GE2025 TEC: Ewe Mungu, Tuma Roho wako, afanye upya uso wa Nchi kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025

GE2025 TEC: Ewe Mungu, Tuma Roho wako, afanye upya uso wa Nchi kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Doctor Mama Amon

Platinum Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
2,311
Reaction score
3,513
1754894043572.png


Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania , TEC, Askofu Wolfgang Pisa​

Muhtasari wa habari

Kibwagizo cha ujumbe wa Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) katika Sala na Mafungo ya kuombea haki na amani yatakayofanyika siku ya tarehe 23 Agosti 2025, kitakuwa tamko kwamba "Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania."

NI kibwagizo kinachotokana na fundisho la Zaburi ya 104:30 isemayo kwamba: “Waipeleka roho yako, Ee Bwana, Wanaumbwa upya, Nawe waufanya upya uso wa nchi” (Zaburi 104:30)

Maaskofu Katoliki wanakusudia kufafanua tamko kwamba "amani ni tunda la haki, usawa, ukweli, mshikamano na ustawi wa wote,” Watataka “chuki ishindwe na upendo,” Watashawishi “kisasi kiuachie nafasi msamaha,” Watahimiza “ugomvi ugeuzwe kuwa urafiki,” Watahamasisha "maadui warejee kwenye mazungumzano," na Watahanikiza "wapiganao wapeane mikono."

Hivyo, sasa ni wazi kwamba Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limeamua kufuata nyayo za Mtakatifu Fransis wa Assiz, Mwalimi Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania, pamoja na Papa Yohane Paulo II, kuhusu ajenda ya kudumu ya kupigania haki na amani.

Katika sala yake ya kuombea haki na amani, Mtakatifu Fransis (1182–1226), mzaliwa wa Italia, anamwomba Mungu amfanye “chombo cha amani” ili aweze kugeuza chuki kuwa upendo, majeraha kuwa msamaha, mashaka kuwa imani, kukata tamaa kuwa matumaini, giza kuwa nuru, na huzuni kuwa furaha.

Mwalimu Nyerere, mwaka 1961, alizindua Mwenge wa uhuru ili autumie kama alama inayoonekana kuwakilisha ndoto yake ya “kugeuza giza la dhuluma kuwa nuru ya haki” katika Taifa jipya.

Naye Papa Yohane Paulo II, wakati wa ziara zake za mwaka 1979 hadi 1989, nchini Poland, alitumia kaulimbiua iliyobeba maneno ya Mzaburi kufanikisha ajenda ya “kuufanya upya uso wa nchi” kwa kuhubiri haki na amani nchini humo.

Mkakati wake ulianzia kwenye maneno ya Zaburi yasemayo kwamba, “Waipeleka Roho yako Ee Mungu, wanaumbwa upya, nawe waufanya upya uso wa nchi.” (Zaburi 104:30).

Huu ndio ujumbe unaosindikiza Mafungo ya Kanisa katoliki kwa ajili ya “Kuomba Haki na Amani” nchini Tanzania utakaohitimishwa tarehe 23 Agosti 2025.

Kwa ufupi, tunaweza kusema kwamba, TEC wameamua kutembea katika nyayo zote hizi.

Habari Kamili

Tarehe 23 Agosti 2025 Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) linakusudia kushirikiana na mapadre, masista, waseminari, Makatekista, Wawata, Viwawa, Uwaka, Kwaya, Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikatoliki, na watu baki wenye mapenzi mema kutoka jumuiya rafiki.

Jumuiya hizo ni pamoja na Walutheri, Wapentekoste, Wasabato, Waislamu, Wakulima, Wafanyakazi, Wafanyabiashara, na Wanafunzi, kufanya Sala na Mfungo kwa ajili ya kuomba haki na amani.

Kulingana na Rejesta ya taarifa za Kanisa Katoliki nchini Tanzania, toleo la mwaka 2020, mafungo haya yatafanyika katika Majimbo Makuu 7, Majimbo 34, na parokia 1,291 zinazojumuisha mapadre zaidi ya 3,201 na masista wapatao 12,000 wanaohudumia wakatoliki 18, 076,000, sawa na 30.4% ya Watanzani wote.

Mafungo haya yatafanyika
kwa ajili ya
kutekeleza kazi zifuatazo katika muda wa masaa 24, kuanzia asubuhi ya Jumamosi, tarehe 23 Agosti 2025 hadi asubuhi ya Jumapili, tarehe 24 Agosti 2025:

Kutoa elimu ya uraia kwamba "Amani" ni mtoto wa "Haki,"
Kwamba "a
mani" ni tunda katika mti wa "haki."
Kwamba "amani" ni tunda la "usawa,"
Kwamba "amani" ni zao "ukweli,"
Kwamba "amani" ni mavuno yaletwayo na "mshikamano,"
Kwamba "amani" ni faida itokanayo na "ustawi wa wote,"
Kwamba "amani" inatokana na uwepo "haki,"
Kwamba
Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kutoa elimu ya uraia kwamba "Haki" ni mzazi wa "Amani,"
Kwamba "haki" ni kikonyo cha mti wa "amani,"
Kwamba "haki" ni chimbuko la "amani,"
Kwamba "haki" ni alama ya "amani,"
Kwamba "haki" ni sababu ya "amani,"
Kwamba "haki"
ni chanzo cha "usawa,"
Kwamba "haki" husababisha "mshikamano,"
Kwamba "haki" ni huleta "ustawi wa wote,"
Kwamba
Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kutaka “chuki ishindwe na upendo” wa kweli ,
Kushawishi “kisasi kiuachie nafasi msamaha” uletao amani,
Kuhimiza “ugomvi ugeuzwe kuwa urafiki” wa kudumu,
Kuhamasisha "maadui warejee kwenye mazungumzano,"
Na kuhanikiza "wapiganao wapeane mikono" ya amani,
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kupigania "uhuru wetu huu usipokonywe" na mamluki,
Yaani wale ndumilakuwili wanaocheza kotekote,
Wakitumiwa na maadui zetu wa kihistoria,
Kwa upande mmoka kuna makuwadi wa utumwa,
Utumwa huu ulioendeshwa na Waarabu kwa miaka 1,200,
Yaani tangu 700 BK mpaka 1,909 BK,
Pia kuna makuwadi wa
ukoloni mkongwe
Ukoloni huu ulioendeshwa na Wazungu,
Kwa kipindi cha miaka 77,
Yaani tangu mwaka 1884 hadi mwaka 1961

