Uchaguzi 2020 TEF yamaliza Mgogoro wa TBC na CHADEMA, wapeana Mkono

Salaam Wakuu,

Baraza la Wahariri Tanzania (TEF) limemaliza Mgogoro kati ya Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Hivi Karibuni CHADEMA iliwafukuza TBC kwenye Mkutano wao baada ya kuwa wanawakatia sauti kwenye Ufunguzi wao wa Kampeni.

Baadaye TBC wakatoa tamko kusitisha kuonesha habari za CHADEMA hadi watakapojirekebisha na kuwahakikishia usalama wa Wafanyakazi wao.

=====

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) leo Ijumaa Septemba 4, 2020 limefanikiwa kumaliza mgogoro uliokuwapo kati ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Shirika la Habari la Utangazaji Tanzania (TBC), baada ya kuwakutanisha viongozi wakuu wa taasisi hizo jijini Dar es Salaam, leo Ijumaaa Septemba 4, 2020. TEF kupitia kwa Kaimu Mwenyekiti wake, Deodatus Balile ilifanya mawasiliano na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayubu Ryoba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Willison Mahera Charles, ambao wamekutana leo katika ofisi za NEC jijini Dar es Salaam kumaliza mgogoro huo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Mahera, wakati anafungua kikao hicho cha usuluhishi, amesema vyombo vya habari vya umma vinawajibika kutoa fursa sawa kwa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 53(2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2010, sambamba na Maadili ya Uchaguzi, Katiba ya Tanzania, Sheria mbalimbali na maelekezo ya Tume. Pia amesema vyama vya siasa na wafuasi wao wanawajibika kutii sheria za nchini kwa kuhakikisha wanalinda amani na utulivu. Amevitaka vyama vya siasa kuepuka kutoa tuhuma zisizo na uthibitisho kwenye mikutano ya kampeni.

Katika mkutano huo Mwenyekiti wa TEF, Balile ameeleza umuhimu wa vyombo vya habari kushirikiana na vyama vya siasa kwa kutimiza wajibu wake wa kitaaluma, lakini pia akafafanua umuhimu wa vyama vya siasa kushirikiana na vyombo vya habari hasa kipindi hiki cha kampeni kupata fursa ya kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya sera za vyama vyao katika majukwaa ya siasa. Amevitaka vyama kukosoana bila kutumia lugha ngumu au kuingia katika ugomvi binafsi na watu au matusi hali inayovipa wakati mgumu vyombo vinavyorusha matangazo ‘live’.

Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ryoba amelishukuru Jukwaa la Wahariri kwa juhudi za kuikutanisha TBC na Chadema, ila akaeleza masikitiko yake kuwa uamuzi wa Chadema kufukuza waandishi wao katika mkutano wa ufunguzi wa Kampeni, Mbagala wiki iliyopita ulikuwa unahatarisha maisha ya waandishi na mali za shirika. Pia amesema hatua ya Chadema ililenga kubomoa kiwango cha TBC kuaminika mbele ya jamii, suala ambalo ni gharama kubwa kwa chombo cha habari. Hata hivyo amekiri upungufu uliofanywa na watangazaji siku hiyo kwa jinsi matangazo yaliyokatwa na mjadala ulioendelea studio, hivyo akasema shirika litajitahidi kutorudia makosa yaliyojitokeza.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameeleza historia ya uhusiano wa TBC na Chadema kwamba kwa muda mrefu umekuwa si mzuri na akasema hata baadhi ya vyombo vya habari binafsi vinakataa kurusha matangazo ya shughuli za chama chao hata kama kinalipia kwa maelezo kuwa vimepewa maelekezo. Mbowe ameviomba vyombo vya habari kufanya kazi kwa weledi na kwa mujibu wa sheria, hasa katika kipindi hiki cha kampeni.

