Pre GE2025 TEC ni chombo cha kidini au ni chama cha kisiasa kisicho rasmi?

Pre GE2025 TEC ni chombo cha kidini au ni chama cha kisiasa kisicho rasmi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbona huulizi wanapojenga shule, hospitali, vyuo vyaufundi na vikuu, n.k. wananchi wanakosa huduma bora kulifanya kanisa lotumie rasilimali zake kutoa huduma hizo, sababu ni mfumo mbovu wa kisiasa. Hivyo wameamua na wao(ni sehemu ya raia) kutaka mambo yakae sawa ili kupunguza mzigo kwa kanisa.
Hayo haulizi,,,,kaka jana nimeenda na shemeji yako government hospital huwezi amini ultrasound ya hospital haifanyi kazi ikabidi wanidirect hospital ya roman afu ndo nitoke. Navipimo kule niwaleteee
 
Nafungua maswali na uzi wangu kwa nukuu hii" KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA".

Hivi hili Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ni chombo cha kidini au ni chama cha kisiasa kisicho rasmi?

Kwa nini mijadala mingi na mambo mengi ya kisiasa wanakuwa nayo kimbelembele kuyazungumzia na kuyatolea matamko na waraka lakini mambo yao ya kidini yanayo husisha masuala kadha wa kadha yenye mikanganyiko wanaficha vichwa ndani ya mashuka na kukaa kimya kama hawajui chochote kile?

Kwani nini TEC isisajiliwe rasmi na kujulikana chama cha kisiasa official kuliko haya maigizo yanayo endelea?
Katoliki ni Mvumbuzi wa Mifumo ya Utawala Duniani.
Baraza la Maaskofu Katoliki halihitaji usajili wowote
 
Wewe ni mkomunisti ?
Ukomunisti haukatai ukwell unaopingana na ujenzi wa tabaka la walionavyo na walała hoi! Kila anapinga matabaka yu pamoja nasi. Wapo wanaojiita Wakomunisti lakini wanajenga usultani kwa kuwarithisha watoto wao madaraka uwaziri ukuu wa wilaya n.k. na kuwaacha watoto wa wengine kuzurura kila mahali na bahasha kubwa za kaki wakitafuta ajira hata za kujitole!
 
Mbona huulizi wanapojenga shule, hospitali, vyuo vyaufundi na vikuu, n.k. wananchi wanakosa huduma bora kulifanya kanisa lotumie rasilimali zake kutoa huduma hizo, sababu ni mfumo mbovu wa kisiasa. Hivyo wameamua na wao(ni sehemu ya raia) kutaka mambo yakae sawa ili kupunguza mzigo kwa kanisa.
Kwani wanatoa huduma bure?
 
Ukomunisti haukatai ukwell unaopingana na ujenzi wa tabaka la walionavyo na walała hoi! Kila anapinga matabaka yu pamoja nasi. Wapo wanaojiita Wakomunisti lakini wanajenga usultani kwa kuwarithisha watoto wao madaraka uwaziri ukuu wa wilaya n.k. na kuwaacha watoto wa wengine kuzurura kila mahali na bahasha kubwa za kaki wakitafuta ajira hata za kujitole!
Mkomunisti na support ya dini na siasa. Mkomunisti uchwara

Dini si ndio moja ya mambo yanayo tengeneza matabaka ya wanyonyaji au hata vitu alivyokuwa anapinga Karl Marx huvijui

Wewe ni dini gani ewe mkomunisti uchwara?
 
Nafungua maswali na uzi wangu kwa nukuu hii" KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA".

Hivi hili Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ni chombo cha kidini au ni chama cha kisiasa kisicho rasmi?

Kwa nini mijadala mingi na mambo mengi ya kisiasa wanakuwa nayo kimbelembele kuyazungumzia na kuyatolea matamko na waraka lakini mambo yao ya kidini yanayo husisha masuala kadha wa kadha yenye mikanganyiko wanaficha vichwa ndani ya mashuka na kukaa kimya kama hawajui chochote kile?