Hawa walitoka Ureno, Ujerumani na Uingereza.
Kwamba
Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kuwaombea watu "waliopotea wapatikane,"
Tena "wapatikane" wakiwa hai.
Kama watu "waliopotea" wamekufa
Kuombea maiti zao ili zirejeshwe
KIsha wazikwa kwa heshima zote
Kulingana na mila na desturi za kiutu.
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kuwatetea "waliotekwa wapate uhuru wao."
Yaani "uhuru wao" dhidi ya utumwa,
Waweze kurudi uraiani wakiwa raia huru,
Pia watekaji wao wahukumiwe kwa haki,
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kuwafariji "walioumizwa wapone,"
Halafu warejea katika majukumu yao,
Kisha waliowaumiza wahukumiwe kwa mujibu wa sheria,
Zinazofahamika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kwamba
Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kuomboleza kwa ajili ya "waliouwawa wapate uzima wa milele,"
Upatikanao mbinguni mbele ya kiti cha enzi ya MUngu,
Na wauaji wao wasakwe na kupata adhabu stahiki
Tena kwa mujibu wa sheria,
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kukemea "uovu ukome katika nchi yetu,"
Kwa kuhakikisha watenda maovu wanaadhabiwa,
Tena kwa mujibu wa sheria za nchi yetu,
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kuweka mkakati wa kufukuzia "maisha mema zaidi"
Tena "kadiri iwastahilivyo wana wa Mungu,"
Yaani Mungu aliye kilele cha wema wote,
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kuhubiri juu ya "hekima ya kutafuta ukweli,"
Tena "ukweli katika mambo yote,"
Tuweze kujitenga na uwongo, na upotoshaji,
Tuweze kuachana naulaghai na utapeli wa kisiasa,
Utapeli huu hutumiwa na watu wahuni,
Hawa hukweza maslahi binafsi juu ya maslahi ya umma wote,
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kuomba Taifa lipate viongozi waadilifu,
Hasa "watakaosimamia na kuiishi demokrasia ya kweli,"
Kulingana na kanuni za demokrasia ya vyama vingi vya Siasa, Kama zinavyotambuliwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kanuni hizi hukataza uendeshaji wa nchi,
Kwa kutumia kanuni haramu za utawala wa kiimla,
Zile zitumiwazo kwenye dola za kisultani na kichifu,
Pia hutumika katika dola za kifalme na kimwami,
Kadhalika hutumika katika nchi za kikomunisti na kijeshi,
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kuhakikisha kwamba "nchi hii iongozwe na viongozi" makini,

Hasa "ambao ni chaguo la Mungu,"
Yaani yule Mungu wa Haki, Amani na Ukweli,
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kupanda mbegu za ujasiri endelevu,
Kwa ajili ya "kupambana na maovu" yanayotekelezwa na mtandao wa wahuni,
Hasa "yawezayo kutufikia kutokea nje na ndani" ya nchi,
Kutoka kwa maadui zetu wa kihistoria,
Waliokuwa makuwadi wa biashara ya utumwa,
Ulioendeshwa na Waarabu wakatili kwa miaka 1,200,
Tangu 700 BK mpaka 1,909 BK,
Pia wakiwemo makuwadi w
a ukoloni mkongwe,
Ulioendeshwa na Wazungu wakatili,
Hasa kutoka Ureno, Ujerumani na Uingereza,
Wakitutawala kwa miaka 77 tangu 1884 hadi 1961,
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kutafuta nguvu ya "kushinda utengano" na kuhimiza umoja,
Nguvu ya kutokomeza hulka ya "ushindani" na kuhimiza ushirikiano,
Kukomesha "chuki ya ukabila,"
Na kuangamiza ubaguzi kwa misingi ya "utaifa,"
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kuombea mabadiliko ya ndani,
Hasa katika "nyoyo za watenda maovu,"
Pamoja na "washirika wao katika uovu,"
Kusudi wapate ujasiri wa kujisahihisha,
Watubu kwa mawazo, kwa maneno na kwa vitendo.
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.

Kufanya tendo la "kuikabidhi nchi yetu ya Tanzania,"
Mikononi "kwa Mungu,”
Kusudi mtu yeyote atakayejaribu kuchezea rasilimaki zetu,
Au kumomonyoa ukuu wa dola yetu,
Au kupora ardhi yetu na kuwapa wageni,
Awe mgeni wa Mungu mara moja,
Na bendera ya kuhimiza Haki na Amani ianze kupepea nusu-mlingoti,
Kwamba Haki na amani ni pande mbili za sarafu ya Utanzania.


1756126489130.png

Watumwa wa KIbantu walivyoathiriwa na biashara ya utumwa chini ya Waarabu kupitia Bahari ya Hindi (Trans-Indian Ocean Slave Trade, 700 AD-1909 AD)​

Ujumbe huu rasmi, kama ulivyofupishwa hapo juu, unapatikana kwenye aya mbalimbali za sala zifuatazo, kama zitakavyotumika kwenye Sala na Mfungo utakaoanza asubuhi ya JUmamosi, tarehe 23 Agosti 2025:
  1. Sala ya kuanza ibada,
  2. Sala ya kuombea dhabihu,
  3. Sala ya Ekaristi ya Upatanisho,
  4. Wimbo wa Komunyo
  5. Sala baada ya Komunyo, na
  6. Sala ya Kuiombea Tanzania.
Ni wazi kwamba, kutokana na kazi hizi, kibwagizo cha Sala na Mfungo wa mwezi huu kinapaswa kutoka kwenye Zaburi ya 104:30 isemayo kwamba:

“Waipeleka roho yako, Ee Bwana, Wanaumbwa upya, Nawe waufanya upya uso wa nchi” (Zaburi 104:30)




Na jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba, kazi hizi zitafanyika kwa kutumia nyenzo ya kawaida kabisa iitwayo "Misale ya Waumini," kulingana na mwongozo wa Misa Namba 30, katika ukurasa wa 931-932.

Mpango kazi huu imetajwa Katika barua ya tarehe 05 Agosti 2025, kutoka Sekretarieti ya TEC.

Pia umefafanuliwa katika barua ya tarehe 8 Agosti 2025 yenye kubeba maagizo ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar Es Salamaam, Jude Thaddeus Ruwaichi.

Sekretarieti ya TEC imetoa mwongozo wa kitaifa, wenye rejea namba TEC/P/05/08/25 05/08/2025, kuhusu utaratibu wa kutekeleza “Ratiba ya Mfungo Kuomba Haki na Amani Nchini Tarehe 23 Agosti 2025.”

Mwongozo huo ni sehemu ya utekekezaji wa maagizo ya Maaskofu Katoliki kupitia Barua Yao ya tarehe 19 Juni 2025.

Barua hiyo ilitoa wito wa kuandaliwa kwa siku maalum ya “sala na mfungo” kwa ajili ya kuombea “amani” ambayo ni “tunda” la “haki, usawa, ukweli, mshikamano na ustawi wa wote.”

Kila Jimbo litajipangia utaratibu wake wa kutekeleza wito wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, kama ambavyo tayari Jimbo Kuu la Dar Es Salaam limefanya.

