Hiki kitu kilichotokea kwa serikali kulipa PAP sio kitu cha bahati mbaya, seriklai ilijua kabisa huwezi lipa PAP wakati huo kuna kesi mahakamani kati ya serikali na SCB-HK, hili lilikuwa ni dili ambalo walilisuka wao wenyewe, hii nchi ya kijinga sana, wakalipa dol mil 200 kwa PAP( haya ni malipo Hewa), leo tena wanaamuliwa kulipa dol mil 148.4 over Bil 300 za kitanzania, bado hao waliolipwa ile pesa ya ESCROW wapo, yule mhindi yupo, watu wa serikali na viongozi walio fanya huu ujanja ujanja hadi malipo yakafanyika kwa PAP wapo, ilitakiwa baada ya habari hii kupatikana serikali ingekuwa imeshamkamata huyu mhindi na wenzake wote haraka ili wasikimbie, lakini tunabaki wote tunashangaa tu. Haiwezekani watu wapige bil 300+ tukawaacha hivi hivi, huu ni wizi wa karne.