Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Hivi yule Mwanasheria mkuu wa Serikali kazi yake kupambana na kila Lisu tu bungeni, dahh serikali ikate Rufaa na mawakili wa chadema walifanyie kazi hili
 
Hiki kitu kilichotokea kwa serikali kulipa PAP sio kitu cha bahati mbaya, seriklai ilijua kabisa huwezi lipa PAP wakati huo kuna kesi mahakamani kati ya serikali na SCB-HK, hili lilikuwa ni dili ambalo walilisuka wao wenyewe, hii nchi ya kijinga sana, wakalipa dol mil 200 kwa PAP( haya ni malipo Hewa), leo tena wanaamuliwa kulipa dol mil 148.4 over Bil 300 za kitanzania, bado hao waliolipwa ile pesa ya ESCROW wapo, yule mhindi yupo, watu wa serikali na viongozi walio fanya huu ujanja ujanja hadi malipo yakafanyika kwa PAP wapo, ilitakiwa baada ya habari hii kupatikana serikali ingekuwa imeshamkamata huyu mhindi na wenzake wote haraka ili wasikimbie, lakini tunabaki wote tunashangaa tu. Haiwezekani watu wapige bil 300+ tukawaacha hivi hivi, huu ni wizi wa karne.
 
Tuliambiwa ELIMU,ELIMU,ELIMU. Taifa kukosa wanasheria wapambanaji,inaligharimu Taifa.
 
Hivi kwanini serikali na Tanesco huwa hawashindi hata kesi moja? Itokee basi washinde hata kikesi kimojawapo Uchwara, dah!

Mara hii wamepata pigo jengine katika mgogoro wao wa kisheria wa muda mrefu dhidi ya Kampuni ya IPTL ambapo sasa wanatakiwa kulipa benki ya Standard Chartered -Hong Kong jumla ya dola za Marekani milioni 148.4(takribani sh.bilioni 320/- za TZ).

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa Baraza la Usuluhishi la Benki ya Dunia kutoa hukumu ya kulipwa kwa fedha hizo ambazo zinajumuisha na riba ya deni la tozo ya uwekezaji.

Uamuzi huo umekuja miaka mitatu tangu serikali iruhusu kitatanishi kufanyika kwa malipo ya dola milioni 200(sh.bilioni 440) kutoka akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) kwenda kampuni ya Pan Africa Power Solutions (T) Ltd ya Harbinder Singh Sethi.

Chanzo: Gazeti la Nipashe leo tar.19/9/2016
 
Nakumbuka gavana aliweka shariti la PAP kulipa gharama zozote zitakazoibuka kabla ya kuruhusu hela zile kutolewa na PAP walikubali sasa naishindwa kuelewa iweje leo TANESCO ndio wadaiwe au ulikuwa ni usanii tu na kutuhadaa watanzania?

Au baada ya hukumu hiyo ndio sasa Serikali /TANESCO wambane PAP alipe gharama hizo?
 
Tanesco hawakuruhusu zile hela zitoke wale waliosema hazikuwa fedha za umma wanajua wahusika ni kina nani
 

Umesema wote lakini umemsahau aliekua pale kwenye jengo jeupe.
 
Deni hatutalipa , wafanye wafanyavyo , wananchi fanyeni kazi , deni hilo halikusababishwa na serikali .
 
Tanesco hawakuruhusu zile hela zitoke wale waliosema hazikuwa fedha za umma wanajua wahusika ni kina nani
.....sasa hapo JPM ndio ana mtihani...maana waliokwapua zile pesa wanajulikana....wamewalipa PAP na VIP kwa makosa pesa za St. chartered bank (HK)...

.....waanze na BoT walioruhusu hela kutoka..na utaona hiyo bil.320+ ndio kiasi cha pesa za escrow zilizochotwa...hizi hela zilibarikiwa zitoke kuanzia juu ......hapo ndipo JPM ana mtihani....ifike mahali sasa aanze na hili la escrow...aache kushughulika na vidagaa wasio na impact kwenye kukua kwa nchi...
 
Nooooo... noooooo...omg..!!

Nooo, nooo over my dead body... Nooo... noooo...!!

Hapanaaaaaa... hatulipiiiiiii, hakunaaaaaaa... jamaniiii, sasa basi... Mh. Rais Magufuli, hili na uhakika kufa na kupona, na sbb nampenda sanaaa mh. Rais kwa uzalendo wa 10000% juu ya nchi yetu, hili atakataaaa...!! Tusiwe tunaibiwa hivi na wazunguuuu..!

I feel pain, naumiaaaa, moyo unaniumaaa, i feel pain & very angry..!! Naumiaa, tutaibiwa hadi liniiiii....? naumia, naumia, nchi yangu Tz utaibiwa hadi liniiii...? naumia, naumia...!!

Mh. Rais wangu Magufuli, hili kataaaa, kata kataaaa...!!

Unyonge na uwizi wa kisheria, uhuni, sasa basiii...

Watukomeee, tutawamaliza, no... noooo... oohh shit..!!
 
Mnatamani sana Serikali ipandishe bei ya umeme ili muwe na ajenda majukwaani. Mmeula wa chuya. Hilo halitarokea kwa utawala wa Rais Magufuli
hahahaa ndugu yangu wewe utakuwa umetumwa sio bure.. hivi kuna mtu mwenye akili timamu atakayefurahia bei ya umeme kupanda ukilinganisha na hali ya leo ya uchumi jinsi ilivyo ngumu? tufike mahali tuache siasa za ushabiki na kuwa wazalendo maana hili tatizo litakuathiri wewe pia
 
Kwa akili yako unamuona ni nani wa kurudisha hizo pesa? Acha tuendelee kukamuliwa kwenye bili ya umeme usishangae ile service charge ya kila mwezi ikarudi tena
..we akili yako finyu huwezi hata kusoma na kuona nani wanatakiwa kurudisha hizo pesa....pamoja na scandal yote kuibuka mwaka jana bado hujui nani wa kulipa...usaidiweje we sasa....
 
Nchi imekuwa ya moto sasa, huko mtaa wa magogoni hakuna usingizi, yaani najalibu kuwaza tu:-
1; Deni la taifa kwa sasa tirioni 50
2: IPTL bilioni 320
3; China tirioni 16....

Watanzania lazima tule nyasi kipindi hiki......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…