Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Wakamatwe wote waliojichotea fedha zetu warejeshe zote. Hayo malipo kwa SCB yatatoka humo
 

Hapo inachanganya kidogo, ina maana kiuhalisia TANESCO hana cha kulipa hapo bali kampuni ya PAP (Pan Africa Power Solutions Tanzania Ltd) ya Mr. H. Singh Sethi ndiyo inatakiwa kuilipa SCB-HK.

Sasa hawa gazeti la ''The Guadian'' kutuwekea kichwa cha habari TANESCO ordered to pay $148m over IPTL dispute kama cha magazeti-pendwa kuwa TANESCO wameshindwa kesi na itabidi walipe deni siyo sahihi ila gazeti la the Guardian wamefanya mbinu kuuza magazeti mengi !

Na mwisho naomba ufafanuzi (kwa faida ya wanaJF), katika mikataba ya kiuwekezaji/kibiashara kimataifa, sheria gani inatiliwa mkazo zaidi kuliko zote (inayofuatwa / take precedence) ni sheria ya nyumbani (Mahakama Kuu ya Tanzania) au sheria ya Kimataifa?
 
Hukumu inahusu TANESCO kulipa $148 millioni. TANESCO walishakusanya pesa taslimu $75 millioni ambazo ziliibwa na mafisadi na kugawana kama njugu huku wakitetewa na Kikwete kwamba zile pesa ni halali ya wale majizi Rugemarila and Co.

Bila shaka Kikwete alinufaika na pesa zile ndiyo sababu akawakingia kifua na kama mtakumbuka kulikuwa na rumours zilizozagaa nchini wakati ule kwamba kuna mke wa kigogo kashikishwa mgao wa kati ya bilioni 2 mpaka 5 lakini mke wa kigogo huyo wa Ikulu hadi hii leo hajulikani ni nani.

Serikali iwakamate mara moja wezi wote wa pesa za escrow, wanyang'anywe passport za kusafiria warudishe kila senti waliyopora toka TANESCO na wataje mali zao ndani na nje ya nchi na bank accounts zao zote ndani na nje ya nchi ziwe frozen na Serikali ili kuhakikisha Serikali inakusanya haraka iwezekanavyo $75 miilioni zilizoibwa na mali za wahusika zifilisiwe ili kuziuza na kuhakikisha hiyo pesa inapatikana haraka iwezekanavyo. Pia wezi wa pesa zile na waliopokea pesa za wizi wakiwemo Chenge, Tibaijuka, Ngeleja na wengine wote wapandishwe kizimbani haraka sana, kama nchi itatikisika bora na itikisike ili kukomesha hawa wahuni na majambazi. Management na Board of Directors waiambie Serikali kwamba wao watalipa $73 millioni tu.
 

Mkuu kuna sheria. Lakni zaidi,mkuu wa nchi alishawahi kusema kuwa escrow sio hela za serikali.
Lakini cha ajabu watu walichukua pesa kwa magunia na kwenda kusikojulikana.
 
Hiyo ndio agenda yao kama taifa hiyo SCB-HK parent company ni SCB-UK wao wanachotaka watambulike kama wamiliki wa IPTL balozi (wa UK) keshatumia nguvu sana kulazimisha hii agenda na wanapofungua kesi za madai huko wanafungua kama wamiliki wa IPTL ndio maana mahakama inaweza toa hizo ruling. Na hakuna anaetaka kujua their legal ownership huko wanapofungua.

Ata wewe kesho ukienda kufungua partnership company kuna vigezo vyake vinavyokutambulisha wewe na huyo partner mwingine huko BRELLA kupitia partnership deed, mfano how partnership comes to an end other than in natural legal aspects kama death, each partners rights; etc with what was drafted in the partnership deed.

Sasa ikitokea mmbia mwenzako kaenda kuchukua mkopo kwa jina la kampuni (which is disputable) halafu baadae huyo mdeni anadai wewe aupo tena na yeye kutumia deni ndio mmiliki mpya. Wewe si utasema hapana nipe deni nilipe mimi sikutambui wewe na wala sheria aimtambui kwenye deed of ownership. Hapo ndio mzozo wa umiliki wa IPTL ulipo mahakama imeamua kwakuwa Rugemalira anatambulika kama mmoja wa mmbia na karidhia kuuza partnership rights zake kwa PAP kwa hivyo PAP ndio mmiliki mpya.

Pamoja na hayo mahakama pia imemtaka PAP kama mmiliki mpya wa IPTL akija mdeni wowote wa IPTL au TANESCO amalizane nae. Wao IPTL awaja kataa deni lilioachwa na mmbia mwingine na wako tayari kulilipa isipokuwa mdeni ataki malipo ya deni yeye anachotaka ni umiliki kamili wa IPTL kwa vigezo gani vya sheria ndio ataki kuja Tanzania anakimbilia huko kwa wazungu wenzake.
 