Lakini mwongozo wa Sekretarieti ya TEC unatoa mapendekezo ya kitaifa yatakayotumika katika kuiadhimisha siku hii maalum kwa sala na mfungo.

Mwongozo huo kutoka Sekretarieti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, umesainiwa na Padre Alister Makubi, Mkurugenzi Wa Uchungaji wa TEC.

Orodha ya watu waliotekwa, kupotea au kuuwawa


1755006064960.png

Kutoka juu kwenda chini: Deusdedith Soka ametoweka, Mdude Nyagali ametekwa, na Ally Mohamed Kibao ameuwawa.​

Tarehe 09 Agosti 2024 Chama cha Wamasheria cha Tanganyika (TLS) kilitaja orodha ya watu wapatao 83 waliopotea kati ya 2016 na 2024. Orodha husika imeambatanishwa katika fomati ya PDF pia. ​

Na kwa hapa, mkeka wa orodha hiyo ni kama ifuatavyo, mkoa wa makazi ya mhusika ukiwa kwenye mabano.

Kuna Deusdedith Soka na wenzake (Dar), Mohammed Ally KIbao (Dar), Mdude Nyagali (Mbeya), Adinan Hussein Mbezi (Geita), Akidu Twaha Salim (Dar), Albert Kiseya Selembo (Arusha), Alphonce Bilasenge (Kagera), Amon Mrigi Magige (Mwanza), Angel Albert Kamugisha (Dar), Aziz Kinyonga (Dar), Azory Gwanda (Pwani), Barack Majigeh (Dar), na Ben Saanane (Dar).

Wengine ni Benson Ishungisa (Dar), Brighton Amos Emmanuel (Dar), Chande Kizega (Dar), Charles (Dar), Damas Vedastus Bulimbe (Geita), Dastan Gervas Nestory (Geita), David Gasper Lema (Mwanza), Dennis KanTanga (Shinyanga), Dioniz Kipanya (Rukwa), Dioniz Kipanya (Katavi).

Kuna Donald Kalist Mboya (Kagera), Dotto Kabwa (Iringa), Edger Mwakalebela (Dar), Edwin Kunambi (Dar), Enock John Chambala (Tanga), Fred Victor Ledidi (Arusha), Hamza Said (Geita), na Hemed Abass (Dar).

Wamo kina Ilham Makoye (Dar), James Sije (Mwanza), James Taki (Arusha), Jerome Kisoka Mapii (Kilimanjaro), Joel Cremes Lessonu (Arusha), Joseph Jartan (Arusha), Joseph Mnyonga (Mwanza), na Joshua (Iringa).

Pia kuna Kambatai Lulu (Arusha), Karongoi Ingoi Olkedenyi Kanjwei (Arusha), Kastory Kapinga (Mbinga), Kelvin Shaso Nairoti (Arusha), Kennedy Mwamlima (Mbeya), Kombo Mbwana Twaha (Tanga),

Halafu wamo Lekerenga Koyee Orodo (Arusha), Lengaripo Lebahati Lukumay (Mwanza), Leshoko Olojiloji (Arusha), Lilenga Isaya Lilenga (Kigoma),

Lucas Magambo Bulimbe (Geita), Lukas K. Njausi (Arusha), Malongo Daniel Paschal (Arusha), Maseke Mwita Maseke (Mara),

Wengine ni Mathew Eliakimu Siloma (Arusha), Matuki Makuru (Mara), Mohamed Kayego Kalebe (Geita),

Moloimeti Yohana (Arusha), Morongeti Masako Mseeki (Arusha), Mwampyate Herman (Mwanza), Mzee Haji Soft (Dar), Mzee Samuel Mkongo Matiko (Geita),

Kadhalika wamo Ngiminis Parmati (Arusha), Nusra Omari (Dar), Orias Oleng’iyo (Arusha), Orosikiria Laizer (Arusha), Prosiper Theonas Mnjari (Dar), Rajabu Mdoe (Dar), Ridhiwani Hemed Msangi (Iringa), Saing’eu Ndirango Senge Laizer (Arusha), Sangau Morongeti (Arusha), Self Swala (Dar).

Pia walitajwa kina Shadrack Chaula (Mbeya), Shengena Joseph Killel (Arusha), Simeli Parmwati (Arusha), Simon Kanguye (Kigoma), Simon Morintanti (Arusha), Simoni Nairiam (Arusha), Taleng’o Twambei (Arusha).

Na kuna Tawafiq Mohamed (Dar), Theresphora Mwakalinga (Dodoma), Thomas Mungo Ihuya (Mwanza), Wilson Kolong (Arusha), Yahya Ally (Dar), Yonzo Shimbi Dutu (Shinyanga), Yusra Musa (Dar), na Yusuph Dudu (Dar).


1754894974186.png

Padre Kitima, Katibu Mkuu wa TEC​

Ukiukwaji wa misingi ya demokrasia

Takwimu za uchaguzi wa serikali za mitaa kati ya mwaka 2014 na 2019 zinathibitisha kwamba kwa mujibu wa utaratibu wa sasa wa kisheria, kikanuni, kikatiba na wa kiserikali, uchaguzi salama usioambatana na mauaji, ulio huru, wenye uwazi na unaofanyika kwa haki hauwezekani tena kufanyika ktk nchi hii. Takwimu ziko hivi:

(a) Katika uchaguzi wa mitaa na vijiji wa 2014: Jumla ya vijiji vilikuwa 11,748; CCM ilishinda vijiji 9,378 (80%); na CHADEMA vijiji 1,754 (15%). Jumla ya mitaa yote ilikuwa 3,875; CCM ilishinda mitaa 2,583 (67%); na CHADEMA ilishinda mitaa 980 (25.29%).

(b) Katika uchaguzi wa vijiji na mitaa 2019: Jumla ya vijiji ilikuwa 12,262; CCM ikashinda 12,260 (99.99%); na CHADEMA haikutajwa kabisa. Jumla ya mitaa nchini 4,263; CCM ikashinda mitaa 4,263 (100%); na CHADEMA haikutajwa kabisa.

(c) Katika uchaguzi wa vijiji na mitaa mwaka 2024: Jumla ya vijiji ni 12,271; CCM ikashinda vijiji 12,150 (99%); na CHADEMA ikashinda vijiji 97 (0.79%). Jumla ya mitaa ni 4,264; CCM ikashinda mitaa 4,213 (99%); na CHADEMA ikashinda mitaa 36 (0.84%).

Takwimu hizi maana yake ni kuwa, mfumo wetu wa uchaguzi wa sasa unayo matatizo mengi, kiasi kwamba, bila kufanyika kwa mabadiliko ya kisheria, kikanuni na kikatiba, kwanza, basi chaguzi za kiinimacho zenye kuwaumiza wapinzani na kuipendelea CCM zitaendelea milele kwa sababu zilizo wazi.

