1. Vipensi kuonesha Mapaja.
Kuna watu wanavaa pensi fupi sana na za kubana, zinaonesha mapaja nje nje. Na wanatembea comfortably kwenye malls au mitaani.
images (9).jpeg

Ni kweli hatuwapangii maisha, ila sio vizuri Mwanaume kuonesha mapaja yako nje nje.

Mbadala:
Kama ni mdau wa pensi tafuta dude pana linaficha ata magoti ukiwa umekaa. Unaweza tupia jeans, au kama za basketball.

images (10).jpeg

images (11).jpeg


Hayo ni mawazo yangu tu.

2. Jeans za kubana au kuchanika chanika.
Hii inaendana na vipensi, sio poa kijana unavaa jeans la kubana sana au lilochanika chanika.
images (12).jpeg

images (15).jpeg

Mbadala vaa tu slim jeans, au track inayokufit ila sio kukubana ivo wala imechanwa.
images (16).jpeg

Iko poa itakupendeza.

3. Crocks na ndala.
Hizi Crocks kuna wanaume wanavaa hafu wanatoka out kabisa comfortably.

images (17).jpeg

Hapa unaweza kuvaa ndani na mtaani tu labda unaenda shop, au upo beach.

Mbadala:

Kuna sandals za kiume unaweza ukavaa na ukaonekana vizuri sana.
images (18).jpeg

Huna haja ya kuvaa madude aya kitoto au kivulana mitaani.

4. T-shirt zenye maandishi au Alama za ajabu.
Kuna hizi Tshirt either by coincidence au purpose unakuta ina maneno na wewe una nunua inaivaa.
images (19).jpeg
images (20).jpeg


Mwanaume vaa tu plain tshirt au simple one word kama unataka maneno mengi vaa zako jezi tosha kabisa.

5. Nguo za Mfanano na Mpenzi wako kipindi cha Matukio.
images (21).jpeg

She is my Queen. Au My Valentine. nk. Tuwaachie madogo wa Magufuli Hostel.

Asanteni.

Narudia kusema, ayo ni mawazo binafsi. Karibuni kwa mawazo yenu.
 
Kwenye viatu hapo.. nakumbuka nilipata Pisi kali kisa viatu tu....

Mie ni mtu wa kuvaa boots 👢 za kupanda.. kumbe watoto wakike ndio ugonjwa wao bhana...
 
Back
Top Bottom