Baada ya mjadala mrefu, Dk. Ryoba na Mbowe walikubaliana kumaliza tofauti zao kwa kupeana mikono na kuahidi kurejesha ushirikiano. Mbowe amesema atawatangazia wanachama wa Chadema kuwa wako tayari kufanya kazi na TBC kuanzia sasa. Dk. Ryoba amesema Chadema wawapatie TBC ratiba ya mikutano yao watashiriki kikamilifu kuitangaza. Pia, amemwabia Mbowe kuwa TBC ina kipindi cha nusu saa kila wiki kwa wagombea kunadi sera zao kinachorushwa bila malipo, hivyo akawaalika Chadema kuitumia fursa hiyo, ambapo Mbowe amekubali kuitumia.

Akifunga kikao, Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Mahera aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, ameishukuru TEF kwa juhudi ilizofanya kuwakutanisha TBC na Chadema na akaviomba vyama vya siasa nchini kufanya kampeni za kistaarabu kwa kutambua kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi. Dk. Ryoba, Mbowe, Dk. Mahera na Balile wamepeana mikono kuashiria kufungua ukurasa mpya na wakaahidi kumaliza migogoro kati ya vyombo vya habari na vyama vya siasa au wanasiasa nchini kwa njia ya mazungumzo badala ya kutegemea sheria pekee katika kipindi hiki cha uchaguzi.

IMETOLEWA NA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF) DAR ES SALAAM, SEPTEMBA 4, 2020

NEVILLE MEENA

KATIBU

View attachment 1558585View attachment 1558604View attachment 1558605View attachment 1558607View attachment 1558608
Hongera sana mh Mbowe kwa kuwatimua hao wanoko wa ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hamna option DStv ya kuondoa channel ya TBC maana inajizia foleni tu!
 
TBC ijirekebishe, wasidhani kuwa ni TV ya chama cha mapinduzi, bali TV ya watanzania wote yenye wajibu wa kuzipa taasisi zote halali za wananchi nafasi ya kuonekana na kusikika!

Kuna tatizo na ninyi mnaoshabikia CHADEMA. Kama chama kina haki zote za kisiasa. Lakini, mnashindwa kutofautisha haki na wajibu wa chama na wa viongozi wake. Chama kitakuwepo milele lakini viongozi wanabadilika.

Viongozi wa sasa hivi wa CHADEMA, bila kumung'unya maneno si wanasiasa wala wanaharakati. Kwa kauli na matendo yao ni wahuni. Kwa mfano mgombea wao wa Urais na Mgombea Mwenza, kwenye mikutano yao yote ya kampeni, hawamalizi bila vitisho kwa viongozi wa Serikali na Vyombo vyake (TRA, vyombo vya ulinzi, mahakama, nk) vilivyoundwa kikatiba. Kama wanaweza kuvibeza hawajapata madaraka, wakipewa madaraka, ni dhahiri kuwa watavitumia kwa maslahi yao binafsi.

Kwa sababu hiyo, nina uhakika makubaliano ya viongozi hao na TBC ni wa mashaka kama ambavyo Mkuu Missile of the Nation unavyodai TBC ijirekebishe, wasidhani kuwa ni TV ya chama cha mapinduzi. Haya ni mawazo hasi nje ya utu.
 
Ila Mbowe hua ana busara za kidwanzi sana,sasa amewalegezea hao jamaa ili iweje sasa wkt wataendelea na utaratibu wao huo huo

Jino kwa jino ilikua ndio mpango mzima.
alikosea ,alitakiwa akomae mwanzo mwisho ,maana Ryoba alivyoongea ni kama wao ndo wanapata hasara ya kuleta taswira mbaya kwa jamii.Mbowe alitakiwa awakazie
 
Kuna tatizo na ninyi mnaoshabikia CHADEMA. Kama chama kina haki zote za kisiasa. Lakini, mnashindwa kutofautisha haki na wajibu wa chama na wa viongozi wake. Chama kitakuwepo milele lakini viongozi wanabadilika.