(a) Mosi, chaguzi za mwaka 2019, 2020 na 2024 zimeweka rekodi za kuenguliwa kwa wagombea wengi wa vyama vya upinzani kwa vigezo visivyo vya kikatiba, mfano kukosea jina, na kukosea kuandika jina la chama. Lakini wagombea wote wa CCM wanabakizwa kwa madai kuwa wao hawana dosari yoyote.

(b) Mfumo wa sasa wa uchaguzi ni mfumo wenye sura ya siasa za chama kimoja. Ulitengenezwa na CCM, kwa ajili ya CCM, unaifaidisha CCM na kwa sababu hiyo si mfumo wa kidemokrasia na unawaumiza wananchi na nchi yote.

(c) Ni mfumo wa CCM kwa kuwa, uchaguzi mkuu unasimamiwa na Tume ya Uchaguzi ambayo ni ya CCM ambayo huteuliwa na kupewa maelekezo na Mwenyekiti wa CCM ambaye mara zote huwa ndiye Rais wa nchi.

(d) Aidha, Mwenyekiti wa CCM ambaye naye mara zote huwa ni mshiriki na mshindani ktk uchaguzi ndiye anayeteua Mwenyekiti wa Tume, wajumbe wote wa Tume na mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume.

Ndiye mwajiri na mteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo (wakurugenzi wa halmashauri za miji, wilaya, manispaa na majiji), watendaji wa kata na wa vijiji. Katika mazingira haya, hawa kamwe hawawezi kutenda haki Bpbali watampendelea aliyewateua.

(e) Mfumo wa ugawaji majimbo ya uchaguzi sio wa haki kwa kuwa hauzingatii idadi ya watu ambao ni wakazi. Maeneo ambayo CCM ina uhakika wa kushinda imeyagawa katika vijimbo vingivingi Ili mradi iingize wabunge wengi bungeni.

Mfano Dar Es Salaam yenye wapiga kura wengi 3,427,000, ambazo ni takwimu za Tume ya Uchaguzi za mwaka 2020, iko sawa na wapiga kura wa mikoa ya Rukwa, Pwani, Songwe, Iringa, Katavi na Njombe kwa pamoja. Lakini DSM ina majimbo 10 tu, sawa na na wastani wa wapiga kura 327,000 kila jimbo la Dar.

Lakini, katika mikoa hiyo sita (6) kwa ujumla ikiwa na majimbo 37, kuna wastani wa wapiga kura 91,000 katika kila Jimbo. Wapiga kura 91,000 katika kila Jimbo kwenye mikoa hiyo ni mara 3.5 ya wapiga kura 327,000 katika jimbo la Dar. Hakuna usawa hapo.

(f) Kwa upande wa Zanzibar, majimbo ya uchaguzi yana wastani wa wapiga kura 10,000. Hii maana yake ni kwamba mbunge kutoka Zanzibar anaweza kuchaguliwa na watu wasiozidi 2,500 akaja Dodoma na akawa na haki sawa na mbunge anayehudumia wapiga kura 327,000 mkoani Dar Es Salaam. Hakuna usawa hapo.

Kwa hiyo, hitimisho ni kwamba, bila Mabadiliko ya kimfumo kwanza, Uchaguzi halali hauwezekani.

Kutokana na hitimisho hapo juu, mapendekezo ya msingi kuhusu mabadiliko yanayotakiwa kufanyika kwa sasa yanapatikana kwenye Ripoti za Tume mbalimbali.

Kuna Tume ya Jaji Francis Nyalali (1991) iliyoundwa na Rais Hayati Ally Hassan Mwinyi; Tume ya Jaji Robert Kissanga (1998) iliyoundwa na Rais Hayati Benjamin Mkapa; Tume ya Jaji Mark Bomani (2003) iliyoundwa na Rais Hayati Benjamin Mkapa; na Tume ya mabadiliko ya Katiba ya Jaji Joseph Sinde Warioba (2014/2015) iliyoundwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Tume hizi zote zilipendekeza mabadiliko yafuatayo:

(a) Lazima tuwe na Tume Huru ya uchaguzi yenye Mwenyekiti na wajumbe wake wanaoteuliwa na mtu baki badala ya Rais; yenye bajeti inayojitegemea kutoka Bungeni kwa ajili ya kuendesha shughuli zake; yenye wafanyakazi wake wa kudumu na wa mikataba ya muda mfupi/maalumu inayowajiri yenyewe wakiwajibika kwa Tume pekee; na yenye wasimamizi wa vituo vya kupigia kura hadi kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na wakurugenzi wa Tume wasiowajibika kwa Rais.

(b) Ugawaji wa majimbo lazima ufanyike upya kwa kuzingatia kigezo cha idadi ya watu kama ilivyokuwa katika sheria za uchaguzi na katiba kuanzia mwaka 1961 hadi 1991. Kigezo cha miumdombinu na jiografia ya eneo hakifai.

(c) Daftari la wapiga kura litengenezwe upya kwa kuandikisha wapiga kura wote upya kwa kuondoa wapiga kura hewa wote.

Aidha, daftari la wapiga kura lisiwe Siri Bali lazima liwe wazi (accessible) kwa yeyote anayetaka kuliangalia Ili mradi kuweka utaratibu rahisi na wa wazi kufanya hivyo.

(d) Utaratibu wa kuengua wagombea wote iwe wa CCM, CHADEMA au chama chochote kwa sababu ambazo si za kikatiba ukomeshwe na kupigwa marufuku na sheria tutakazotunga.

(e) Utaratibu wa vyombo vya dola kuwafanyia vurugu wagombea wa vyama pinzani na CCM upigwe marufuku na sheria na sheria iweke utaratibu wa kuwashitaki, kuwalipisha fidia na kufukuzwa kazi mwenye mamlaka yeyote atakayetumia mamlaka yake vibaya kwenye eneo hili.

(f) Barua rasmi tu ya chama cha siasa ambako wakala anatoka ili kusimamia kura za mgombea wake inatosha kumfanya wakala atambuliwe na msimamizi wa kituo cha uchaguzi.

Hivyo, utaratibu wa Sasa wa mawakala wa wagombea wa vyama vya siasa kuapishwa kiapo cha kutunza siri ni batili na hauna sababu na unaleta urasimu usio na maana yoyote kwa sababu kwenye kituo cha kupigia kura hakuna Siri ya kutunzwa hapo kwa sababu kila kitu kinatakiwa kufanyika kwa uwazi huku kila mtu akiona.

(g) Utangazaji wa matokeo ya uchaguzi kwa nafasi zote kuanzia kwenye kituo cha kupigia kura ufanyike tu pale ambapo mawakala wa wagombea wote wameridhika na kusaini fomu za matokeo.

