ABC ZA 2025
JF-Expert Member
- May 2, 2018
- 1,299
- 832
Rais Samia kupitia mitandao yake ya kijamii ameandika haya kumpongeza Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa
Pongezi za dhati kwa Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa, Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC). Kuchaguliwa kwako katika nafasi hii ya uchungaji kwa Kanisa Katoliki nchini ni matokeo ya imani na matarajio ya Kanisa kwa utumishi wako.
Nanukuu maneno mawili toka katika Biblia Takatifu kwenye Injili ya Yohana 19:28, “...Naona kiu” ambayo pia uliyachagua kuwa kaulimbiu yako ya Uaskofu. Katika utumishi huu nakuombea kiu ya kuendelea kufanya kazi ya kujenga Kanisa kwenye misingi ya upendo, haki, kweli, kujali masikini, umoja, amani, mshikamano, utu na kuhudumia jamii na Watanzania kwa ujumla, ndani na nje ya Kanisa Katoliki.
Nakutakia kila la kheri. Mwenyezi Mungu akushike mkono na kukuongoza.