Viongozi wa sasa hivi wa CHADEMA, bila kumung'unya maneno si wanasiasa wala wanaharakati. Kwa kauli na matendo yao ni wahuni. Kwa mfano mgombea wao wa Urais na Mgombea Mwenza, kwenye mikutano yao yote ya kampeni, hawamalizi bila vitisho kwa viongozi wa Serikali na Vyombo vyake (TRA, vyombo vya ulinzi, mahakama, nk) vilivyoundwa kikatiba. Kama wanaweza kuvibeza hawajapata madaraka, wakipewa madaraka, ni dhahiri kuwa watavitumia kwa maslahi yao binafsi.

Kwa sababu hiyo, nina uhakika makubaliano ya viongozi hao na TBC ni wa mashaka kama ni Mkuu Missile of the Nation unavyodai TBC ijirekebishe, wasidhani kuwa ni TV ya chama cha mapinduzi. Haya ni mawazo hasi nje ya utu.
huo ushauri wako niwa mihemko na chuki kwa chadema kwahiyo haufai kaa chini sahizi na familia yako usome kwa sauti kama hata watoto wako hawajakupiga makofi akili ikae sawa
 
Haina haja ya kuwarushia matangazo? Hiyi jeuri mnaitoa wapi? wakati hata online Media hamna imeparalyse , kila siku mnakilalamikia kitengo chenu cha habari hapa

Pilipili usizozila zinakuwasha je jombi?

"Why do you keep poking your nose onto issues of no concern to yourself?"

Kazi kweli kweli.
 
Mbowe nae, kwani lazima wapatanishwe? Angewapotezea tu hawatajirekebisha maana kupatana kwao wamelazimishwa na TEF
 
huo ushauri wako niwa mihemko na chuki kwa chadema kwahiyo haufai kaa chini sahizi na familia yako usome kwa sauti kama hata watoto wako hawajakupiga makofi akili ikae sawa
Kwa lugha na wazo lililomo kwenye jibu lako hakika umewakilisha sawasawa uhuni wenu
 
ushauri wangu ufanyie kazi usilete bangi zako hapa siyo kijiwe cha wahuni
 
TBC wajanja sana.

Wanataka kufutilia mbali picha za kuchonga si watakuwa live.
 
Twende mbele turudi nyuma bila ccm kung'oka madarakani hali itakua ile ile
 
Salaam Wakuu,

Baraza la Wahariri Tanzania (TEF) limemaliza Mgogoro kati ya Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Hivi Karibuni CHADEMA iliwafukuza TBC kwenye Mkutano wao baada ya kuwa wanawakatia sauti kwenye Ufunguzi wao wa Kampeni.

Baadaye TBC wakatoa tamko kusitisha kuonesha habari za CHADEMA hadi watakapojirekebisha na kuwahakikishia usalama wa Wafanyakazi wao.

=====

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) leo Ijumaa Septemba 4, 2020 limefanikiwa kumaliza mgogoro uliokuwapo kati ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Shirika la Habari la Utangazaji Tanzania (TBC), baada ya kuwakutanisha viongozi wakuu wa taasisi hizo jijini Dar es Salaam, leo Ijumaaa Septemba 4, 2020. TEF kupitia kwa Kaimu Mwenyekiti wake, Deodatus Balile ilifanya mawasiliano na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayubu Ryoba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Willison Mahera Charles, ambao wamekutana leo katika ofisi za NEC jijini Dar es Salaam kumaliza mgogoro huo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Mahera, wakati anafungua kikao hicho cha usuluhishi, amesema vyombo vya habari vya umma vinawajibika kutoa fursa sawa kwa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 53(2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2010, sambamba na Maadili ya Uchaguzi, Katiba ya Tanzania, Sheria mbalimbali na maelekezo ya Tume. Pia amesema vyama vya siasa na wafuasi wao wanawajibika kutii sheria za nchini kwa kuhakikisha wanalinda amani na utulivu. Amevitaka vyama vya siasa kuepuka kutoa tuhuma zisizo na uthibitisho kwenye mikutano ya kampeni.