Kwenye kituo cha majumuisho matokeo yatangazwe pale tu ambapo wagombea wote wameridhika na kusaini fomu ya matokeo.

Kama mgombea au wakala wa mgombea hajaridhika kwa sababu yoyote sheria iseme ni marufuku kwa msimamizi wa kituo kutangaza matokeo hayo. Na ikitokea hivyo, basi mgogoro wa namna hiyo uende mahakamani kuamuliwa.


1754981195572.png
​

Milima, mabonde, makorongo na miiba kwenye uwanja wa kisiasa

Tuhuma kwamba chaguzi zote za 2010, 2015, 2019, 2020 na 2024 zinaonyesha kuwa tunayo mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu, kiasi kwamba, kwa kipindi cha miaka 15, tumekuwa tukiongozwa na serikali haramu zilizotokana na mbinu haramu, nazi zinao ushahidi wa kuziunga mkono kama ifuatavyo:

(a) Uchaguzi unaosimamiwa na ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, na ma-RAS unakosa uhuru, uwazi na ushindani wa kweli, kwa sababu wao ni watumishi wa serikali ya chama tawala, na hivyo kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwa faida ya chama tawala.

(b) Sheria za uchaguzi zinawaruhusu Watumishi wa umma kuvaa kofia za Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati w auchaguzi na hivyo kufungua milango ya uhalifu wa kiuchaguzi.

(c) Tume ya Taifa ya Uchaguzi imo kwapani mwa Rais wa nchi, ambaye ndiye huteua wajumbe wake, na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria pekee kwa sababu ya kuyumbishwa na maagizo kutoka Ikulu.

(d) Tume ya Taifa ya Uchaguzi haina uwezo wa kisheria wala kifedha wa kusimika watumishi wake kwenye kila jimbo la uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

(e) Katiba inamruhusu Rais wa nchi aliye madarakani na ambaye ni mgombea kuendelea kutekeleza majukumu yake ya Urais wakati wa kampeni za uchaguzi ilihali yeye ni Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, na Msimamizi Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Jambo hili linafungua mianya kwa baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama, kama vile Jeshi la Polisi na TISS, kufanya uhalifu wa kiuchaguzi ili kumsaidia “bosi” wao kushinda.

(f) Katiba inaruhusu Rais wa nchi kushika nafasi ya mwenyekiti wa chama cha siasa, kabla na wakati wa uchaguzi, na hivyo, kufungua mlango wa Rais huyu kuvitumia vyombo vya ulinzi na usalama kwa faida ya chama tawala.

(g) Katiba na sheria zetu vinazuia matokeo ya uchaguzi wa Rais yanayobishaniwa kupingwa mahakamani kisheria. Hivyo, uhalifu wa kiuchaguzi kuhusiana na kura za urais hauwezi kukosolewa kimahakama.

(h) Sheria na Katiba havijapiga marufuku tabia ya uhalifu wa kiuchaguzi wa kugeuza mchakato wa uchaguzi kuwa mashindano ya kujaza fomu za wagombea, jambo ambalo linazalisha wagombea wa kupigiwa “kura za ndio au Hapana,” na hivyo kukiuka kanuni ya uchaguzi wenye ushindani.

(i) Sheria ya TAKUKURU chini ya kifungu cha 31 inairuhusu TAKUKURU kuwakamata watu wote wanaotumia madaraka yao vibaya kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Lakini hili halijawahi kutokea kuhusiana na uhalifu wa kiuchaguzi.

Tatizo ni kwamba sheria hiyo inamfanya Mkuu wa TAKUKURU kuripoti kwa Mkuu wa nchi, kabla, wakati na baada ya uchaguzi, bila kujali kwamba kuna wakati Mkuu wa nchi ni mgombea anayeweza kuwazuia watumishi wa TAKUKURU kufanya kazi yao katika namna ambayo itamkwamisha bosi wao mkuu, yaani "Rais ambaye pia ni mgombea."

(j) Sheria ya Jeshi la Polisi inawapa mamlaka polisi kukamata wahalifu wa kiuchaguzi chini ya kifungu cha 21. Lakini hawajawahi kudanya hivyo dhidi ya mkubwa yeyote. Sababu ni kwamba polisi wanawajibika kwa Rais na mgombea Urais wa chama tawala. Hivyo hawawezi kutekeleza jukumu hilo.


1754896400140.png
​

Ratiba ya Sala na Mfungo

Kwa mujibu wa ratiba ilyotangazwa, Jumuiya zote za Kitume ndani ya Kanisa katoliki zinatakiwa kushiriki kikamilifu.

Kuna Kwaya, Viwawa, Uwaka, Wawata na Jumuiya Ndogo Ndogo. Mgawanyo wa majukumu ni kama ifuatavyo:

SAA 2:00—03:00 Asubuhi: Kutakuwepo na matukio mawili.