Kwani nini TEC isisajiliwe rasmi na kujulikana chama cha kisiasa official kuliko haya maigizo yanayo endelea?
Kwani TEC hawalipi kodi? wakisifia mbona mnafurahia? kazi ya kanisa ni kulinda maslahi ya wananchi. Wajinga wakubwa nyie
 
Mnaleta propaganda?

Mnataka walolala (wananchi) usingizi wa pono waendelee kulala?

Mwenyezi Mungu huwa kuna namna anaamua kuingilia kati.
 
Faiza. Kanisa lina uzoefu wa zaidi ya miaka 1000 pale wanapokaa kimya hali mbaya ikajitokeza. Vita ikijikeza watu hukimbilia kanisani tena kanisa katoliki. Hivyo wameamua kutosubiri kipokea wakimbizi bali kuzuia hali mbaya kwa gharama yeyote ile.
Aisee kuhusu vita labda umesahau waliokimbilia kutafuta hifadhi wakachomwa mule mule na kuuwawa kanisani kwenye vita ya Hutu na Tutsi
Ukiona vita kimbia au pigana
 
Huelewi wabarikiwa wanavyokuwa kimbelembele kila sehemu?

Kitu cha kwanza ambacho wabarikiwa wanaondolewa ni haya, hawana haya hao wala hawajuwi vibaya.
Acha uhayawani we ustazati dini inapaswa kujali mwili na roho ndomana dini zamaana zinajenga shule,hospitali,vituko vya yatima nk. nk.
Kunadini mnamiliki mapepo na waganga kutwa nikuchomeana ubani kuamsha maruhani hamna shule za maana,hamna miradi ya maji,hamna hospitali tunawabeba sana so ilitakiwa mtuheshimu!!
Leo serikali ikifanya upuuzi lazima iambiwe maana hatuna unafiki, hata marehemu magu aliambiwa aache ujinga kuhusu Korona... ikamdinya!!!
Tatizo hamna shule mnafunika vichwa na akili pia badala ya kuwaza maendeleo mnawaza visomo ndomana miji ya pwani imezubaaa isipokuwa Ile ambayo "wabarikiwa" wameingia na kuibariki.
Wekelea heshima webinti au hujafundwa bado?
 
TEC ni Taasisi pekee iliyo na viongozi wenye maono ya nchi na sio chawa wa kujipendekeza. Wanaoishtumu TEC hawana hoja ya kupingana nao, ila kutetea na kutaka kuuendeleza usułtani wa chama kile. Ukweli wake unawatishia sana mafisadi na madalali wa nchi hii! Ukisikia kelele gizani ujue jiwe limewapata🫢🫢🫢
Waambie mkuu hasa wale wanaochagua waganga wa kienyeji kuongoza taasisi za dini/madhehebu yao!
 
Mbona hauulizi Bakwata?
Acha kufananisha BAKWATA na TEC! BAKWATA wao wameamua kujinasibisha na CCM moja kwa moja, umeona wapi TEC wakifanya hivyo? wao wanatoa maoni kama taasisi inayoaminiwa na kuongoza sehemu moja wapo ya watanzania. Uwe unatafakari kabla ya kuandika!
 
Mkomunisti na support ya dini na siasa. Mkomunisti uchwara

Dini si ndio moja ya mambo yanayo tengeneza matabaka ya wanyonyaji au hata vitu alivyokuwa anapinga Karl Marx huvijui

Wewe ni dini gani ewe mkomunisti uchwara?
Elimu duni! Uelewa wa kiujima ukaririshwaji wa dhana endelevu wa mambo ndio unaofanya utukane badala ya kujibu hoja. Mjadala nawe nimeufunga kwani unaulewa mdogo wa mambo kufanya nawe dialogue !
 
Back
Top Bottom