Katika mkutano huo Mwenyekiti wa TEF, Balile ameeleza umuhimu wa vyombo vya habari kushirikiana na vyama vya siasa kwa kutimiza wajibu wake wa kitaaluma, lakini pia akafafanua umuhimu wa vyama vya siasa kushirikiana na vyombo vya habari hasa kipindi hiki cha kampeni kupata fursa ya kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya sera za vyama vyao katika majukwaa ya siasa. Amevitaka vyama kukosoana bila kutumia lugha ngumu au kuingia katika ugomvi binafsi na watu au matusi hali inayovipa wakati mgumu vyombo vinavyorusha matangazo ‘live’.

Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ryoba amelishukuru Jukwaa la Wahariri kwa juhudi za kuikutanisha TBC na Chadema, ila akaeleza masikitiko yake kuwa uamuzi wa Chadema kufukuza waandishi wao katika mkutano wa ufunguzi wa Kampeni, Mbagala wiki iliyopita ulikuwa unahatarisha maisha ya waandishi na mali za shirika. Pia amesema hatua ya Chadema ililenga kubomoa kiwango cha TBC kuaminika mbele ya jamii, suala ambalo ni gharama kubwa kwa chombo cha habari. Hata hivyo amekiri upungufu uliofanywa na watangazaji siku hiyo kwa jinsi matangazo yaliyokatwa na mjadala ulioendelea studio, hivyo akasema shirika litajitahidi kutorudia makosa yaliyojitokeza.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameeleza historia ya uhusiano wa TBC na Chadema kwamba kwa muda mrefu umekuwa si mzuri na akasema hata baadhi ya vyombo vya habari binafsi vinakataa kurusha matangazo ya shughuli za chama chao hata kama kinalipia kwa maelezo kuwa vimepewa maelekezo. Mbowe ameviomba vyombo vya habari kufanya kazi kwa weledi na kwa mujibu wa sheria, hasa katika kipindi hiki cha kampeni.

Baada ya mjadala mrefu, Dk. Ryoba na Mbowe walikubaliana kumaliza tofauti zao kwa kupeana mikono na kuahidi kurejesha ushirikiano. Mbowe amesema atawatangazia wanachama wa Chadema kuwa wako tayari kufanya kazi na TBC kuanzia sasa. Dk. Ryoba amesema Chadema wawapatie TBC ratiba ya mikutano yao watashiriki kikamilifu kuitangaza. Pia, amemwabia Mbowe kuwa TBC ina kipindi cha nusu saa kila wiki kwa wagombea kunadi sera zao kinachorushwa bila malipo, hivyo akawaalika Chadema kuitumia fursa hiyo, ambapo Mbowe amekubali kuitumia.

Akifunga kikao, Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Mahera aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, ameishukuru TEF kwa juhudi ilizofanya kuwakutanisha TBC na Chadema na akaviomba vyama vya siasa nchini kufanya kampeni za kistaarabu kwa kutambua kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi. Dk. Ryoba, Mbowe, Dk. Mahera na Balile wamepeana mikono kuashiria kufungua ukurasa mpya na wakaahidi kumaliza migogoro kati ya vyombo vya habari na vyama vya siasa au wanasiasa nchini kwa njia ya mazungumzo badala ya kutegemea sheria pekee katika kipindi hiki cha uchaguzi.

IMETOLEWA NA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF) DAR ES SALAAM, SEPTEMBA 4, 2020

NEVILLE MEENA

KATIBU

View attachment 1558585View attachment 1558604View attachment 1558605View attachment 1558607View attachment 1558608
Huyo ndo mwamba mbowe, tibisii wameona cdm watakuwa ikulu soon wameona waombe pooooo
 
Kuheshimiana muhimu sana , umesikia wewe bwana Bulile
 
Back
Top Bottom