  • Kwanza ni Misa Takatifu ya ufunguzi “kwa ajili ya kudumisha amani na haki.”
  • Misa hii inapaswa kufanyika kwa kuzingatia utaratibu wa “Misa namba 30,” unaopatikana kwenye kitabu cha Misale ya Kiroma, ukurasa wa 931-932.
  • Kisha litakuwepo tukio la “Kuabudu Ekaristi Takatifu” lengo lake likiwa ni “kuabudu, kuikabidhi nchi yetu ya Tanzania Kwa Mungu.”
SAA 3:00—5:00 Asubuhi: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani:
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu”; na
  • “Maungamo”; na “Mafundisho ya Biblia.”
  • Matukio haya yatakayoongozwa na “Makatekista na Watumikizi.”
SAA 5:00—7:00 Mchana: Kutakuwepo na matukio manne, yaani:
  • “Kuabudu kwa Watoto,” somo kuu likiwa ni “Yesu rafiki wa watoto”;
  • “Sala ya Kuombea haki na amani nchi yetu na nyimbo”; na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu”; na “Maungamo.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Utoto Mtakatifu na Walezi Wao.”
SAA 7:00—9:00 Mchana: Kutakuwepo na matukio manne, yaani
  • “Sala ya Malaika wa Bwana na Rozari Ya Huruma ya Mungu,”
  • “Nyimbo za kusifu na kuabudu Ekaristi Takatifu,” na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu;” na
  • “Maungamo.”
  • Matukio haya yataongozwa na “KWAYA.”
SAA 9:00 Alasiri—11:00 Jioni: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani
  • “Neno la Mungu na Litania ya Bikira Maria”;
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu” na
  • “Maungamo.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Vijana Wafanyakazi Wakatoliki-VIWAWA.”
SAA 11:00 — 12:00 Jioni: Kutakuwepo na matukio manne, yaani,
  • “Tafakari ya Neno la Mungu”;
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu,”
  • “Maungamo”; na
  • “Litania ya Moyo Mt. wa Yesu.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Umoja wa Wanaume Katoliki -UWAKA.”
SAA 12:00 — 2:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
  • “Rozari Takatifu,”
  • “Litania ya Bikira Maria”; na
  • “Ukimya na Maungamo.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Wanawake Wakatoliki Tanzania-WAWATA.”
SAA 2:00 — 4:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio manne, yaani,
  • “Mafundisho juu ya Huruma ya Mungu,”
  • “Litania ya huruma ya Mungu,”
  • “Tafakari ya mateso ya Kristo,” na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu.
  • Matukio haya yataongozwa na “Watawa, Waseminari na Mapadre.”
SAA 4:00 — 6:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
  • “Ukimya na Sala za Kibinafsi,”
  • “Nyimbo za Kusifu na kuabudu Ekaristi Takatifu,” na
  • “Maombi binafsi.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Jumuiya Ndogo Ndogo –JNNK,” Kundi la Kwanza.
SAA 6:00 — 8:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
  • “Neno la Mungu na Litania ya Bikira Maria,”
  • “Litania ya Jina Takatifu la Yesu,” na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Jumuiya Ndogo Ndogo –JNNK,” Kundi la Pili.
SAA 8:00 — 10:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
  • “Ukimya na Kuimba Nyimbo za Ekaristi Takatifu,”
  • “Neno la Mungu na Litania ya Huruma ya Mungu,” na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu.”
  • Matukio haya yataongozwa na Jumuiya za “Moyo Mtakatifu Wa Yesu Na Karismatiki Katoliki.”
SAA 10:00 — 12:00 Asubuhi: Kutakuwepo na matukio manne, yaani,
  • “Neno la Mungu,”
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu,”
  • “Rozari Takatifu na Litania ya Bikira Maria,” na
  • “Sala ya asubuhi na Maandalizi ya Misa.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Jumuiya Ndogo Ndogo –JNNK,” Kundi la Tatu.
SAA 1:30 — 3:30 Asubuhi: Kutakuwepo na tukio moja pekee, yaani,
  • “Misa Takatifu ya Kufunga.”
  • Kwa mujibu wa mwongozo, “siku ya kuhitimisha itaadhimishwa Misa ya Dominika” lakini lazima iwekwe nia ya “kumshukuru Mungu kwa siku hii ya Mfungo na Sala.”

Hitimisho

Kwa sababu ya ubora wa ratiba hii, ni wazi kwamba, mafungo haya yanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kugeuza nyoyo za waumini katika msimu huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Na hapa tusisahau kwamba, sala ni wajibu wa kila Mkristo. Maana tunasoma kwamba, "Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtakaribishwa" (Luka 11:9)

Hivyo, sasa ni wazi kwamba Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limeamua kufuata nyayo za Mtakatifu Fransis wa Assiz, Mwalimi Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania, pamoja na Papa Yohane Paulo II, kuhusu ajenda ya kudumu ya kupigania haki na amani.

Katika sala yake ya kuombea haki na amani, Mtakatifu Fransis (1182–1226), mzaliwa wa Italia, anamwomba Mungu amfanye “chombo cha amani” ili aweze kugeuza chuki kuwa upendo, majeraha kuwa msamaha, mashaka kuwa imani, kukata tamaa kuwa matumaini, giza kuwa nuru, na huzuni kuwa furaha.

Mwalimu Nyerere, mwaka 1961, alizindua Mwenge wa uhuru ili autumie kama alama inayoonekana kuwakilisha ndoto yake ya “kugeuza giza la dhuluma kuwa nuru ya haki” katika Taifa jipya.

Naye Papa Yohane Paulo II, wakati wa ziara zake nchini Poland za mwaka 1979 hadi 1989, alitumia kaulimbiua iliyobeba maneno ya Mzaburi kufanikisha ajenda ya “kuufanya upya uso wa nchi” kwa kuhubiri haki na amani nchini humo.

Mkakati wake ulianzia kwenye maneno ya Zaburi yasemayo kwamba, “
Waipeleka Roho yako Ee Mungu, nawe waufanya upya uso wa nchi.” (Zaburi 104:30).

Huu ndio ujumbe unaosindikiza Mafungo ya Kanisa katoliki kwa ajili ya “Kuomba Haki na Amani” nchini Tanzania utakaohitimishwa tarehe 23 Agosti 2025.

Kwa ufupi, tunaweza kusema kwamba, TEC wanatembea katika nyayo zote hizi.


1754895283755.png

Padre Makubi (kushoto) ​
 

Attachments

Mungu alisema "tuumbe mtu kwa mfano wetu.... " kwa hiyo yanayofanyika sasa yana baraka za Mungu kwa kuwa wanaofanya ni mfano wa Mungu. Ulishajiuliza vita walizopigana Israel na mauaji waliyofanya bado Mungu alikausha? Au Mungu hakuona Nazism ya Hitler? Ukoloni na biashara ya watumwa?kanisa katoliki liliua watu 70,000,000 lakini mpaka leo lipo linakenua meno. Nani hajui kwamba kanisa katoliki ndio wale waliitwa mawakala wa ukoloni (agents of colonialism)?
 
Mungu alisema "tuumbe mtu kwa mfano wetu.... " kwa hiyo yanayofanyika sasa yana baraka za Mungu kwa kuwa wanaofanya ni mfano wa Mungu. Ulishajiuliza vita walizopigana Israel na mauaji waliyofanya bado Mungu alikausha? Au Mungu nakuona Nazism ya Hitler? Ukoloni na biashara ya watumwa?
Maiti wengi wanawaza kama wewe
 
Mungu atujalie tuwe na upendo na huruma kwa wengine. Maana ukweli ni kwamba baina yetu upendo umepoa ndio maana mambo ya hovyo, kuogofya na kutisha yanasikika kila uchao.

Watanzania wamekuwa kama yatima anayeshambuliwa na adui asipate wa kumsaidia anapopiga ukelele wa kuomba msaada.

Waliopewa dhamana ya kulinda na kuitetea haki ya watanzania miongoni mwao wamo chui waliojivika ngozi ya kondoo. Wanatoa amri na maelekezo yenye matokeo ya kuleta simanzi na vilio.

Wapo wanaokula mkate wao wa kila siku na familia zao kutokana na kazi za mikono ya watanzania. Hawa kwa hakika wanatakiwa kuwa na huruma na heshima kwa watanzania lakini badala yake, wao wakipewa amri bila hata kujali kama amri hizo zina tija kwa mjibu wa Sheria, kanuni, taratibu na miiko ya kazi zao, wao hebeba marungu, mabomu ya machozi na mabunduki kama vile wako vitani. Lakini ukiangalia anayebebewa masilaha yote hayo kosa lake ni kuongea au kukosoa tu wale aliowaweka madarakani.

Wapewa amri hao wakati mwingine hutengeneza mazingira ya kuwakomoa walalahoi au kenge ambao hawana mbele wala nyuma.