Kikwete hana utaalamu wowote ule wa mambo ya pesa kuliko Wataalam wa TRA, CAG na BoT ambao wote walithibitisha kwamba pesa zile ni za umma

Mkuu kuna sheria. Lakni zaidi,mkuu wa nchi alishawahi kusema kuwa escrow sio hela za serikali.
Lakini cha ajabu watu walichukua pesa kwa magunia na kwenda kusikojulikana.
 
Eric Cartman, ungekuwa unafanya preview kidogo kabla ya kubonyeza send ingesaidia sana...ni ushauri tu.
 

Mkuu,
Basi katika masuala haya ya kitaalamu unaweza kutupia kila kitu 100% kwa kutumia ''plain english'' naamini asilimia kubwa tutakuelewa. Maana tunataka kufahamu kwa undani na usahihi suala hili kwa kuwa vyombo vingine vya kupashana habari Tanzania hakuna ''uhuru'' wa kujieleza, kuchangia mawazo au kuulizwa kama humu JamiiForums.
 
If I have to hakuna shida matter of fact shughuli zangu za kila zina involve kuandika kwa kizungu na believe me huko zinapoenda zinarudi well written work na kigezo moja wapo kutumia lugha za kitaaluma; but then I have to check and edit tatizo hapa sina muda.
 
Kimenuka,Tundu lisu alisema kuna kesho ya tanesiko,na bank ya stands chat ya China,na akataharisha kuwa tukiahindwa kesi tutalipa mabilion ya pesa
 
Kimenuka,Tundu lisu alisema kuna kesho ya tanesiko,na bank ya stands chat ya China,na akataharisha kuwa tukiahindwa kesi tutalipa mabilion ya pesa
Published on 27 Nov 2014
Tundu Lissu ameibuka na kuijia juu ripoti iliyotolewa na Waziri Muhongo kuhusu fedha za Escrow akidai ni ya uongo na akaenda mbali kwa kuwataja wahusika.
Source: Said Ebraim
 
Published on 27 Nov 2014
Tundu Lissu ameibuka na kuijia juu ripoti iliyotolewa na Waziri Muhongo kuhusu fedha za Escrow akidai ni ya uongo na akaenda mbali kwa kuwataja wahusika.
Source: Said Ebraim
Subiri uone kitakacho fuata ndio utajua jamaa mropokaji tu
 
Wale wazee wa 'vijesenti vya ugoro' na 'pesa ya mboga' ndio wakalipe.., sio kutiana umasikini namna hii
Nilisikia upo mchakato wa kuanzisha mahakama ya ufisadi(mafisadi) pia nilimsikia "mtu" mmoja akisema yeye hajaribiwi. Ukitilia maanani hayo mawili, hili sakata la "kutiana umasikini namna hii" unalionaje?
Hii sio kujaribiwa kweli?
Hawa jamaa wanamjaribu au wanachezea sharubu za paka?

Hili kampuni "la kutoza ada ya kuzalisha umeme" kukomba milioni 400!? kwa siku, kila siku ni utapeli au ufisadi?

Milioni 400 kila siku, kwa miaka 2 unajenga viwanda vingapi?

Juzi walisema serikali ina fedha za kutosha na uchumi haujasinyaa, sasa wajanja wanazitaka hizo fedha.
Kila unapotaka kushangaa,unapigwa na butwaa.

Shamba la bibi, business as usual.
 
FLASHBACK:

Published on 26 Nov 2014

Kashfa ya TegetaEscrow inazidi kufukuta nchini Tanzania. Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) leo aliwasilisha ripoti ya uchunguzi katika bunge la nchi hiyo. Katika matangazo ya Dira ya Dunia TV, Zuhura Yunus alimhoji mbunge huyo kujua zaidi.
ZITTO AKIHOJIWA NA BBC DIRA TV KUHUSU TEGETA ESCROW
Source: Swahili Buzz
 
SIYO MAKOSA YA NCHI ZA SOUTH, NI VIONGOZI WETU. KILA CONTRACT IN DEAL NDANI YAKE, MAWAKILI WANAPIGA DEAL WAPATE MKATO WAO. TANZANIA YA KIKWETE ILIKUWA IMEOZA.

Ile siku anahutubia wale wazee pale dar ,alivyokuwa anababaika , aliposema pesa si za umma nilikuwa nimeshika soda mkono nikatetemeka ,ikaanguka ,
Halafu kuna wapinzani wanamkumbuka huyu jamaa wakati kila mtu alitamani amalize muda wake aondoke pesa chafu chafu ndo watu wanazililia kwa sasa
 
Mungu wangu! deni analodaiwa kila mtanzania linazidi kupaa, limeishatoka kwenye 1.2m limesogea mbele ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…