Zaidi sana siku hizi wapo na hao ambao haijulikani wanatumwa na nani. WASIOJULIKANA. Hawa ni watu wenye mafunzo maalum kutoka kwenye vyuo maalum kwenye nchi isiyojulikana. Hawa wako above all Seculity organs kiuwezo na kiweledi.

Nasema hivyo kwa sababu:

1: WASIOJULIKANA, wamekuwa hawajulikani kwa vyombo vyetu vyote vya Ulinzi na Usalama maana yake wako smart professionally.
2: WASIOJULIKANA wamekuwa wakitekeleza matukio ya utekaji na mauaji kwa raia wasio na hatia bila kuacha unyayo wowote unaoweza kusababisha kukamatwa kwao in the scene au baada ya kutekeleza unyama huo. Wako very smart ndio maana

3: WASIOJULIKANA wamehusika kwenye matukio mengi ya utekaji, utesaji na mauaji Sina sababu ya kutaja matukio hayo maana ni mengi mno lakini yanajulikana. Katika matukio yote hayo vyombo vyetu havijaweza kufanikiwa kuwakama au kiwajua hao WASIOJULIKANA ni akina nani!! Tuombe Mungu atusaidie sana na vyombo vyetu avipe nguvu na uwezo wa kutekeleza wajibu wao ili hofu inayotokana na mambo haya itoweke. Mwananchi asipoishi kwa utulivu na amani, hiyo shilingi anayoipata akulipe wewe kila mwezi ataitoa wapi?
 
TEC: “Ewe Mungu Wetu, Tuma Roho wako, Afanye Upya Uso wa Nchi Kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025” (Zaburi 104:30)
  • Wameandaa Sala na Mafungo ya kuombea haki na amani nchini
  • Watataka “chuki ishindwe na upendo”
  • Watashawishi “kisasi kiuachie nafasi msamaha”
  • Watahimiza “ugomvi ugeuzwe kuwa urafiki.”
Sasa ni wazi kwamba Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limeamua kufuata nyayo za Mtakatifu Fransis wa Assiz, Mwalimi Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania, pamoja na Papa Yohane Paulo II, kuhusu ajenda ya kudumu ya kupigania haki na amani.

Katika sala yake ya kuombea haki na amani, Mtakatifu Fransis (1182–1226), mzaliwa wa Italia, anamwomba Mungu amfanye “chombo cha amani” ili aweze kugeuza chuki kuwa upendo, majeraha kuwa msamaha, mashaka kuwa imani, kukata tamaa kuwa matumaini, giza kuwa nuru, na huzuni kuwa furaha.

Mwalimu Nyerere, mwaka 1961, alizindua Mwenye wa uhuru ili alama inayoonekana kuhusu ndoto yake ya “kugeuza giza la dhuluma kuwa nuru ya haki” katika Tanzania mpya.

Huu ndio ujumbe unaosindikiza Mafungo ya Kanisa katoliki kwa ajili ya “Kuomba Haki na Amani” nchini Tanzania utakaohitimishwa tarehe 23 Agosti 2025.

Naye Papa Yohane Paulo II, wakati wa ziara zake nchini Poland za mwaka 1979 hadi 1989, alitumia kaulimbiua iliyobeba maneno ya Mzaburi kufanikisha ajenda ya “kuufanya upya uso wa nchi” kwa kuhubiri haki na amani nchini humo. Mkakati wake ulianzia kwenye maneno ya Zaburi yasemayo kwamba, “Waipeleka Roho yako Ee Mungu, nawe waufanya upya uso wa nchi.” (Zaburi 104:30).

Tunaweza kusema kwamba, TEC wanatembea katika nyayo hizi. Tarehe 08 Agosti 2025, Sekretarieti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, yenye Makao yake Makuu Jijini Dar es Salaam, imetoa mwongozo wa kitaifa, wenye rejea namba TEC/P/05/08/25 05/08/2025, kuhusu utaratibu wa kutekeleza ratiba ya “Ratiba ya Mfungo Kuomba Haki na Amani Nchini Tarehe 23 Agosti 2025.”

Mwogozo huo unatokana na Barua ya Maaskofu Katoliki ya tarehe 19 Juni 2025 iliyotoa wito wa kuandaliwa kwa siku maalum ya “sala na mfungo” kwa ajili ya kuombea “amani” ambayo ni “tunda” la “haki, usawa, ukweli, mshikamano na ustawi wa wote.”

Pamoja na utaratibu ambao kila Jimbo litajipangia katika kutekeleza wito huo, mwongozo wa sasa unatoa mapendekezo ya kitaifa yatakayotumika kama utaratibu wa kuiadhimisha siku hii maalum kwa sala na mfungo.

Mwongozo huo kutoka Sekretarieti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, umesainiwa na Padre Alister Makubi, Mkurugenzi Wa Uchungaji wa TEC.

Padre Makubi amewaagiza viongozi wa Kanisa Katyoliki nchi nzima kutekeleza mkakati wa Kanisa Katoliki wa kuombea Haki na Amani kwa kutumia mwongozo wa “Misa Namba 30.”

Misa hii inapatikana kwenye kitabu kinachoitwa “Misale ya Waumini,” zu tusema “Misale ya Kiroma,” ukurasa wa 931-932.

Kurasa hizi ndizo zinabeba ujumbe rasmi wa Kanisa Katoliki kwa Waumini wote na Taifa kwa Ujumla. Ujumbe hii umetapaa kwenye salama kadhaa zikiwemo cifuatazo:

  • Sala ya kuanza ibada,
  • Sala ya kuombea dhabihu,
  • Sala ya Ekaristi ya Upatanisho,
  • Wimbo wa Komunyo na
  • Sala baada ya Komunyo.
Sala ya kuanza ibada inabeba maneno yanayomwomba Mungu, awape “amani” wamngojao na ukatuongoze “kwenye nijia ya haki”; kwamba, kwa vile amefunua kwamba “wapatanishi wataitwa wana wa Mungu,” basi asiache mwaka huu upite bila ahadi hii kutumia.

Aidha, Sala ya kuanza ibada inabeba maneno yanayomwomba Mungu atujalie uwezo wa kuimarisha “bila kukoma haki ile ambayo peke yake inaleta kwa uhakika amani ya kudumu na ya kweli”; kwamba, kwa vile anawashughulikia “watu wote kwa wema,” basi awe “radhi kuwajalia wanadamu” aliowapa “chimbuko moja wawe familia moja yenye amani’; na kwamba watu wote “waunganishwe daima kwa roho ya udugu.”

Sala ya kuombea dhabihu inabeba maneno yanayosema kwamba, sadaka ya Misa Takatifu “ambayo inatolewa kwa ishara hizi za sakramenti zinazoonyesha amani na umoja, ifae kwa kazi ya kuimarisha uelewano kati ya wana” wake wote.

Sala ya Ekaristi ya Upatanisho inabeba maneno yanayosema kwamba, “japo familia ya wanadamu imefarakana na kutengana kwa fitina, tumefahamu na kutambua kwamba wewe unaweza kulegeza mioyo, ili watu wawe tayari kupatanishwa”.

Aidha, Sala ya Ekaristi ya Upatanisho inabeba maneno yanayosema kwamba, Mungu ana uwezo wa kuishawishi “mioyo ya watu, ili maadui warejee kwenye mazungumzano, wapiganao wapeane mikono, na mataifa watafute njia ya kukutana kwa amani”; na kwamba, kwa sababu hii, basi, “chuki ishindwe na upendo, kisasi kiuachie nafasi msamaha, na ugomvi ugeuzwe kuwa urafiki.”

Wimbo wa Komunyo unabeba maneno yenye ujumbe kwamba “Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu (Mt 5:9)” na kwamba “Amani nawaachieni, amani yangu nawapa, asema Bwana (Yn 14:27).”

Na sala baada ya komunyo inabeba maneno yasemayo kwamba, “tunakuomba utujalie roho ya mapendo,” ili kwa sababhu hiyo “tustawishe kwa ufanisi kati ya wote ile amani ambayo wewe mwenyewe umetuachia.”

Ratiba ya Sala na Mfungo

SAA 2:00—03:00 Asubuhi
: Kutakuwepo na matukio mawili.

  • Kwanza ni Misa Takatifu ya ufunguzi “kwa ajili ya kudumisha amani na haki.”
  • Misa hii inapaswa kufanyika kwa kuzingatia utaratibu wa “Misa namba 30,” unaopatikana kwenye kitabu cha Misale ya Kiroma, ukurasa wa 931-932.
  • Kisha litakuwepo tukio la “Kuabudu Ekaristi Takatifu” lengo lake likiwa ni “kuabudu, kuikabidhi nchi yetu ya Tanzania Kwa Mungu.”
SAA 3:00—5:00 Asubuhi: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani:
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu”; na
  • “Maungamo”; na “Mafundisho ya Biblia.”
  • Matukio haya yatakayoongozwa na “Makatekista na Watumikizi.”
SAA 5:00—7:00 Mchana: Kutakuwepo na matukio manne, yaani:
  • “Kuabudu kwa Watoto,” somo kuu likiwa ni “Yesu rafiki wa watoto”;
  • “Sala ya Kuombea haki na amani nchi yetu na nyimbo”; na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu”; na “Maungamo.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Utoto Mtakatifu na Walezi Wao.”
SAA 7:00—9:00 Mchana: Kutakuwepo na matukio manne, yaani
  • “Sala ya Malaika wa Bwana na Rozari Ya Huruma ya Mungu,”
  • “Nyimbo za kusifu na kuabudu Ekaristi Takatifu,” na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu;” na
  • “Maungamo.”
  • Matukio haya yataongozwa na “KWAYA.”
SAA 9:00 Alasiri—11:00 Jioni: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani
  • “Neno la Mungu na Litania ya Bikira Maria”;
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu” na
  • “Maungamo.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Vijana Wafanyakazi Wakatoliki-VIWAWA.”
SAA 11:00 — 12:00 Jioni: Kutakuwepo na matukio manne, yaani,
  • “Tafakari ya Neno la Mungu”;
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu,”
  • “Maungamo”; na
  • “Litania ya Moyo Mt. wa Yesu.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Umoja wa Wanaume Katoliki -UWAKA.”
SAA 12:00 — 2:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
  • “Rozari Takatifu,”
  • “Litania ya Bikira Maria”; na
  • “Ukimya na Maungamo.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Wanawake Wakatoliki Tanzania-WAWATA.”
SAA 2:00 — 4:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio manne, yaani,
  • “Mafundisho juu ya Huruma ya Mungu,”
  • “Litania ya huruma ya Mungu,”
  • “Tafakari ya mateso ya Kristo,” na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu.
  • Matukio haya yataongozwa na “Watawa, Waseminari na Mapadre.”
SAA 4:00 — 6:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
  • “Ukimya na Sala za Kibinafsi,”
  • “Nyimbo za Kusifu na kuabudu Ekaristi Takatifu,” na
  • “Maombi binafsi.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Jumuiya Ndogo Ndogo –JNNK,” Kundi la Kwanza.
SAA 6:00 — 8:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
  • “Neno la Mungu na Litania ya Bikira Maria,”
  • “Litania ya Jina Takatifu la Yesu,” na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Jumuiya Ndogo Ndogo –JNNK,” Kundi la Pili.
SAA 8:00 — 10:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
  • “Ukimya na Kuimba Nyimbo za Ekaristi Takatifu,”
  • “Neno la Mungu na Litania ya Huruma ya Mungu,” na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu.”
  • Matukio haya yataongozwa na Jumuiya za “Moyo Mtakatifu Wa Yesu Na Karismatiki Katoliki.”
SAA 10:00 — 12:00 Asubuhi: Kutakuwepo na matukio manne, yaani,
  • “Neno la Mungu,”
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu,”
  • “Rozari Takatifu na Litania ya Bikira Maria,” na
  • “Sala ya asubuhi na Maandalizi ya Misa.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Jumuiya Ndogo Ndogo –JNNK,” Kundi la Tatu.
SAA 1:30 — 3:30 Asubuhi: Kutakuwepo na tukio moja pekee, yaani,
  • “Misa Takatifu ya Kufunga.”
  • Kwa mujibu wa mwongozo, “siku ya kuhitimisha itaadhimishwa Misa ya Dominika” lakini lazima iwekwe nia ya “kumshukuru Mungu kwa siku hii ya Mfungo na Sala.”
Jumuiya zote za Kitume ndani ya Kanisa katoliki zinatakiwa kushiriki kikamilifu. Kuna Kwaya, Viwawa, Uwaka, Wawata na Jumuiya Ndogo Ndogo.

Kwa sababu hii, ni wazi kwamba, mafungo haya yanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kugeuza nyoyo za waumini katika msimu huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Na hapa tusisahau kwamba, sala ni wajibu wa kila Mkristo. Maana tunasoma kwamba, "Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtakaribishwa" (Luka 11:9)
Pale mnapoamua kuchanganya dini na siasa
 
Kuna namna Waislamu nao wanapasws kujiandaa kwa ajili ya kugawana hii nchi, ni dhahiri TEC wamedhamilia kabisa kumuonea na kumdhulumu Haki yake ya kuongoza huyu mama. Hilo liko wazi kabisa na yule polepole ni mtu wao wanayemuwezesha na kumpa jeuri ya kufanya anayofanya......kinachokera hawana sababu nyingine zaidi ya udini.
 
Back
Top Bottom